Habari kamanda wa anga! Nakusalimu Kwa salamu ya chama!
Baada ya salamu Hiyo, niandike machache hapa juu ya hatari iliyopo mbele yetu Sisi kama chama usipochukua hatua haraka Sana juu ya the so called wabunge wa viti maalumu!
1. Tumesikia na kuona pia Kwenye official pages za chama zile za ndani (WhatsApp group za chama) Juu ya majina ya viti maalumu 19, kuwa kamati ndogo ya kamati kuu imependekeza Kati ya hizo nafasi 19, nafasi 16 wamejipa wabunge waliokuwepo Bunge lililopita bila kujali kama waligombea viti maalumu Kwenye mikoa Yao na kushinda au kushindwa, na 3 wamepewa wengine wapya!
Hili ndugu mwenyekiti linaenda kukipasua chama wazi wazi, kwanini walioshinda Kwenye kura za maoni za mikoa Kwenye viti maalumu waenguliwe na nafasi zao kupewa mahawala wa akina salumu mwalimu na viongozi wengine ngazi ya taifa??? THIS TIME TUSIJELAUMIANA HATUTAKUBALI huu upuuzi wa akina salumu mwalimu na mahawala zake!
Sisi kama viongozi wa mikoa na kanda hatutakubali uvunjifu huu wa utaratibu, Aliyeshinda kura ya maoni apewe nafasi yake aliyeshindwa naye apumzike aje ajenge chama kama ambavyo wanachama wengine wanajenga chama Kwa gharama kubwa!
Hili naomba lisiangalie Sura ya MTU au umaarufu wake, kama M/kiti wa BAWACHA Halima mdee aligombea viti maalumu Dar na akashika nafasi ya Kwanza ana-deserve kwenda bungeni ila kama hakugombea au alishindwa Kwenye kura za maoni ATUPISHE, hali kadhalika na Kwa wengine pia wanajiona ni maarufu Kwenye chama kanuni na taratibu zifuatwe, kugombea Jimbo sio kigezo cha kupewa kiti maalumu Hilo lipo na linajulikana Kwenye miongozo yetu.
Huu ubinafsi haukubaliki na hautakubalika anymore, 2015 tulikaa kimya this time patachafuka, tena tunaomba afande muroto wa Dodoma ajuee kabsa kamati kuu mkibariki uvunjifu huu wa utaratibu kupendekeza majina ya viti maalumu Kwa walioshindwa na kwa ambao hawakugombea kabsa viti maalumu Kwenye kura za maoni mikoani, kuwabeba akina Fulani atuachie nafasi tuwashikishe watu Fulani adabu, hili hatutanii! Afande muroto tunakuomba Sana juu hili bakoora zitatembea Sana, kama hamuamini Jaribuni muone, sumu huwa haionjwi tumeshatoa tahadhari!
2. Pia kamanda tunakuomba Sana huyu salumu mwalimu ni kirusi, anavuruga taratibu Kwa maslahi yake binafsi deal naye immediately, ukishindwa usijetulaumu, haiwezekani ajaze mahawala zake bungeni tunamwangalia tuu tena Kwa kuvunja taratibu, wengi wa mahawala zake Kwenye kura za maoni walishindwa!
Ombi Kwa NEC: majina yatakapokuja kwenu plz over plz jiridhishe na regulation kama zimefuatwa, tabia za kuchomeka mahawala na ndugu ambao hata Kwenye mchakato wa kura za maoni hawakupitia haikubaliki!
Nimemaliza samahanini Sana wanajukwaa nimeandika huku hasira imejaa baada hizi habari za kipuuzi za akina Halma na genge la salumu kutaka kuvuruga utaratibu!
Wasalaam.