NEC yamuonya Nape kuhusu 'Goli la mkono'

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva amewaonya wanasiasa wanaotoa matamshi yenye uchozezi huku akitolea mfano maneno yaliyotamkwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa hakumtaja, kuwa chama chake kitashinda Uchaguzi Mkuu ujao hata kwa goli la mkono.

“Viongozi wawe makini wasitoe matamshi yanayoweza kuleta tafsiri mbaya. Goli la mkono ni matamshi yasiyo na breki,” amesema Jaji Lubuva.
 
Tunacho taka uje ututangazie mshindi halali na wewe usije chakachukua itakula kwako
 
hahahahaha hata kwa gori la mguu hawafungi mpaka sasa UKAWA wanaongoza ball position na tumeshafunga 1 bila wamebaki kushangaa hao madarali. team UKAWA for real.

wadau naomba kujuzwa nani kapita ubunge kura za maoni kigoma kaskazini.
 
* 'Goli la mkono' limezungumzwa lini na Tume inakuja kujibu lini...baada ya kushinikizwa ndipo wameona wazungumzie ....Tume kweli kimeo...
 
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva amewaonya wanasiasa wanaotoa matamshi yenye uchozezi huku akitolea mfano maneno yaliyotamkwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa hakumtaja, kuwa chama chake kitashinda Uchaguzi Mkuu ujao hata kwa goli la mkono.

“Viongozi wawe makini wasitoe matamshi yanayoweza kuleta tafsiri mbaya. Goli la mkono ni matamshi yasiyo na breki,” amesema Jaji Lubuva.

Kuna nukuu niliipenda sana inasema GOLI LA MKONO MWISHO WAKE BAFUNI
 
Hivi goli la mkono utafungaje wkt saa zote umepark bus golini kwako kuzuia mashambulizi? Labda goli la mkono la kujifunga. CCM bye bye, ntacheka tu mtakavyoanza kugombania lile gari la KUB analotumia Mbowe ikifika November.
 
Kwa utaratibu huu yaonekana Jaji Lubuva anaongozwa(akili tegemezi)alikua wapi kukemea kauli hyo cku zote? au anafikiri watanzania bado tu wavivu kupambanua mambo? kwa taarifa yake mwaka huu mchele una chuya.
 
Mzee kingunge ameshawahi kusema ushindi ni lazima wakati wa safari fulani sasa sijui maneno yanabaki palepale
 
Mbona Tume imechukua muda mrefu kutoa kauli hii au walikuwa wanam consult kwanza Nape ili atoe go ahead.
 
Back
Top Bottom