NECTA mnafeli wapi?

NECTA mnafeli wapi?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,614
Udanganyifu kwy mitihani ya darasa la saba 2022 unampunguzia sifa kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA Athumani Amasi; za kuthibitishwa kwenye nafasi hiyo adhimu na kuibua matamanio ya enzi za Katibu Mtendaji wa zamani wa taasisi hiyo Dr. Charles Enoch Msonde aliyehamishiwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwenye wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu.

Jitihada za Dr. Msonde zilipewa msukumo na nguvu ya Mhe. Prof. Joyce Ndichako aliyeapa na kufanikiwa kuishi kwenye kiapo chake hicho cha mitihani kutovuja au udanganyifu kutofanyika kwa muda wote wa utumishi wake wizara ya elimu.

Kwa litmus test hii ya kwanza kabisa kwa Athumani Amasi; ya udanganyifu kwenye mitihani ya taifa ya darasa la saba, ni wazi kabisa kwamba ama mmoja wa wafuatao arudishwe kwenye nafasi zao za awali au nchi iendelee kunasa kwenye uozo:

1. Dkt. Charles Enoch Msendo

2. Prof. Joyce Ndalichako
 
Hahahaha, waiba mtihani mmeshikwa pabaya....Dokta Athumani amejua kuwakaba.
Mleta mada upuuzwe, Dk anachapa Kazi hasa, hataki janjajanja, mnacorrupt wasimamizi wawaonyeshe mitihani na kuwapa watoto majibu, halafu mnakuja kujitapa shule zenu zinaongoza.

Wahusika popote mlipo, Dk athibitishwe, Kwa hili sebene alilowachezesha kwenye hii mitihani Dk anatufaa, tena ikiwapendeza apewe na Uwaziri kabisa.
 
Kwa litmus test hii ya kwanza kabisa kwa Athumani Amasi; ya udanganyifu kwenye mitihani ya taifa ya darasa la saba, ni wazi kabisa kwamba ama mmoja wa wafuatao arudishwe kwenye nafasi zao za awali au nchi iendelee kunasa kwy uoza:-
Kwa taarifa yako hata mitihani ya ualimu mwaka huu kuna madudu mengi hasa mitihani ya TEHAMA, inasemekana vituo vilifanya mitihani computer zikiwa kwenye network, watahiniwa wakawa wanahamishiana majibu kwenye network, ikumbukwe wasimamimizi waliokuwepo siyo wataalamu wa masuala hayo, na wakitaka ushahidi wafuatilie mawasiliano ya simu kati ya wasahishaji wa mitihani na walimu wa masomo hayo.
 
Wamiliki wa shule binafsi mmeitana, madudu yalikuwepo, makatibu waliopita wakawa wanawachekea....kutwa mnatapa kufaulisha.
Hili jembe limekuja kuwanyoosha na kuweka uozo hadharani ndio mnatoka kumchafua.
Dk Athumani mitano tena, tunyooshee waiba mitihani.
 
Wewe ni mtoto mdogo hujui kinachoendelea

Unajua kwanini mwaka huu hawajatangaza shule bora kitaifa?

Huyo bwana athumani baada ya miaka miwili atakuwa ameharibu kwenye elimu

Kwa Tanzania sekta taasisi zilizobaki na uadilifu Baraza la mitihani na jeshi tu

Ila athumani kapelekwa kwenda kuharibu
Elimu ya kujibia watoto mitihani kisha wanapata A zote wakati kichwani hamna kitu?
 
Heagton
Heagton
Heagton English medium school,iko Tarime. Pale ukipeleka mtoto wako anafaulu na alama za juu kabisa hata kama hatajua kuhesabu 1-10.
Hongera zao shule ilishika nafasi ya kwanza kitaifa. 296 meanscore sio haba.
 
Wewe ni mtoto mdogo hujui kinachoendelea

Unajua kwanini mwaka huu hawajatangaza shule bora kitaifa?

Huyo bwana athumani baada ya miaka miwili atakuwa ameharibu kwenye elimu

Kwa Tanzania sekta taasisi zilizobaki na uadilifu Baraza la mitihani na jeshi tu

Ila athumani kapelekwa kwenda kuharibu
Prof. Ndalichako na Dr. Msendo waliisuka NECTA ikawa Afro Role Model, nchi nyingi zikaja kujifunza NECTA ambayo hao wawili waliijengea uwezo wa kitaalamu kwamba ingeweza hata kuhesabu kura za NEC na kupunguza hofu ya wizi wa kura kwenye chaguzi.

Athumani anaweza kuuambia umma kwanini asiwajibike maana anachukuwa hatua (ya wezi/wadanganyifu kurudia mitihani) baada ya wizi udanganyifu kufanyika badala ya kuchukuwa hatua kabla ya wizi/udanganyifu ili kuzuia tatizo kutokea.
 
