Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
NEC imetangaza mikakati ya kulinda kura wakati wa uchaguzi
Mkakati wa kwanza
- Matokeo yatajumlishwa kisayansi majimboni na ya urais yatabandikwa kila yatakapohesabiwa
- Kutakuwa na kituo cha matokeo, ambapo yatajumlishwa kwa uwazi na waandishi wa habari kuruhusiwa kushuhudia.
Mkakati wa pili
Kuhusu tetesi kuwa kuna masanduku ya kura yametengenezwa na kuhifadhiwa katika maeneo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ):
NEC imesema: Kwenye kila sanduku la kura kutakuwa na namba kulingana na namba ya jimbo. Kama kuna watu wametengeneza masanduku ya kura watakuwa wamejisumbua, kwani hayatatumiwa; masanduku ya Tume yatakuwa na namba maalumu kulingana na jimbo husika.
Mkakati wa tatu
Ingawa sheria inaitaka Tume kuwasilisha Daftari kwenye vituo siku nane kabla ya uchaguzi, lakini mwisho wa mwezi huu watavipelekea vyama vya siasa Daftari hilo, ili kupunguza malalamiko ya wapiga kura kutoona majina yao kwenye Daftari la wapiga kura.
Mkakati wa nne
Karatasi za kura zimechapishwa uingereza na si nchini kama inavyosikika, picha na majina ya wagombea yataandikwa kwa kufuata alfabeti na yataanza na chama chenye herufi ya A na kuendelea, mpango ambao umewekwa kuwarahisishia wasioona.
Kwa maana hiyo majina na picha za wagombea urais na vyama vyao vitakuwa katika mpangilio ufuatao:
1: APPT-Maendeleo; Peter Mziray
2: CCM; Jakaya Kikwete
3: CHADEMA; Dk. Willibrod Slaa
4: CUF; Profesa Ibrahim Lipumba
5: NCCR-Mageuzi; Hashim Rungwe
6: TLP; Mutamwega Mugahywa
7: UPDP; Fahmi Dovutwa