NEC yaweka masharti matumizi ya simu vituoni Oktoba 28


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imeweka masharti ya matumizi ya simu katika vituo vya kuhesabu, kupigia na kujumulishia kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mambo hayo yasiyotakiwa ni;

Mosi; mtu yeyote kutumia simu ya kiganjani ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura isipokuwa msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao watatumia simu zao pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu na simu hizo wakati wote ziwe zimeondolewa mlio na ziwe kwenye mtetemo.

Pili; viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha fujo, vurugu katika vituo vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura.

Tatu; vyama vya siasa, wagombea na wafuasi wao katika siku ya kupiga kura kufanya kampeni ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na kuvaa vazi lolote au kuwa na kitu chochote kinachoashiria kushawishi watu kumpigia kura mgombea Fulani.

Hii ni pamoja na matumizi ya vyombo vya usafiri vilivyokuwa vinatumika wakati wa kampeni vinavyoashiria utambuzi wa chama Fulani.

Nne, kiongozi, mgombea au mtendaji yeyote wa chama cha siasa kutoa lugha ya matusi kwa mtendaji wa uchaguzi.

Endapo kuna changamoto au lalamiko lolote kuhusiana na mchakato au taratibu za uchaguzi katika kituo cha kupigia kura, changamoto hizo zitawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi wa kituo kupitia kwa wakala.

Tano; kiongozi au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kuvamia au kukaa kwa nguvu ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura.

Sita; kiongozi, mgombea au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kujihusisha na vitendo vifuatuvyo:

I. Kuwahamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi mmoja
II. Kununua kadi ya mpiga kura, kununua kura au kutoa hongo, zawadi, shukrani au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpiga kura au mtendaji wa uchaguzi.
Hoja kubwa ya kuzuia simu ni kuogopa karatasi za matokeo kupigwa picha na kuwa ushahidi watakapo badirisha matokeo. Kumbuka nakala za matokeo kwa mawakala awamu hii imeelekezwa si lazima kutolewa. Kuwazuia watu kutumia simu vituoni ambapo mtu hutumia zaidi ya masaa 4 ni kuingilia Uhuru binafsi.
 
IMG-20201009-WA0012.jpg
 
Haya masharti yametolewa lini na nec na viongozi wa upinzani wanayachukuliaje?
Kama hali ndiyo hii ushindi mtausikia kwenye redio tu
Hii kitu Ni yakupinga kwa nguvu zote kabla ya uchaguzi kufika
 
Ata kivuli chao watakuja kuki ogopa
Wame juwa matokeo we utangaze ajira 13,000 za walimu waombaji wajitokeze zaidi 80,000 unahisi hizo kura za 67,000+ zita kwenda wapi!? CCM Ipo hoi ni polisi tu wana wapa oxygen vinginevyo wasinge kuwepo!
Hata hizo nafasi 13000 ni uongo, mpaka kura zinapigwa trh 28 hakuna atakaekuwa ameajiriwa. Ikitokea majina yakatoka, itafuata plan b, nayo ni pindi wakiripoti kwa wakurugenzi wataambiwa mafungu ya mishahara bado, warudi makwao watajulishwa mwaka mpya wa serikali.
 
Hata hizo nafasi 13000 ni uongo, mpaka kura zinapigwa trh 28 hakuna atakaekuwa ameajiriwa. Ikitokea majina yakatoka, itafuata plan b, nayo ni pindi wakiripoti kwa wakurugenzi wataambiwa mafungu ya mishahara bado, warudi makwao watajulishwa mwaka mpya wa serikali.
Mkuu ata TRA na mashirika mengine wameambiwa wadai baada ya 28
 
Mkuu ata TRA na mashirika mengine wameambiwa wadai baada ya 28
Watanzania kudanganywa imekuwa kawaida. Ajira 800 kwa vijana waliojitolea OP MAGUFULI alizoagiza waajiriwe ziliishia wapi? Au 1500 alizo agiza waajiriwe vijana waliojenga ukuta wa melerani zilikwama wapi?
 
Back
Top Bottom