Uchaguzi 2020 NEC: Wagombea muwe makini, tusilaumiane

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,947
2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa kuchagua watu makini ili kuepusha migogoro baina yao na Tume, pindi wanapotakiwa kukamilisha mchakato wa kupitisha majina ya wagombea.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage, wakati akizungumza na wadau wa vyama hivyo leo Agosti 1, 2020, jijini Dar es salaam, ambapo wamejadili Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, na mambo ya kuzingatiwa.

Amesema kuwa fomu za uteuzi zitaanza kutolewa Agosti 5, 2020, kwenye makao makuu ya ofisi za Tume jijini Dodoma kwa wagombea wa kiti cha Urais huku Wabunge na Madiwani watafuata fomu hizo katika makao makuu ya Halmashauri ya Majimbo na Kata husika.

“Fomu zitaanza kurejeshwa muda wowote pindi mgombea anapomaliza kujaza kwa usahihi hadi Agosti 25 saa 10 jioni, ambayo ndiyo itakuwa siku ya uteuzi, naomba mjaze kwa usahihi bila dosari yoyote ili usijekosa sifa na usiteuliwe na kuanza lawama”, amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaijage ameongeza kuwa, “Wale wote wenye malalamiko na tume tunaomba mtuletee wenyewe tutayafanyia kazi, ila sio kulalamikia mitandaoni hatutajihusisha na malalamiko ya mitandaoni”.

Ameongeza kuwa Tume imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambapo waliojiandikisha ni zaidi ya Milion 29 na kusisitiza kampeni za uchaguzi kwa Zanzibar zitaisha Oktoba 26,2020 ili kupisha upigaji kura ya mapema ya Rais wa Zanzibar, Mwakilishi na Diwani.
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,193
2,000
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume kuhakikisha wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea.

Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendezi.

Amandla....
 
Katashekadm

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
367
500
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea. Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendenezi.

Amandla....
Kwani Kuna wagombea vichaa?
Kama mgombea kiti cha urais hawezi kujaza fomu kwa usahihi, hafai
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
740
1,000
Wagombea mkumbuke kurekodi video ya jinsi mlivyojaza fomu zenu isaidie kutobadilishwa au kurekebishwa kwa nia ovu na wasimamizi ili ipigwe pingamizi, na pia mrekodi video ya kukabidhi fomu wakati wa kurudisha kwa msimamizi wa uchaguzi.

Kumbukeni ushahidi wa video ya kukabidhi fomu ulivyomsaidia mgombea wa CHADEMA Jimbo la Ludewa mwaka 2015 marehemu Deo Filikunjombe alivyotaka kucheza rafu ya kupita bila kupingwa.
 
Shambaboy jogoli

Senior Member
Apr 7, 2020
143
250
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea. Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendenezi.

Amandla....
Hadi kujaza fomu mpaka msaidiwe na Tume? Duh hii Kali, ukikosea tume haina lawama na hufai kabisa kuwa mgombea!
 
Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
3,487
2,000
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea. Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendenezi.

Amandla....
Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
 
nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,297
2,000
Wagombea mkumbuke kurekodi video ya jinsi mlivyojaza fomu zenu isaidie kutobadilishwa au kurekebishwa kwa nia ovu na wasimamizi ili ipigwe pingamizi, na pia mrekodi video ya kukabidhi fomu wakati wa kurudisha kwa msimamizi wa uchaguzi.

Kumbukeni ushahidi wa video ya kukabidhi fomu ulivyomsaidia mgombea wa CHADEMA Jimbo la Ludewa mwaka 2015 marehemu Deo Filikunjombe alivyotaka kucheza rafu ya kupita bila kupingwa.
Ndio maana alikufa na alifia porini. Ukiwana roho mbaya kifo chako kinakuwa kibaya pia
 
Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
942
1,000
Wagombea mkumbuke kurekodi video ya jinsi mlivyojaza fomu zenu isaidie kutobadilishwa au kurekebishwa kwa nia ovu na wasimamizi ili ipigwe pingamizi, na pia mrekodi video ya kukabidhi fomu wakati wa kurudisha kwa msimamizi wa uchaguzi.

Kumbukeni ushahidi wa video ya kukabidhi fomu ulivyomsaidia mgombea wa CHADEMA Jimbo la Ludewa mwaka 2015 marehemu Deo Filikunjombe alivyotaka kucheza rafu ya kupita bila kupingwa.
Naam! Ni sahivi kutoa copy, au ku-scan fomu iliyojazwa kabla ya kuirudisha ili kubaki na nakala ngumu/ na laini kwa ajili ya kuja kuwaumbua mawakala wa shetani waliohujumu wagombea wa upinzani mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni vyema pia kuweka ushahidi wa video wa makabidhiano ya fomu, maana mawakala wa shetani wameshapokea maelekezo wazichome fomu waseme hawajapokea, mwaka huu tutaenda sambasamba mpaka home "nait kali" tutawazukia ikibidi
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,596
2,000
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea. Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendenezi.

Amandla....
Hiyo lugha tu ni kiashiria cha mtu mbabaishaji
 
Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
360
1,000
Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
Aliyekuambia kujaza fomu ni kama kufanya mtihani nani? Kujaza fomu ni swala la kuelekezana tu na wala halitakiwi kuwa swala la kukomoana. Unapolilinganisha na mtihani unataka kutuaminisha kuwa kwenye kujaza fomu ndio uchaguzi wa wananchi. Acheni kuanza kutengeneza mazingira ya kuhujumu upinzani kabla hata ya kura kupigwa.
 
mr.London

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
2,782
2,000
Kama kampeni zanzibar zitaisha october 26 ni dhahiri kwa zanzibar uchaguzi hautafanyika siku sawa na ule wa tanganyika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom