NEC hoi, itaharibu mambo

NEC hoi, itaharibu mambo

Anayelazima huu mchakato kum'make sana! Anayedanganya watu kuwa mchakato unaendelea vizuri na kura ya maoni itafanyika April 30 kum'make sana na ma.ta.ko yake!! Kwa ufupi UKAWA hapa wamepiga 3-0 maana walisema tangu mwanzo kuwa muda ni mfupi mno!! Lubuva ona aibu Mzee hili zoezi limebuma, hivi mtu huoni aibu mpaka unautangazia umma eti ulienda kuazima mashine za BVR Kenya na Nigeria, shenji kabisa yaani wenzio watumie kodi zao Wewe uende kuazima? AIBUUUUUUUU! NEC mmejivua nguo!!

Leo alfajiri kwenye TBCCM wamejitapa wanaleta BVR 2000*3 kwa kutumia Boeing 747 cargo plane
 
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwa sababu ya NEC. NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa, katika kuandikisha wapiga kura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.

Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.

NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.

NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Nakubaliana na wewe NEC ina mapungufu ya kimfumo na kiutendaji lakini kilichochoka; kiko taabani ICU sio NEC; bali ni serikali yenyewe ambayo imeshindwa kuiwezesha NEC kwa wakati na kikamilifu; mpaka Babu Lubuva anahaha huko na kule kwenda kuazima BVR kits?! kumbe wenzao huko alikokwenda; zoezi la kuboresha daftari la wapiga kura ni Continous; sio kama NEC yetu na Firebrigade style yao!!
 
Leo alfajiri kwenye TBCCM wamejitapa wanaleta BVR 2000*3 kwa kutumia Boeing 747 cargo plane

Wameenda kudurufu BVR machine fake ili kutuhadaa wananchi, fedha wamezitoa wapi wakati nchi iko hoi kifedha?
 
Hatauchaguzi mkuu hakutakuwa na cha maana kitakachokuwa kimefanyika
 
Mi nachokiona Lubuva anajiandaa kuwa Sita mwingine, kulazimisha vitu kutokana na matakwa ya watawala! Mi namuasa Jaji Mstaafu akajipumzikie ili hata aki rest in peace iwe kwa heshima yasije yakamkuta ya Komba!
 
Back
Top Bottom