Neno La Leo: Kikwete Ni Kama Mungu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kikwete Ni Kama Mungu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Feb 5, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180


  Ndugu zangu,

  Ni Jumapili nyingine. Nina neno. Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kagera , Dk. Methodius Kilaini ameongea na mwandishi wa gazeti la Mwananchi leo Jumapili, Februari 5, 2012.


  Askofu Kilaini ameulizwa juu ya kauli yake ya miaka ya nyuma alipokaririwa akitamka, kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Je, Kikwete ni chaguo la Mungu?


  Askofu Kilaini anajibu; ” Nilichosema ni kwamba, sauti ya watu ni sauti ya Mungu”. Anajibu Askofu Kilaini na kufafanua; kwa vile Rais alichaguliwa na asilimia 80 ya watu, hivyo, amekubalika na watu. Anasema Askofu Kilaini.

  Askofu Kilaini anatuleta kwenye mantiki hii; kuwa Kikwete ni kama Mungu, na hapa kwa vile Katiba yetu ya sasa nayo inampa nguvu nyingi Rais, basi, ni nguvu zinazoweza kufanana na za Mungu.

  Na Askofu Kilaini anatamani tutawaliwe na ’ dikteta’ ili mambo yetu yanyooke. Ndio, Askofu Kilaini amekaririwa na gazeti la Mwananchi la leo Jumapili akitamka; kuwa ili nchi isonge mbele, inahitaji kiongozi atakayeongoza kwa ’ mkono wa chuma’. Amemtaja Rais Paul Kagame kama mfano wa aina hiyo ya kiongozi.


  Natumaini Askofu amenukuliwa vibaya na mwandishi, lakini, kama alichosema ndicho, basi, natumaini hakumaanisha alichosema. Na kama amemaanisha alichosema, basi, napingana vikali na mafundisho hayo ya Baba Askofu Kilaini.

  Maana, nchi yetu inachohitaji ni kiongozi na si mtawala. Anayetumia ’ mkono wa chuma’- Iron Feast huyo anatawala, haongozi. Huyo atakuwa ni dikteta na si kitu kingine.

  Ndio, mtawala anayetumia ’ mkono wa chuma’ hutumia pia risasi za shaba kuwanyamazisha wanaopingana nae, hata kwa hoja tu. Samahani Askofu Kilaini, Watanzania tungependa tupate kiongozi na si mtawala. Na tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha kuwa na mtawala anaendesha nchi kwa ' mkono wa chuma'.


  Na Kikwete huyu tuliye naye walau ameonyesha uongozi kwa kutamani Tanzania ije kupata kiongozi. Ni kwa kupitia mabadiliko haya ya Katiba tunayokwenda kuyafanya. Na ndio maana, hata ndani ya chama chake kuna wanaojipanga kupingana nae ili azma ya Kikwete kufanikisha mabadiliko makubwa ya Katiba ya nchi ishindikane.


  Na ni matumaini yetu, kuwa Rais Jakaya Kikwete atatumia nguvu hizi za mfano wa Mungu alizopewa na Katiba ya sasa katika kuhakikisha Bunge linapitisha marekebisho ya sheria ya kuanzisha mchakato wa Katiba kama alivyoshauriwa na wadau nje ya CCM na akaafikiana nao.


  Hakika, Rais Kikwete atakuwa mtu wa ajabu kama ataendekeza matakwa ya wachache wasiotaka mabadiliko ndani ya chama chake na hivyo basi, kujinyima mwenyewe nafasi yake katika historia ya nchi hii. Maana, Kikwete huyu anaweza kuacha nyuma yake, kumbukumbu ya kudumu ’ Legacy’ ya kuwa ndiye Rais wa nchi, baada ya miaka 50 ya uhuru, aliyefanikiwa kuwafanya Wazanzibar kuendesha siasa zisizo na chuki miongoni mwao, lakini, aliyefuta pia ubaguzi wa kisiasa kwa Tanzania bara. Ni kwa kuwezesha kuwepo kwa Katiba mpya ambayo, bila shaka, itasafisha njia ya kuwepo , mbali ya mambo mengine, kipengele kitachoruhusu kuundwa kwa Serikali ya Mseto kama ilivyo kwa visiwani.


