Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,215
- 3,587
Kuna mkanganyiko mkubwa nchini katika utoaji taarifa za deni la taifa. Kuna usemi kuwa miluzi mingi huchanganya mwelekeo wa Mbwa.
Ndugai ni Spika, Balile ni Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Luoga ni Gavana, sasa nani ana taarifa sahihi za kutufanya tumuamini?
Ndugai amesema deni la taifa ni 70 tr, Balile (Gazeti la Jamhuri October 26, 2021) alisema ni 78 tr, Luoga anasema liko 27.9% halijafikia hata nusu ya kiwango cha kukopa.
Lipumba naye huenda akaibuka na takwimu zake, Mbatia naye anajifua kufanya uchunguzi ili aje Ki-NCCR, Tundu naye ataibuka kivyake. Baghosha!
Kwa mkanganyiko huu kama hauna sababu za kisiasa basi huenda mtu akatamani enzi ya Magufuli ya kudhibiti utoaji takwimu, kwa sababu kama nchi, tunatia aibu duniani, tunajipaka matope wenyewe, tunaonekana hatuna mifumo mizuri ya kitakwimu, utoaji taarifa nyeti, wala kumbukumbu sahihi za deni la taifa.
Hivi unawezaje kumlipa mdeni wako kama hujui kiasi sahihi anachokudai?
Magufuli alisema kazi ya urais ni ngumu, Nyerere alisema Ikulu ni mzigo, JK alisema Ikulu ni sawa na kulalia kitanda chenye kunguni wengi.
Kwa upande wa Ndugai, nadhani kauli yake imethibitisha kwamba ameamua kufanyakazi ya Msemaji Rasmi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (simjui ni nani).
Msome Balile hapa:
Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78 | JamiiForums
Msome Ndugai hapa:
Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai | JamiiForums
Gavana yeye alitoa ufafanuzi wake jana Jumatano Disemba 29, 2021 kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachoendeshwa na Redio ya Clouds FM. (nimetafuta clip nimeikosa).
Taswira zote kwa hisani ya google.