NEC na jina kamili la mpiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC na jina kamili la mpiga kura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamayu, May 24, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Jana nimebadilisha kata na jimbo la uchaguzi katika daftari la kudumu la wapiga kura. Mwandikishaji akaandika majina mawili tu badala ya matatu ambayo nilikuwa nimeandikisha awali (Jina la kwanza, la kati na la ukoo).

  Nikamwuliza kwa nini akuandika 'surname' na akajibu kuwa wameambia waandikishe majina mawili tu. Nilikuwa mbogo kidogo na ilibidi aandike yote matatu, sasa kama vitambulisho hivi inasemekana hununuliwa je hii sio mbinu ya kupata vitambulisho vyenye majina tofauti vya ziada bila gharama yoyote?

  Cha ajabu vitambulisho vya zamani vinabaki na kurudishwa kwenye tume bila kutobolewa mbele ya mpiga kura aliyekibadilisha, je akitakwenda kutumika kama vile vinavyonunuliwa? Hivi jina kamili uandikwa vipi? Nijuavyo mimi ni 'first name', 'middle name' na 'surname'. Kabla ya uchaguzi tutasikia takwimu zao ambazo zitakuwa na utata tu!
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  Senior member,Mwanamavu,mkulu aliposema haihitaji kura za wafanyakazi (of course na wategemezi wao pia) hukuelewa maana yake? au Waziri Chami alipowaambia Kilimanjaro kwamba hata kama msipompa kura Mkulu,atashinda tu tena kwa kishindo,hukuelewa? Wana namna zaidi ya 5 za kupata kura za idadi wanazotaka wao. Inaniuma sana kwamba,ni wangapi wanafahamu maana ya FULL NAME....ni wangapi wenye guts za kudai hicho ulichodai......ni wangapi wanaoweza ku-speculate implication ya kuandikwa majina nusu nusu......!! CCM wapo strategic sana...wanawanyima watu elimu ya uraia ya kutambua haki zao (shule bila elimu na walimu=St. Kayumba a.ka. za kata) na ndi maana waraka wa wakatoliki wa kuelimisha waumini wake (na watanzania wote kwa ujumla) uliwauma sana!!
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vyama vya upinzani vimelala usingizi. Wanapaswa sasa hivi kuwa na inteligencia yao wawepo vituoni kuhakikisha kwamba hakuna mchezo mchafu wa aina yoyote utakaofanyika wakati huu wa kujiandikisha hadi wakati wa uchaguzi. Wanapaswa kufuatilia kila hatua ya uandikishaji, lakini sidhani kwamba wanafanya hivyo. Wanasubiri kura zikipigwa mshindi akishatangazwa ndio wakurupuke na malalamiko kibao. Haya mambo ya mapungufu na uzembe katika uandikishaji pamoja na vitambulisho kukusanywa kiholela bila kujua vinapelekwa wapi upinzani wanapaswa kuyafuatilia kwa karibu.
   
 4. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mimi nilishasema CCM tunajua imeoza, lakini na nyinyi upinzani nyinyi! Ohoooooo, tutaonana wa baya, nyie haya we!
  Itafika pahala upinzani tutawaamsha kwa viboko, nyie ngojeni tu, mnaacha kufikiri kabla ya kutenda mnakuja kufikiri baada ya kutenda. Nyinyi vipi nyinyi? Nani kawaloga? Ni njaa, uroho wa madaraka ama kukosa dira? Utasikia wanahama hama na mwishowe wanarudi CCM. Yaani ndo maana CCM wanawakebehi na kuwadharau, infact na wananchi ndio maana wanaona hamfai kuaminiwa, kwa sababu hamueleweki! Hivi nyinyi hamna kale-kautaratibu kakunyweshana maji ya bendera?
  Iko siku wapiga kura watachoka kabisa ndipo hapo wote ,si CCM wala Upinzani, wote mnakula bakora. Huwezi ukakaa kwenye kiti cha dereva ukaacha kuendesha na wasafiri wakuangalie tu hivi hivi ilhali wanachelewa kule wanakotaka kufika!
  Nyinyi ngojeni tu!
   
 5. M

  Mkono JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu umenikuna vya kutosha,hawa jamaa wanastahili kuamushwa kwa viboko.
   
Loading...