NEC hoi, itaharibu mambo

NEC hoi, itaharibu mambo

Rais ndiye hubeba taswira ya taifa! Taifa huwa imara kwa kadiri ya kiongozi wake mkuu anavyokuwa imara, and the converse is also true!
 
haya aliwah kuyasema Nguruvi3 kwamba NEC iache kuhadaa watu kwamba watamaliza kufanya kazi ya kuandikisha kwa mudaa huu mfupi ili kura ya maoni ipigwe
haya sasa hata njombe hapajaisha kura ya maoni ni mwezi wa 4 inakuwaje?

Wanasubiri Maelekezo Kutoka Lumumba. Lumumba ikisema hakuna Kura ya Maoni kesho yake utamuona Jaji Lubuva kwenye Media
 
Ccm imechoka
Sihofii kura ya maoni kama navyoofia uchaguzi wa October naona kama ccm wanatafuta sababu waendelee kuongoza kwa nguvu
 
Ya leo kali kweli mwenyekiti analalamika kanyimwa bvr kits Kenya na Nigeria..teeeh huyu mzee huyu

Hii ni aibu ya RAIS wa Tanzania.Yaani huko wanacheka na kumng'on'ga,yaani Mzee kwa kusafiri lakini ameshindwa kununua vifaa muhimu vya uchaguzi.

Duh,kwa pesa za kununua Khanga na Tshirt,kuiba wanazo,za kununua vitu vya maana hakuna,..."Eti tumeenda kuazima"Kweli aliyezoea kukalia JAMVI ukimpa kiti atashindwa atataka akae chini kabisa...................
 
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwa sababu ya NEC. NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa, katika kuandikisha wapiga kura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.

Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.

NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.

NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ati walienda kuazima vifaa vya kuandikisha NIGERIA na Kenya! na wakanyimwa! AIBUUUUU.... kwa kweli Taifa lipo mashakani kwa namna hii. kila kitu tunaomba, tuna azima, tunakopa.... hata kuandikisha hakuna plan hadi tuazime! Shame on you !
 
Kweli kabisa mkuu, kuna siku niliwahi kuweka uzi hapa kuhusu Mzee Lubuva kuwa amechoka kimwili na kiakili hawezi hii kazi, na haoni hatari ya mbeleni kwa taifa hili endapo mambo yatavurugika kwa watu kukosa haki yao ya msingi. Ifike mahali mwenyekiti wa tume ya uchaguzi si lazima awe jaji anaweza kuwa mtu yeyote mwenye uwezo. Kenya walikuwa na kijana mdogo kabisa Bw. Isack kama sikosei alikuwa around 40yrs. Sasa leo tunakuwa na mtu hata kumbu kumbu zimeanza kumtoka bado tunampa majukumu mazito na yenye kugusa maslahi mapanda na mustakabali wa nchi yetu.
Taifa hili watu 45 milioni kweli tunakosa mtu makini atufanyie hii kazi??????

Tatizo siyo Mwenyekiti wa Tume bali watawala.
 
haya aliwah kuyasema Nguruvi3 kwamba NEC iache kuhadaa watu kwamba watamaliza kufanya kazi ya kuandikisha kwa mudaa huu mfupi ili kura ya maoni ipigwe
haya sasa hata njombe hapajaisha kura ya maoni ni mwezi wa 4 inakuwaje?

Aliyepanga kura ya maoni anajulikana; siyo NEC. Wanaotoa fedha za kugharamia uboreshaji daftari la wapiga kura ili kura ya maoni ifanyike siyo NEC. Serikali ndiyo inayolazimisha kura ya maoni na serikali hiyo hiyo imeshindwa kuipatia NEC fedha kwa wakati. Wa kulaumiwa kwa hili siyo NEC bali ni serikali.
 
Ccm imechoka
Sihofii kura ya maoni kama navyoofia uchaguzi wa October naona kama ccm wanatafuta sababu waendelee kuongoza kwa nguvu
Umecheza na akili yangu kabisa. Hata walazimishe kupitisha katiba kibabe cha muhimu ni kuhakikisha uchaguzi mkuu wa october ushindi mkubwa unakwenda kwa upinzani. Hapo hiyo katiba inapigwa chini kwa ridhaa ya wananchi kisha tunafuata katiba ya akina Warioba. Cha muhimu bunge hili kama litaweza lipitishe tume huru ya uchaguzi na ninapendekeza tume ya akina Jaji Warioba ndio ipewa mikoba ya tume.
 
Wanasubiri Maelekezo Kutoka Lumumba. Lumumba ikisema hakuna Kura ya Maoni kesho yake utamuona Jaji Lubuva kwenye Media

hapa panatakiwa hata wananchi wenyewe tufanye maamuzi magumu kidogo
 
Aliyepanga kura ya maoni anajulikana; siyo NEC. Wanaotoa fedha za kugharamia uboreshaji daftari la wapiga kura ili kura ya maoni ifanyike siyo NEC. Serikali ndiyo inayolazimisha kura ya maoni na serikali hiyo hiyo imeshindwa kuipatia NEC fedha kwa wakati. Wa kulaumiwa kwa hili siyo NEC bali ni serikali.

NEC nailaumu manake inashindwa kuiaambia serikali ukweli. sion haja ya LUBUVA kusema kura ya maoni itawezekana na wananchi wataandikishwa ikiwa naona mapungufu yaliyopo. kwann assiambie serikali kwa mwenendo wenu wa kutiokuleta fedha kwa wakati na kuwa na vifaa vichache zoezi halitoweza kumalizika ndani ya muda mnao taka ili kura ipigwe.

kwenye action plan yake NEC si ilipanda ikijua kwamba vifaa wanavyotaka vingefika? SASA KAMA HAVIJAFIKA KWANN WASISEME HAPA TUTASHINDWA KUFIKIA LENGO?
 
Baada ya kufanikiwa kufanya mambo kwa kubahatisha bahatisha na uzembe wa hali ya juu na kukwepa kushughurikia mambo ya msingi kwa takribani miaka tisa ya utawala wake sasa kikwete hana pakutokea.

wahenga walisema hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, na sasa inatokea

wahenga pia walisema, mficha ugonjwa ataumbuliwa na kifo, na ssa inatokea

Crisis hii haiharishiki, Kikwete asipokimbilia kudai amekubariana na ushauri wa wale wanaopendekeza hili zoezi lisitishwe kupisha uchaguzi mkuu nchi inaingia matatizoni sasa hivi.

na udhaifu wake utakuwa bayana kwa ulimwengu mzima.
 
Hii ni aibu ya RAIS wa Tanzania.Yaani huko wanacheka na kumng'on'ga,yaani Mzee kwa kusafiri lakini ameshindwa kununua vifaa muhimu vya uchaguzi.

Duh,kwa pesa za kununua Khanga na Tshirt,kuiba wanazo,za kununua vitu vya maana hakuna,..."Eti tumeenda kuazima"Kweli aliyezoea kukalia JAMVI ukimpa kiti atashindwa atataka akae chini kabisa...................

Hivi pesa ya escrow haitoshi kununua???
 
Mambo mengine ni kukaa kimya tu. Time will speak...
 
Hivi pesa ya escrow haitoshi kununua???

Umesahau wameshagawana maana mpaka Housegirl wa nanii alipewa ili asitoe siri:eyebrows::eyebrows:.....Ila angalia KUCHA tu............:disapointed::disapointed:
 
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwa sababu ya NEC. NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa, katika kuandikisha wapiga kura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.

Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.

NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.

NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

NEC wanadai vitambulisho vya zamani ni tosha! Sasa hizi bvr za nini? Khalafu kuhakiki ghost voters inakuwaje?
 
Back
Top Bottom