Uchaguzi 2020 NEC: Wagombea muwe makini, tusilaumiane

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,249
2,000
Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
Mfano wako mzuri sana. Nchi zilizoendelea mwalimu anahakikisha wanafunzi wana vifaa vya kuandikia. Na anakueleza mahitaji ya swali kwa sababu lengo la mtihani sio kukufelisha bali kupima uelewa wako.

Ndio maana mara nyingi unaruhusiwa kuingia na vitabu na calculator kwenye mtihani. Kwenye uchaguzi hatutafuti bingwa wa kujaza fomu bali mtu ambae wananchi wataona anafaa kuwawakilisha na kuwapigania.

Kumtoa mgombea kwa sababu ameandika Fundi Mchundo badala ya F Mchundo sio haki.

Amandla...
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,249
2,000
Kwani Kuna wagombea vichaa?
Kama mgombea kiti cha urais hawezi kujaza fomu kwa usahihi, hafai
Wangekuwa vichaa, hata kuwaelekeza ingekuwa bure. Tatizo la hali iliyopo ni kuwa inatoa nafasi kwa wasimamizi kuwasaidia tu wale wanaowapenda na hata kwa baadhi kuingiza dosari ( herufi katika jina) katika fomu ya yule wasiemtaka. Hii inawezekana isiwe kweli lakini ndivyo watu watakavyoamini hasa inapotokea kuwa ni wagombea wa vyama fulani tu ndio wanaokosea.

Amandla...
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,249
2,000
Naam! Ni sahivi kutoa copy, au ku-scan fomu iliyojazwa kabla ya kuirudisha ili kubaki na nakala ngumu/ na laini kwa ajili ya kuja kuwaumbua mawakala wa shetani waliohujumu wagombea wa upinzani mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ni vyema pia kuweka ushahidi wa video wa makabidhiano ya fomu, maana mawakala wa shetani wameshapokea maelekezo wazichome fomu waseme hawajapokea, mwaka huu tutaenda sambasamba mpaka home "nait kali" tutawazukia ikibidi
Nani atakuruhusu kupiga picha fomu yako? Ingekuwa vyema kama msimamizi angekuwa anasaini nakala ya fomu iliyowasilishwa kuthibitisha kuwa amepokea.

Na pale inapoonekana imekosewa mgombea arudishiwe fomu aliyowasilisha ikionyesha dosari zilizoonekana. Lakini sidhani kama inakuwa hivyo.

Amandla...
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
7,881
2,000
Mfano wako mzuri sana. Nchi zilizoendelea mwalimu anahakikisha wanafunzi wana vifaa vya kuandikia. Na anakueleza mahitaji ya swali kwa sababu lengo la mtihani sio kukufelisha bali kupima uelewa wako. Ndio maana mara nyingi unaruhusiwa kuingia na vitabu na calculator kwenye mtihani. Kwenye uchaguzi hatutafuti bingwa wa kujaza fomu bali mtu ambae wananchi wataona anafaa kuwawakilisha na kuwapigania. Kumtoa mgombea kwa sababu ameandika Fundi Mchundo badala ya F Mchundo sio haki.

Amandla...
Hawa washenz wa akili hawawez kukuelewa
 

lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,000
2,000
Kujaza fomu ni njia tu ya kupata taarifa sahihi za mgombea. Nia ovu za kipuuzi zimeanza kutumika kupitia fomu kuwaondoa wagombea, hii siyo sawa hata kidogo (rejea uchaguzi wa serikali za mitaa).

Watu wenye hila mbaya hawatakiwi kuwa waamuzi katika jamii au taifa. Uovu unaweza kuhalalishwa kwa kutumia sheria na kanuni pale tu kwenye waamuzi wabaya.
 

Nguruka

Member
Dec 6, 2006
37
95
Tume makini ingesema kuwa wagombea wanaweza kupata ushauri kutoka kwa Tume kuhusu ukamilifu wa fomu zao. Ili kulinda demokrasia, ni wajibu wa Tume kuhakikisha wagombea wengi iwezekanavyo wanapata fursa ya kugombea. Ningetegemea msimamizi anapo pokea fomu aipitie pamoja na mgombea na kumpa nafasi ya kusahihisha dosari zozote zinazoonekana kabla ya dirisha kufungwa.

Lugha za tusilaumiane hazipendenezi.

Amandla....
Tume ipo sahihi sema kuna wagombea husubiri siku ya mwisho ndio wanarudisha fomu. Tabia hiyo ibadilike.
 

Nguruka

Member
Dec 6, 2006
37
95
Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
Hahahaaaaaaaa kukosea ndio moja ya kuonesha huwezi kazi.
 

petrol

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
351
250
Naomba ufafanuzi: Kama mgombea au mtia nia asipojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura bado atakuwa na sifa ya kugombea Urais, Ubunge au Udiwani. Kuuliza si ujinga.
 

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,054
2,000
Baada ya utawala wa JPM hakuna tena mtu atakayeheshimika kwa title yake....sijui Dkt (PhD), Profesa, Jaji n.k

Wote wamekuwa wapuuzi puuzi tu
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,190
2,000
Kuna mtu alikwishawahi kujiuliza swali hili?? Inakuwa mgombea wa chama kimoja anaweka pingamizi kuwa fomu ya mgombea wa chama kingine sio sahihi wakati mgombea huyo hakukabidhiwa fomu hiyo???

Ukweli ni huu - NEC huchukua fomu za wagombea na kuzikabidhi kwa chama fulani ili wagombea wake waweke pingamizi. Tume haijawahi kuweka pingamizi kwa mgombea!!

Kwa sasa tume ingeita wagombea wote pamoja na kuzikagua na kuzirekebisha. Mapingamizi mengine ambayo sio makosa ya jinai au madai hayana maana lakini Tume imekuwa ikiyakubali kwa faida ya chama kimoja!
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,210
2,000
Hii tume sio rafiki kabisa kwa wadau wa uchaguzi pia haina ushirikiano kabisaaaa yaaani mi siamini kwa tume hii kama kutakuwepo na uchaguzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom