NECTA: Hili ni jipu

Goweko

Member
Nov 30, 2014
6
1
Wana JF,

Baraza la Mitihani Tanzania mwaka uliopita wa 2015 liliendesha mitihani ya darasa la nne kama ilivyo ada.Lakini mwaka huo wa 2015 ilifanya mabadiliko kidogo katika usahihishaji kwa kuendesha zoezi hilo la usahihishaji kimkoa kwa usimamizi wa moja kwa moja wa NECTA.

Hapa Kagera zoezi la usahihishaji lilifanyikia wilayani Muleba kwa kuwashirikisha walimu toka wilaya zote zilizopo mkoani hapa.Jipu ninalotaka kulisema hapa linahusu malipo.
Baada ya shughuli ya usahihishaji kukamilika walibaki walimu wachache ili kukamilisha zoezi hilo.

Walimu hao wanadai posho ya siku sita kuanzia tarehe 25 -30/12/2015 lakini cha ajabu mpaka leo tarehe 19/01/2016 posho hiyo haijalipwa.Ubabaishaji huu wa malipo ulionekana tangu mwanzo kwa kulipwa posho hiyo kidogo kidogo.

Siku ya kumaliza zoezi hilo walimu waluondoka wamejiinamia kwa kuahidiwa kuwekea fedha hizo kwenye akaunti zao za benki.Tunaomba Katibu Mtendaji wa NECTA aingilie kati ili posho hizo zilipwe maana walimu walijituma na kazi ikafanyika ipasavyo.

Wito ni kwamba wawajali walimu na siyo kuwapuuza.

Nawasilisha wana JF.
 
Bila shaka kilio chao kimefika mahali panapohusika maana NECTA wamo humu. Lakini kwanini mnafanya kazi bila kujua mtalipwaje?
Baraza linatakiwa kujiandaa vizuri ili lifanye kazi zake kwa ufasaha na kuondoa malalamiko kama haya kutoka kwa walimu.
 
Back
Top Bottom