Ndugu zangu,
Tuna wajibu wa kizalendo kuzuia nchi yetu isigeuzwe kuwa Jamhuri ya Migomba.
Maana, ilivyo sasa, tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi wakiwa na matarajio ya kuvuna utajiri wa haraka kwa kufanya biashara na uchumi wa nchi ili kujinufaisha wao binafsi na makundi yao ya wizi, badala ya kuunufaisha umma.
Wameigeuza nchi kuwa ‘Banana Republic’- Jamhuri ya Migomba.
Kwenye siasa Jamhuri ya Migomba ina maana ya nchi ambayo baadhi ya viongozi na watendaji wake wanafanya biashara na uchumi wa nchi kwa maana ya kutumia vibaya madaraka yao na hivyo kufanya biashara na rasilimali za nchi badala ya kuzilinda na kuhakikisha zinawasaidia wengi.
Tanzania Should Never Be A Banana Republic.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)