Wamiliki wa shule binafsi mmeitana, madudu yalikuwepo, makatibu waliopita wakawa wanawachekea....kutwa mnatapa kufaulisha.
Hili jembe limekuja kuwanyoosha na kuweka uozo hadharani ndio mnatoka kumchafua.
Dk Athumani mitano tena, tunyooshee waiba mitihani.
Kabla ya Athumani kuwa Kaimu KM leo, enzi za awamu ya 5 tulisahau wizi na udanganyifu kwenye mitihani. Athumani alikuwepo ndani ya mfumo huo makini km mtumishi mwandamizi hivyo alijuwa mfumo ulivyoziba mianya ya wizi, iweje leo ana mamlaka makuu (hata km anakaimu) ashindwe kutumia mfumo ule ule uliotumika kuziba mianya ya udanganyifu? Akiri tu kuna sehemu amepwaya.

Au tunataka kujaza majengo ya madarasa tuliyoongeza kwa kuwapa wadanganyifu second chance?

Vyeti feki wamelipwa mafao manono (sijui na wengine wamerejeshwa!?) Wadanganyifu wa mitihani nao wanapewa fursa ya pili!? Madhali wadanganyifu wanajulikana kwanini wasipandishwe kortini ili iwe fundisho? Vinginevyo tufute mitihani ya shule tubakishe ile ya vyuo
 
Lini udanganyifu uliisha? Awamu ya tano ipi unayozungumzia? Sema viongozi hawakuwa huru kuibua madudu, tena udanganyifu ulifanyika Kwa kiwango cha kutisha Ili kupata sifa.
 
Prof. Ndalichako na Dr. Msendo waliisuka NECTA ikawa Afro Role Model, nchi nyingi zikaja kujifunza NECTA ambayo hao wawili waliijengea uwezo wa kitaalamu kwamba ingeweza hata kuhesabu kura za NEC na kupunguza hofu ya wizi wa kura kwenye chaguzi.

Athumani anaweza kuuambia umma kwanini asiwajibike maana anachukuwa hatua (ya wezi/wadanganyifu kurudia mitihani) baada ya wizi udanganyifu kufanyika badala ya kuchukuwa hatua kabla ya wizi/udanganyifu ili kuzuia tatizo kutokea.
Wamiliki wa shule binafsi hamumpendi Dk Athumani Kwa sababu Kaja kuwavurugia ugali, Siku hizi mitihani haivuji nje, mitihani inavujia ndani ya chumba cha mtihani....mnawalaghai wasimamizi na migambo wawaonyeshe mitihani mnasolve na kuwapa watoto majibu, au mnamlaghai msimamizi avuruge sitting plan Ili watoto wasaidiane.
Alichowafanyia Athumani mwaka huu hamtamsahau, na huo ni mwanzo Tu🤣
Fundisheni watoto acheni kutegemea mbinu chafu kutafuta sifa.
 
Yuko kimkakati kuokoa dini fulani hivi.
🤣🤣🤣🤣🤣 Kumbe sababu ni Dini yake? Hapo nimekuelewa, kuhusu uchapakazi Dk Athumani ni next level.
Tumechoka udanganyifu, darasa zima linapata A za mchongo kumbe mmeiba mtihani, kujishaua mtihani shule ya kwanza kimkoa, kumbe mnawalaghai walimu masikini Kwa vijisenti Ili waoneshe watoto majibu.
Acha aendelee kuwapa dozi.
 
Kabla ya Athumani kuwa Kaimu KM leo, enzi za awamu ya 5 tulisahau wizi na udanganyifu kwenye mitihani. Athumani alikuwepo ndani ya mfumo huo makini km mtumishi mwandamizi hivyo alijuwa mfumo ulivyoziba mianya ya wizi, iweje leo ana mamlaka makuu (hata km anakaimu) ashindwe kutumia mfumo ule ule uliotumika kuziba mianya ya udanganyifu? Akiri tu kuna sehemu amepwaya.

Au tunataka kujaza majengo ya madarasa tuliyoongeza kwa kuwapa wadanganyifu second chance?

Vyeti feki wamelipwa mafao manono (sijui na wengine wamerejeshwa!?) Wadanganyifu wa mitihani nao wanapewa fursa ya pili!? Madhali wadanganyifu wanajulikana kwanini wasipandishwe kortini ili iwe fundisho? Vinginevyo tufute mitihani ya shule tubakishe ile ya vyuo
Kuna point nyingi nzuri umezisema lkn pale uliposema juu ya mdanganyifu kupewa fursa ya pili kwakweli nimeshindwa kukushangaa!!! Hao ambao wewe hutaki wapewe fursa ya pili ya kurudia mitihani ni hawahawa watoto wa miaka 11-13+ Kweli kabisa watoto hao ulitaka waondelewe kwenye mfumo wa elimu eti kisa mitihani yao ilionesha kuwapo kwa udanganuifu? Is your head really well?
 
