asanteHi wana Jf MMU, tunaongea habari nyingi sana, mikasa ya mapenzi,ugomvi na kadhalika.Nimeona sio mbaya pia niwakumbushe wote leo ni jpili si vibaya tukakumbushana Kusali, kutoa kwa maskini, na kupendana , kujamiiana na kusameheana jumapili ya leo. nimeamua kushare na nyie hili cause leo tumefundishwa na tumeambiwa tuwaambie na wenzetu misingi ya maneno hayo hapo juu.
Katika hayo yote mie nimeamua niongelee kutoa kwa maskini na wasiojiweza, watu wengi tunasahau kwamba maisha haya tunayoishi leo inaweza kuwa kwa yule kesho kwetu. hivo basi tujifunze kutoa kusaidia kadri tuwezavyo, kwani kutoa sio utajiri au kwamba unacho sana.Tusiwasahau wazazi wetu kwani bila wao leo hii tusingekuwepo. Inasikitisha kuona mtu anaweza kutumia pesa hovyo bila mpangilio ila linapokuja kutoa msaada kwa wazazi tunajisahau sana.Tuwapende wazazi wetu na kuwaonyesha kwamba bila wao sisi si kitu.Mzazi ni Mungu wa pili wa kila binadamu.
Nakupenda Ivuga Jumapili jema
Hi wana Jf MMU, tunaongea habari nyingi sana, mikasa ya mapenzi,ugomvi na kadhalika.Nimeona sio mbaya pia niwakumbushe wote leo ni jpili si vibaya tukakumbushana Kusali, kutoa kwa maskini, na kupendana , kujaliana na kusameheana jumapili ya leo. nimeamua kushare na nyie hili cause leo tumefundishwa na tumeambiwa tuwaambie na wenzetu misingi ya maneno hayo hapo juu.
Katika hayo yote mie nimeamua niongelee kutoa kwa maskini na wasiojiweza, watu wengi tunasahau kwamba maisha haya tunayoishi leo inaweza kuwa kwa yule kesho kwetu. hivo basi tujifunze kutoa kusaidia kadri tuwezavyo, kwani kutoa sio utajiri au kwamba unacho sana.Tusiwasahau wazazi wetu kwani bila wao leo hii tusingekuwepo. Inasikitisha kuona mtu anaweza kutumia pesa hovyo bila mpangilio ila linapokuja kutoa msaada kwa wazazi tunajisahau sana.Tuwapende wazazi wetu na kuwaonyesha kwamba bila wao sisi si kitu.Mzazi ni Mungu wa pili wa kila binadamu.
Nawapenda nyote Jumapili jema
We mtoto hujatulia wewe hivi umeenda kusali kweli
Siku ya mwisho itakukuta hivohivo umelala ukiamka unakuta wenzio wote tumenyakuliwa
Huendi kokote labda baharini kwa shostito
sio kweliUtaendaje na wakati umeng'ang'na na wa pande ingine? si unajua huyo kule haingii hata kwa mtutu
kwa hiyo unabisha au? yan utaingia na huyo mgeni wako kule kwa baba?
Mimi Ivuga ndo kanimaliza,yaani alivyopindisha na kuchakachua post ya Gaga,mmmhh Ivuga we mwisho wa njia kama ni barabara we ni Chalinze- Tanga!
Gaga ahsante mama tutafuata ushauri.