Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Hekima haifundishwi popote! Kazi ya msingi ya chuo kikuu chochote ni kufundisha, tafiti, na ushauri. Nani duniani humu amewahi kufikia "Hekima ya Sulemani"? Alisomea chuo kikuu kipi kuipata hekima ile? UDSM ijikite kwenye majukumu yake ya msingi badala ya kuambatana na siasa uchwara!
Hakuna mwanadamu anayezaliwa na hekima.Hata sulemani hakuzaliwa na hekima.Ndio maana hata Mungu kwenye biblia amesema wazi "mtu akipungukiwa na hekima na aombe" kwa hiyo hekima inapatikana baada ya kuzaliwa na wala si kuzaliwa nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... na wala hekima haifundishwi darasani. Tuko pamoja.
 
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:

Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.

Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.
Hapo ni jalalani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahaha Wengi mtaani wanasemaga ni freemason mara blah blah kibao..

Skia ni ivi...

Wakati wana waisraeli walivyo kua Safarini kuelekea nchi ya Ahadi mnakumbuka Kuna kisanga kilitokea pale Musa akaambiwa achukue nyoka amtundike mtini iwe kama ishara ya Uponyaji na Kila aliye Mtizama Kwa imani ya Kupona Alipona na Kuishi

HES. 21:8-32

Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi
Kwani hizi nembo waasisi wake hawaweki maana zake kama kumbukumbu? Hiyo yako imekaa kidini sana
 
hakuna haja ya kubadili slogani Ya hekima ni uhuru.Ni kweli kuwa hekima haifundishwi popote lakin Hekima inapatikana kutokana na mambo mbalimbali kwa pamoja.Mojawapo ni elimu,malezi ya wazazi na jamii inayotuzunguka.Miaka ya 2010 kurudi nyuma chuo hiki kilikuwa mstari wa mbele kufanya hekima itamalaki.Lakini siasa za majitaka zikajitungia sheria za kuwabana wanaUDSM kuendesha tena ile midahalo ya wazi ambayo ilikuwa inachochea maarifa ndio maana hata serikali kwa kutambua hilo katika sh.Mia5 noti wakaweka ukumbi wa Nkurumah kutokana na hekima iliyokuwako pale.Watu walitoa maoni kwa uhuru kabisa.
Cha kufanya ni rais ajaye kurusisha tena midaharo vyuoni ili wajadili changamoto zinazoikabili nchi ili zipatiwe fumbuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya mambo tunahoji hayana logic yoyote.......anyway sisi WaTz ujuaji umezidi sana wakati hatujui
Kweli kabisa Mkuu, badala ya kuwaza jinsi ya kutengeneza kombola linalo pangua na kung'oa kabisa ma- Bomu ya Nuclear na wataam wote beba, peleka pasipo julikana. Ili

Tukapige hela ndefu huko Tel aviv.
lazima litakuwa na soko na tutaishi vizuri.yeye anawaza vitu vidoogo sana.

Haoni fursa huyu dogo. Vilaza watasema aaaaah! Iwezekani. Wakati yesu alisema, nothing impossible under the Sun.
 
Kwa muktadha wa maelezo yako unaonekana uliwahi kwenda shule, lakini haijakusaidia. Badala ya kuangalia hoja na hitaji la mtoa mada wewe unakimbilia kwenye mrengo wa siasa na kudhalilisha watu. Yeye alitoa dukuduku lake lililohitaji maelezo au majibu. Kama huna jibu ya nini kum-attack mtoa hoja? Una matatizo gani? Kama unafahamu hata mambo ya GPA unashindwaje kudhibiti mihemko yako? Nini tatizo lako? Wewe katika maisha sharti ujue kuna kutofautiana. Watu wotw hawawezi kuwa CCM wale CUF kwa wakati mmoja. Huoni wengine walikuwa Chadema na sasa ni CCM na kinyume chake? Unatakiwa ukue kiakili
Toba, nakimbilia ktk siasa wakati hoja nzima alikuwa anauliza siasa na taaluma naona uwezowenu wa kufikiri wewe na yeye na mawazo yenu na nia zenu ni moja sasa nitawasaidiaje mimi. Ndiyo maana nikasema hamtaishia hapo mtaende ktk bendera ya taifa mtataka irekebishwe, mtaenda katika ngao ya taifa mtataka irekebishwe,
Na si kama hatuwajui mwnge wa uhuru mmeupinga, kuamia dodoma mmepinga, ununuzi wa ndege mmepinga, elimu bure mmepinga ndiyo nikamalizia na Benjamini William Mkapa WAPUMBAFU na MALOFA ktk UBORA WAKE sasa ninatatizo gani mimi kukupiga kwa ulofa wenu.
 
