NEC yaweka masharti matumizi ya simu vituoni Oktoba 28

Hata Malawi simu janja iliwaponza sana ndio maana uchaguzi ukarudiwa.Vyama vya upinzani nawashauri wanunue vyombo vya kurekodi na kupiga picha kama kalamu, saa, miwani nk vitawasaidia mbeleni.

Vinapatikana wapi vitu hivyo na kwa bei gani?
 
Simu janja inaogopwa kama bom !! CCM mtakuja kuwambia ata Mawakala muda wa kuhesabu wafunge macho!
Huu uoga umepitiluza aisee yaani ni ili uchakachuaji usijulikane, hili lilitakiwa lipingwe kwa nguvu zote.
 
Saba: Matokeo yaliyosainiwa kubandikwa nje ya kituo Cha kupiga kura kabla ya kutangazwa kwa mashindi.
Nane: Kura kuhesabiwa hadharani .
Mkuu hiyo kuhesabiwa hadharani ndiyo kabisa hawataki kuisikia. Zile mbwembwe za uwazi kwenye uteuzi wa wagombea kwenye vyama vyao kuwa live huku hawataki kabisa!!!
 
Tume nao wahakikishe wasimamizi wao wa uchaguzi hawafanyi jambo lolote litakalo sababisha kuzua taharuki kwa umma, kazi ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ifanyike kwa weledi, uaminifu, na wepesi wa hali ya juu ili kuepuka vurugu zozote.


Wasimamizi wa uchaguzi nao wafuate Kanuni za uchaguzi.

Mambo yaliyotokea Kinondoni kwenye uchaguzi wa marudio yasijirudie.

RIP AA.
 
Hiyo kuzuia simu lengo lake ni kuhakikisha hujuma zote zitakazofanyika kituoni hazifahamiki. Nawashauri watu wawe na silaha za jadi za kutosha kuzunguka vituo vya kura. Wakala wa upinzani akiona hujuma wakati wa upigaji, uhesabuji na kutangaza matokeo apige kelele ya mwizi mwizi. Hapo wananchi wenye hasira kali wavamie na kutoa kipigo kikali.
 
Wangesema simu hairuhusiwi period.

Msimamizi wa kituo na msaidizi wake wao simu wanaitumia kufanya nini ndani ya kituo cha kuhesabia kura na kutoa matokeo?!

kama wao lazima wawe na simu basi kuna ulazima wa wasimamizi wa vyama kuwa na simu zao pia.
 
Hawa WAHUNI wa CCM Mpya ni suala la muda tu, hakuna Mwananchi anayejitambua anayependa kuendelea tena na hii Serikali ya WATEKA NYARA, Kubambikia kesi zisizo na dhamana Watu, Kulipisha Kodi mara mbili zaidi ya gharama halisi za manunuzi, Kukandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa habari n.k
 
Uoga wote wa Nini wakati mna madaraja, mandege, maflyover
 
Siku zote watu waovu hupenda kufanya mambo yao kifichoni, ili kuweza kukamilisha uovu wao. Uwazi na ukweli wowote ule ambao unaweza kifuchua njia zao uovu huwekea vizingiti vingi, na hata kuutafutia kila aina ya hila ili uonekane kuwa wenyewe ndiyo ni tishio.

Hivi ndivyo vikaragosi vilivyofichwa ktk sura ya NEC ndiyo vinavyofanya. Wengi wao ni makada wasiokuwa na maadili ambao wamewekwa kimkakati kuzuia machaguo sahihi ya wapigakura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…