NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,463
- 17,291
Wadau wa elimu nchini.
Ipo haja mitihani hii isimamiwe na NECTA ILI kuiongezea TIJA na mkazo mashuleni KULIKO ulivyo Sasa.
Napendekeza yafuatayo kufanyika.
1. RATIBA
Ratiba ya ufanyikaji wake iwe sawa kote nchini ILI kuepusha ratiba kutofautiana toka mkoa mmoja hadi Mwingine kama Sasa. Hii italeta uwajibikaji wa pamoja(collective responsibility) kwa walimu kiufundishaji na utimizaji wa syllabus KWA wakati ILI kuwaandaa vijana na mitihani huo! Napendekeza Ratiba iwe fixed Mwezi wa nane au wa Tisa miezi miwili kabla ya mitihaniya Taifa. Hii itaepusha kila mkoa KUWA na mitihani yake na ratiba zake.
2. UTUNGAJI WA MITIHANI
Mitihani itungwe na Baraza kwa kufuata utaratibu kama ile ya Taifa, iwe yenye TIJA na kuwapima wahusika kidato cha nne, pili na Darasa la saba! kuepusha utungaji holela wa mitihani kama Sasa tena kwa zimamoto. Walimu wanapigiwa simu ghafula watunge mitihani haraka haraka matokeo yake unakuwa chini ya kiwango. Napendekeza Baraza litunge mitihani hii.
3. RASILIMALI FEDHA
Baraza litaagiza watahiniwa wasajiliwe mapema kama kawaida, wajue idadi yao mapema halafu liombe kibali toka hazina kuingizwa fedha za elimu Bure automatic kutokana na idadi ya ya watahiniwa kwa KILA Shule nchini, Fedha hizo zitatumika kuandaa mitihani! Napendekeza sh.7000/= kwa KILA mwanafunzi. Itasaidia kuepuka sarakasi na ubadhirifu wa fedha hizi unaofanywa na Maafisa elimu na kufanya mitihani hii kutokuwa na tija KWA watahiniwa,
4. USAHISHAJI NA USIMAMIZI
Mitihani isahishwe kimkoa vitengwe vituo maalumu KWA usahishaji chini ya uangalizi wa Baraza kea kuteua wawakilishi wasimamizi wakuu wa zoezi Hilo!
Wasahishaji wawachague wenyewe kwa KUTUMIA database yao KWA KILA mkoa.Hii itawapa fursa na exposure walimu wengi na kuwajengea uzoefu na uweledi katika utendaji KULIKO ilivyo Sasa ambapo walimu wanaosahisha MITIHANI ya NECTA ni wachache ukilinganisha na idadi yao nchini.
Usimamizi upewe uzito kama mitihani ya NECTA ilivyo kuongeza tija KWA mitihani hii.
NB: Napendekeza kile kikosi KAZI cha mtaala mpya wa elimu nchini kiharakishe mchakato, wimbi la vijana wasio na ajira nchini linaongezeka kwa Kasi Sana.
"Mzee Warioba arudishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"