Wamiliki wa shule binafsi hamumpendi Dk Athumani Kwa sababu Kaja kuwavurugia ugali, Siku hizi mitihani haivuji nje, mitihani inavujia ndani ya chumba cha mtihani....mnawalaghai wasimamizi na migambo wawaonyeshe mitihani mnasolve na kuwapa watoto majibu, au mnamlaghai msimamizi avuruge sitting plan Ili watoto wasaidiane.
Alichowafanyia Athumani mwaka huu hamtamsahau, na huo ni mwanzo Tu
Fundisheni watoto acheni kutegemea mbinu chafu kutafuta sifa.
Ni hivi mkuu.

Eneo la shule wakati wa mitihani ya taifa linahesabika kama ni eneo la NECTA kwa sababu taratibu zinazoratibu uwepo pale ni taratibu za NECTA.

Ndiyo maana wanafunzi wasiyo watahiniwa na walimu (kasoro Mwl Mkuu) wanapumzishwa nyumbani wala raia hapasogelei.

Shule inapoitwa au inapopewa hadhi ya Kituo cha Mitihani maana yake ni eneo la NECTA kwa wakati wa mitihani ya NECTA, hivyo udanganyifu wa mitihani ukifanyikia pale kwy Kituo cha Mitihani tafsiri yake ni kwamba udanganyifu umefanyikia eneo la NECTA.

Athumani hili ni lake na ndiyo maana ameamua kuchukuwa hatua za kukabili saratani hii kwa kutangaza mitihani ya marudio.

Kama vituo vya mitihani siyo maeneo ya NECTA basi hasingechukuwa hatua anazochukuwa kurekebisha kasoro hizo za NECTA.
 
Kumbe sababu ni Dini yake? Hapo nimekuelewa, kuhusu uchapakazi Dk Athumani ni next level.
Tumechoka udanganyifu, darasa zima linapata A za mchongo kumbe mmeiba mtihani, kujishaua mtihani shule ya kwanza kimkoa, kumbe mnawalaghai walimu masikini Kwa vijisenti Ili waoneshe watoto majibu.
Acha aendelee kuwapa dozi.
Mkuu.

Binafsi sijataja dini yake Athumani wala sijui yeye ni dini gani.
 
Kuna point nyingi nzuri umezisema lkn pale uliposema juu ya mdanganyifu kupewa fursa ya pili kwakweli nimeshindwa kukushangaa!!! Hao ambao wewe hutaki wapewe fursa ya pili ya kurudia mitihani ni hawahawa watoto wa miaka 11-13+ Kweli kabisa watoto hao ulitaka waondelewe kwenye mfumo wa elimu eti kisa mitihani yao ilionesha kuwapo kwa udanganuifu? Is your head really well?
Wakipewa 2nd chance watadanganya tena O level na kupewa 3rd chance ya QT. A level pia watadanganya na kupewa 4th chance ya QT pia

Chuo Kikuu pia watadanganya kwa kujichangisha ela na kumnunulia Mhadhiri IST na Msimamizi Tablet.

Wakifika Muhimbili kuajiriwa watampasua kichwa mgonjwa wa kupasuliwa mguu.

Au wakifika Mahakamani watahukumu kesi kwa udanganyifu.

Wakiwa Wakurugenzi serikalini watanunuwa mabehewa na injini za mtumba za SGR kwa bei za mpya. Watajitetea kuwa hawajadanganya hadi CAG na PCCB ndiyo waje wawaumbue.

Mbele ya sheria na misahafu udanganyifu ni udanganyifu tu haunaga excuse wala compromise.

Mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Ukimkuta kwenye kabati la nguo ukamuonea huruma kwamba ni nyokamtoto umpe 2nd chance ya kuwa nyoka mkubwa, andaa jeneza lako mapema na andika urithi mapema pia. Is your head really adult or toddler? You rank quasi Trump's IQ with standard deviation of above 15.
 
Kuna point nyingi nzuri umezisema lkn pale uliposema juu ya mdanganyifu kupewa fursa ya pili kwakweli nimeshindwa kukushangaa!!! Hao ambao wewe hutaki wapewe fursa ya pili ya kurudia mitihani ni hawahawa watoto wa miaka 11-13+ Kweli kabisa watoto hao ulitaka waondelewe kwenye mfumo wa elimu eti kisa mitihani yao ilionesha kuwapo kwa udanganuifu? Is your head really well?
Usidanganywe na umri. Sheria za uhalifu (ukiwemo udanganyifu) hazinaga umri. Ndiyo maana nchi ina juvenile prisons (magereza ya watoto) na huko wamejazana tele tena wengine kwa kesi za mauaji kabisaaa, mbona hujaiambia serikali iwaweke huru? Mbona hujaiambia Parole iwaingize kwenye orodha ya misamaha ya rais ya wafungwa? Is your head really human?
 
Kwani mitihani inaibwa na watoto?au watu wazima (walimu/wenye shule)ndio huwapelekea hayo majibu ya mitihani (wizi).
Wanaotakiwa kuadhibiwa ni wezi wa mitihani ambao kimsingi sio watoto kwa sababu wao hawajui hata inapohifadhiwa hiyo mitihani.
 
Back
Top Bottom