Naomba nitofautiane na wewe; lengo la msingi la chuo kikuu ni kupata KNOWLEDGE not WISDOM! Ni kupata MAARIFA sio HEKIMA! Hakuna mahali popote darasani uliwahi kukaa ili ufundishwe HEKIMA; tunaingia darasani kupata MAARIFA. Huwezi kuniambia wote ambao hawajafikia elimu ya chuo kikuu au ambao hawajasoma (darasani) kabisa hawana HEKIMA!

"Where is the wisdom we have lost in knowledge? Where is the knowledge we have lost in information?" —T.S. Eliot. Knowledge is gathered from learning and education, while most say that wisdom is gathered from day-to-day experiences and is a state of being wise. Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.
Kudos!
I second u!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa hamna vitu vya kufanya vikawaletea maendeleo?? nembo ni nembo tu siyo mission na vission ya taasisi
 
wewe una tatizo gani?Mwenge ni moto ni mwanga,hekima ni uhuru.Nembo ya UDSM ina maana sana kuliko hio uliyoweka ya TUMA.Sema kwa sababu uelewa wako ni mdogo unataka upewe vitu laini.Sioni tatizo la nembo naona tatizo la uwezo wako wa kuelewa mambo
 
Ngoja tuweke kwa kizungu huenda utaelewa na tutajua kama kuna siasa au ni abstract message imewafanya musielewe ujumbe mzito katika hiyo motto sijui tuite Slogan.

HEKIMA NI UHURU = "WISDOM IS FREEDOM".
Jiulize lengo la kutafuta elimu au maarifa pale chuo kikuu ni nini?
Jiulize hekima inapatikananje kama haujazaliwa nayo?
Jiulize hekima inaleta uhuru wa nini au kwa namna ipi?

Huo ni ujumbe mzito sana kuliko akili ya kawaida. Ni Abstract art, ni philosophical message.

Kwa kuanzia tu kujibu hayo maswali nakuambieni mnaodhani hiyo ni siasa.
Hekima huleta uhuru wa fikra.
Hizo fikra ndio hutumika kwenye hizo tafiti, kutoa huduma,kutoa elimu yenye manufaa kwa jamiii, n.k.
Kwa hivyo utaona ujumbe wa kwenye nembo ya Tumaini University upo ndani ya Ujumbe wa nembo ya UDSM.
Ni sehemu moja tu ya ujumbe mkubwa uliopo ktk nembo ya UDSM.

Hekima huleta uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuhoji, uhuru kufanya chochote bila kuvunja sheria, Uhuru wa kuchagua kitu unacho amini, uhuru wa kutafuta ukweli(tafiti), uhuru wa serikali kutoingiliwa na dini, n.k.

Mwenge ni alama ya uhuru(a torch is a universal symbol of freedom), kwa kesi hii ya chuo kikuu ni uhuru wa kifikra.
Tunaona uhuru wa kifikra huleta uhuru wa kila kitu kuanzia wa maoni , udadisi, uhuru wa kutafuta maarifa, uhuru wa kutafuta ukweli sio kwa hisia bali kwa kuegemea majibu ya tafiti(facts based in research ), uhuru wa kiuchumi, kutenganisha dola na dini, n.k.

Ni kama vile wamarekani walivyo tumia alama ya mwenge kwenye sanamu la uhuru ile sanamu yao inaitwa kwa kimombo The Liberty Statue.
Lile sanamu limeshika mwenge.
Watu hawaangalii movie,movie nyingi za wenzetu haswa za kiintelejensia wanatumia philosophy message kuweza kufanikisha mambo yao na kama utakuwa sio mtambuzi hutoelewa kabisa kama huyo jamaa asivyoweza kuelewa maneno yaliyoandikwa kny log hiyo. Binafsi nimekuelewa vizuri sana, watu wengine wanapenda kuleta mada kwa kusingizia ipo kisiasa kumbe wao ndio wanaleta usiasa huku.
 