  Naam, Kikwete wa sasa amekuwa ni kiongozi anayejitahidi sana kupima upepo. Huenda ameshabaini , kuwa Watanzania walio wengi, ni wale asilimia 80 anaosema Askofu Kilaini, kuwa ni wenye kutaka mabadiliko. Ndio, sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Anasema Askofu Kilaini.


  Hivyo basi, na Kikwete bila shaka anajua , kuwa CCM ni mkusanyiko wa wanachama milioni tano tu kati ya Watanzania milioni 40. Na kama Mungu, kama wananchi walio wengi wanataka mabadiliko ya kimfumo kupitia Katiba. Basi, anapaswa kusikiliza sauti za wengi, hata kama wako nje ya chama chake.


  Na kama walio wengi wanatoa sauti za kupinga ongezeko la posho za wabunge. Rais anapaswa kusikiliza sauti za wengi. Kwamba anaweza kuacha ’ kubariki’ ongezeko la posho na umma ukabaki nyuma yake. Maana, sauti za wananchi zapaswa kuwa sauti ya Rais, kwa mantiki ya Askofu Kilaini. Ndio, Rais asipobariki ongezeko la posho za wabunge bado atabaki na ’ waumini’ wengi tu.


  Na je, wenzake ndani ya chama wakiamua kupiga kura ya kukosa imani na Kikwete?  Astaghafillulahi! Hebu tema mate chini usije fikwa na laana. Hilo haliwezekani kamwe. Si tulimsikia Beatrice Shelukindo akipendekeza hilo kwa wabunge wenzake wa CCM juzi kule Dodoma. Akasimama Mbunge Ole Sendeka na kumtamkia Shelukindo; ” Futa kauli yako!” Na Shelukindo akasimama haraka na kukubali kufuta kauli yake. Naam. Kikwete ni kama Mungu. Na yawezekana hataki Rais ajaye awe kama yeye. Kama hivyo ndivyo, basi, Mwenyezi Mungu ashukuriwe.


  Kuna wakati , miaka ya mwanzoni mwa uhuru, Julius Nyerere alipata kumwambia mwandishi wa habari wa Kimagharibi; ” Rais Afrika n i mtu mwenye nguvu sana. Akikohoa tu. Waliomzunguka watashtuka na kunong’onezana kwa kusema; ” Bwana mkubwa amekohoa!”.


  Ndio, Rais Afrika anaweza kuamka asubuhi na kuamua kufanya chochote anachotaka, hata kama kutaifisha mashamba na nyumba za watu. Rais yuko juu ya kila kitu.


  Na Katiba yetu ya sasa inasema , mbunge anapovuliwa uanachama wa chama chake anapoteza sifa ya kuwa Mbunge. Lakini, hakuna mahali popote kwenye Katiba panaposema , kuwa Rais anapovuliwa uanachama wa chama chake, kuwa anapoteza sifa ya kuwa Rais. Hivyo basi, kimsingi, Rais anaweza kuhama chama chake, akaingia chama kingine na akabaki kuwa Rais, kwa mujibu wa Katiba ya sasa.


  Naam, haiyumkini kwa ’ waumini’ kumvua Mungu mamlaka yake. Lakini, waumini wanaweza kujitenga au kutengwa na Mungu wao. Mungu hawezi kukosa waumini wapya . Na waumini wale waliojitenga au kutengwa na Mungu wao wanaweza kuzibiwa njia ya kwenda peponi, na Mungu wao.


