NEC yafafanua Upotoshaji kuhusu Karatasi za kupiga kura Uchaguzi Mkuu 2020

Nguruka

Senior Member
Dec 6, 2006
180
124
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Willson Mahera Charles ametoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji uliofanywa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika kuhusiana na mchakato wa Manunuzi wa Karatasi za kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
 
Huyu mwanaccm kindakindaki aliyepo tume hana chochote..
Mkuu umeona utata wa wazi kwenye hiyo barua. Hizo kampuni mbili kwanza kuna utata wa namba, tunaona kampuni namba 2 ya Kenya na 3 ya Dubai. Ukiachia utata wa hizo namba maana hakuna namba moja. Lakini hizo kampuni mbili za Kenya na Dubai zina uhusiano gani na Kampuni iliyoshinda zabuni ya Afrika Kusini?

CDM wanapaswa kuibana tume ifaavyo maana ukweli unazidi kusogea karibu.
 
Mkuu unge download document nzima ndio ukaja kuelezea utata wa namba, ila kutumia hii iliyowekwa kama picha unakosea sana, hapo ndipo chadema mnapokwama
 
Mkuu umeona utata wa wazi kwenye hiyo barua. Hizo kampuni mbili kwanza kuna utata wa namba, tunaona kampuni namba 2 ya Kenya na 3 ya Dubai. Ukiachia utata wa hizo namba maana hakuna namba moja. Lakini hizo kampuni mbili za Kenya na Dubai zina uhusiano gani na Kampuni iliyoshinda zabuni ya Afrika Kusini?

CDM wanapaswa kuibana tume ifaavyo maana ukweli unazidi kusogea karibu.
Una akili sana mwandishi anataka kudanganya halafu hajafuzu uongo maana wameandika kampuni ya Dubai na Kenya huku tunaona afrika kusini,swali kampuni gani inayosambaza vifaaa watuambie
 
Mshana Jr uzi wako wa Jamana Printers unasimama wapi. Tukiweka siasa pembeni na kutazama kisomi umeelezewa taratibu zilivyofanyika sasa ndo sijui ni za ukweli au za magumashi ila suala la Jamana uliingia mkenge. Taarifa zenye ushahidi kama hizi ukianzisha uzi ilimradi unakamatika, hii ni tofauti na uchawi ambao hatuwezi prove ukweli au uongo.
 
Unakili sana mwandishi nataka danganya alafu ajafuzu uongo maana wameandika kampuni ya Dubai na Kenya uku tunaona afrika kusini swali kampuni gani inayosambaza vifaaa watuambie
Wewe na tindo hamjapakua hata hiyo document tiyari mshaanza kuikosoa. Kuna tofauti kati ya taarifa ilivyotolewa na ilivyowasilishwa. Aliyeileta ndiye kakata ile kampuni ya kwanza.

Soma hapa
Screenshot_2020-10-12-17-47-54-96_c37d74246d9c81aa0bb824b57eaf7062.jpg
 
Inawezekana ile tabia ya kudeka viongozi wa CDM washaambukizana wote..kila siku kulialia tu wakati ukweli upo wazi
 
Back
Top Bottom