Hekima haifundishwi popote! Kazi ya msingi ya chuo kikuu chochote ni kufundisha, tafiti, na ushauri. Nani duniani humu amewahi kufikia "Hekima ya Sulemani"? Alisomea chuo kikuu kipi kuipata hekima ile? UDSM ijikite kwenye majukumu yake ya msingi badala ya kuambatana na siasa uchwara!

Nyie wenye diploma wasumbufu sana

Kwa hiyo kww akili zako suleimani hakuwa na elimu na alikuwa kizazi cha royal family?

Tangu Musa anasoma shule, iwe suleiman? Au elimu yako wewe lazima iwe formal? Na kutoa degree???

Suleiman alifundishwa tamaduni, madawa, historia, uongozi, hesabu, ustaarabu, protocal n.k.......

Acha kuwaza kitoto
 
Ngoja tuweke kwa kizungu huenda utaelewa na tutajua kama kuna siasa au ni abstract message imewafanya musielewe ujumbe mzito katika hiyo motto sijui tuite Slogan.

HEKIMA NI UHURU = "WISDOM IS FREEDOM".
Jiulize lengo la kutafuta elimu au maarifa pale chuo kikuu ni nini?
Jiulize hekima inapatikananje kama haujazaliwa nayo?
Jiulize hekima inaleta uhuru wa nini au kwa namna ipi?

Huo ni ujumbe mzito sana kuliko akili ya kawaida. Ni Abstract art, ni philosophical message.

Kwa kuanzia tu kujibu hayo maswali nakuambieni mnaodhani hiyo ni siasa.
Hekima huleta uhuru wa fikra.
Hizo fikra ndio hutumika kwenye hizo tafiti, kutoa huduma,kutoa elimu yenye manufaa kwa jamiii, n.k.
Kwa hivyo utaona ujumbe wa kwenye nembo ya Tumaini University upo ndani ya Ujumbe wa nembo ya UDSM.
Ni sehemu moja tu ya ujumbe mkubwa uliopo ktk nembo ya UDSM.

Hekima huleta uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuhoji, uhuru kufanya chochote bila kuvunja sheria, Uhuru wa kuchagua kitu unacho amini, uhuru wa kutafuta ukweli(tafiti), uhuru wa serikali kutoingiliwa na dini, n.k.

Mwenge ni alama ya uhuru(a torch is a universal symbol of freedom), kwa kesi hii ya chuo kikuu ni uhuru wa kifikra.
Tunaona uhuru wa kifikra huleta uhuru wa kila kitu kuanzia wa maoni , udadisi, uhuru wa kutafuta maarifa, uhuru wa kutafuta ukweli sio kwa hisia bali kwa kuegemea majibu ya tafiti(facts based in research ), uhuru wa kiuchumi, kutenganisha dola na dini, n.k.

Ni kama vile wamarekani walivyo tumia alama ya mwenge kwenye sanamu la uhuru ile sanamu yao inaitwa kwa kimombo The Liberty Statue.
Lile sanamu limeshika mwenge.
Wachache tutakuelewa ila wale wengine sidhani.
 
Nyie wenye diploma wasumbufu sana

Kwa hiyo kww akili zako suleimani hakuwa na elimu na alikuwa kizazi cha royal family?

Tangu Musa anasoma shule, iwe suleiman? Au elimu yako wewe lazima iwe formal? Na kutoa degree???

Suleiman alifundishwa tamaduni, madawa, historia, uongozi, hesabu, ustaarabu, protocal n.k.......

Acha kuwaza kitoto
Ahsante mkuu.
Ni kwamba jamaa anajifanya hajui royal family walikuwa wanapewa elimu ya vitu vingi ili waweze kuwa na uwezo wa kutawala vizuri.
Hajui kwamba maarifa (knowledge) inayopatikana kwa kujifunza/kufunzwa humfanya msomaji awe na hekima za kufanya vitu sahihi.

Anasahu hekima humuwezesha mtu kujifunza vitu vingi bila kuathiriwa na hisia au itikadi.
 
Back
Top Bottom