Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 3,731
- 6,786
Baraza la mitihani NECTA ongezeni macho katika usimamizi wa mitihani ya darasa la Saba wilayani TARIME.
Kuna mbinu chafu zimebainika zitatumiwa na baadhi ya wamiliki wa shule za binafsi ili kufaulisha kwa kiwango kisicho Cha kawaida ili mwakani wapate wanafunzi wengi.
Baadhi ya shule hizo ziko maeneo yafuatayo
1. Tarime mjini
2. Sirari
3. Nyamwaga
4. Nyamongo
Kutoka chanzo changu Cha taarifa baadhi ya mbinu kuu zinazotumika ni hizo:
( a) kubadilishana karatasi kwenye vyumba vya mitihani.
(b) kuwapa rushwa wasimamizi waliopangwa kwenye vituo husika.
(c) kuonesha watoto majibu
(d) kupanga madawati kwa ukaribu kwa ajili ya wanafunzi kuibiana.
Na mbinu zingine nyingi.
Narudia tena shule hizo zimetenga vyumba maalum kwa baadhi ya walimu wanaoaminika kuokoa jahazi pindi inapohitajika.
Baraza la mitihani fanyeni ukaguzi kwenye mazingira mnayoweza kuyahisi kuwa maficho ya mamluki hao.
Niwatakie maandalizi mema kuelekea mitihani ya darasa la Saba
FAIR PLAY.