Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,985
144,312
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:

1581930635140.png

Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.

1581930424574.png

Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.
 
'Hekima ni uhuru', sijui hata maana yake ni nini.
Ngoja tuweke kwa kizungu huenda utaelewa na tutajua kama kuna siasa au ni abstract message imewafanya musielewe ujumbe mzito katika hiyo motto sijui tuite Slogan.

HEKIMA NI UHURU = "WISDOM IS FREEDOM".
Jiulize lengo la kutafuta elimu au maarifa pale chuo kikuu ni nini?
Jiulize hekima inapatikananje kama haujazaliwa nayo?
Jiulize hekima inaleta uhuru wa nini au kwa namna ipi?

Huo ni ujumbe mzito sana kuliko akili ya kawaida. Ni Abstract art, ni philosophical message.

Kwa kuanzia tu kujibu hayo maswali nakuambieni mnaodhani hiyo ni siasa.
Hekima huleta uhuru wa fikra.
Hizo fikra ndio hutumika kwenye hizo tafiti, kutoa huduma,kutoa elimu yenye manufaa kwa jamiii, n.k.
Kwa hivyo utaona ujumbe wa kwenye nembo ya Tumaini University upo ndani ya Ujumbe wa nembo ya UDSM.
Ni sehemu moja tu ya ujumbe mkubwa uliopo ktk nembo ya UDSM.

Hekima huleta uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuhoji, uhuru kufanya chochote bila kuvunja sheria, Uhuru wa kuchagua kitu unacho amini, uhuru wa kutafuta ukweli(tafiti), uhuru wa serikali kutoingiliwa na dini, n.k.

Chuo kikuu ni mahali ambapo unafundishwa na kukuzwa maarifa(knowledge) kwa uhuru na kwa kiwango cha juu kabisa.
Maarifa ya vitu vingi ndio hujenga hekima(wisdom). Kwa hivyo maarifa na hekima ni kama vina kamilishana(complement each other).

Mwenge ni alama ya mwanga, mwanga huondoa giza, giza kwa muktadha huu ni ujinga.
Mtu mjinga ni kama yupo gizani.

Mwenge ni alama ya uhuru(a torch is a universal symbol of freedom), kwa kesi hii ya chuo kikuu ni uhuru wa kifikra.
Tunaona uhuru wa kifikra huleta uhuru wa kila kitu kuanzia wa maoni , udadisi, uhuru wa kutafuta maarifa, uhuru wa kutafuta ukweli sio kwa hisia bali kwa kuegemea majibu ya tafiti(facts based in research ), uhuru wa kiuchumi, kutenganisha dola na dini, n.k.

Ni kama vile wamarekani walivyo tumia alama ya mwenge kwenye sanamu la uhuru ile sanamu yao inaitwa kwa kimombo The Liberty Statue unaweza kutafsiri kama Sanamu la Uhuru.
Lile sanamu limeshika mwenge.
 
Titicomb,
Hekima haifundishwi popote! Kazi ya msingi ya chuo kikuu chochote ni kufundisha, tafiti, na ushauri. Nani duniani humu amewahi kufikia "Hekima ya Sulemani"? Alisomea chuo kikuu kipi kuipata hekima ile? UDSM ijikite kwenye majukumu yake ya msingi badala ya kuambatana na siasa uchwara!
 
Hiyo alama ya nyoka kwenye nembo ya Tumaini ina maanisha nini?
Tumaini University is affiliated to religious organization; "Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.
 
Back
Top Bottom