  Hakika, tunahitaji Katiba Mpya itakayotunusuru na balaa la siku moja kuamka na kukuta tuna mtawala anayetumia ’ mkono wa chuma’. Ni Katiba mpya itakayotusaidia kumpata kiongozi mkuu na viongozi wa kumsaidia kiongozi mkuu katika kuliongoza taifa letu n a si kulitawala. Na hilo ni Neno la Leo.


  Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

  Maggid Mjengwa
  Dar es Salaam,
  Jumapili, Februari, 5, 2012
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  What do you people take God for?
  upuuzi huu,this is too much insult to God.
   
 3. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjengwa, wewe kweli humuogopi MUNGU na kumfananisha na wenye dhambi?
  Tubu dhambi hii na kama si hivyo itakuandama mpaka hukumuni.
  Yu aja upesi, na kila jicho litamuona Mwokozi, naam, yu aja tena.
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mjengwa's arrogance @ work
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huwezi jua,labda mungu anae muabudu yeye ni kikwete au
  anafanana na kikwete.

  Kilaini alisema "kikwete ni chaguo la Mungu",....eti kisa kachaguliwa na watu wengi.

  Kilaini sio malaika,he was and he is still wrong.
  Hakuna sehemu kwenye biblia inasema kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
  Huu ni msemo tu umetungwa na wanasiasa wezi na watu wanafiki wanao tumia
  maneno hayo kuhadaa wenzao.

  Biblia inasema njia ya Mungu ni nyembamba na wapitao huko ni wachache.


  Kumfananisha **** na Mungu ni upungufu wa akili,....tena ni kulewa mafanikio
  na kudhani unaweza kumuita au kumfananisha Mungu na chochote na usipatwe na lolote.
   
 6. rifwima

  rifwima JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Yaani huyi kiazi mbatata Jakaya Mrisho Kiwete ndo awe MUNGU!!!!
   
 7. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh................be carefuloh
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Soma vizuri hiyo makala.
   
 9. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mjengwa unaleta ushetani sasa,kumumlinganisha Mungu na kikwete ni kudhihirisha ushetani ndani yako. Kusema Kikwete ni chaguo la Mungu inaweza kuwa sahihi ila kusema ni kama Mungu apo mjengwa unapindisha maneno ya mzee kilaini ili kudhihirisha uendawazimu wako. Muache Mungu aitwe Mungu..
   
 10. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi yule mke wako wa Kizungu na watoto wako wale nao ni Mungu,kama Kikwete jambazi ni Mungu.
   
 11. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Sema mungu mmoja,hakuzaa wala kuzaliwa na hafanani na chochote!!!
   
 12. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  MUNGU hafananishwi na kitu chochote kile....wala nguvu zake hazilinganishwi na chochote kile

  atakalo na hua at the right time.....so huu ni upungufu wa imani ya huyo Mjengwa na aliesema eti ni chaguo la mungu ili bidi huyu ASKOFU ajiuzuru kwa upupu wake huu....Kama huna cha kuzungumza na ukajiona unaweza kuzungumza mbele ya watu wenye akili ndo mwanzo wa pumba km hizi za KILAINI he just talks nonsense ata km hana cha kuzungumza.......
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  wewe mwandishi ndo unayetaka tuamini hivyo

  .....sijui unadhani Mungu ni wa kumfananisha tu...
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  sii kweli kwamba kauli ya wengi ni kauli ya Mungu. Huu msemo ni kauli mbiu ya freemasons kuitawala dunia nje ya mapenzi makamilifu ya Mungu. Msemo huu ungekuwa kweli basi ungeibatilisha kauli ya Bwana Yesu kwamba, njia ya kuuingia ufalme wa Mungu ni nyembaba na watakaouingia ni wachache, tofauti na ufalme wa shetani ambao alisema ndio utakuwa na majority.
  .
   
 15. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Masikini wana JF wote waliochangia hawajamuelewa Mjengwa. So much for the alleged Great Thinkers.
  Read without prejudice!
   
 16. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kilaini mropokaji kama ndugu yake Bana
   
Loading...