Ndugu zangu wananichukia

Dada mwenye akili na maarifa tafuta mume mwema ujenge familia yako utayasahau yote hayo.
 
Are you married miss Jay?
Yaani wanawake wenye traits kama zako ni so rare kufind siku hizi.
 
cha kufanya usiwashirikishe tena na tena ktk biashara zako wala mipango yako.....hata ukitaka kujenga tena nunua kiwanja kimya kimya anza kujenga kimya kimya....achana nao kabisa wasahau ktk ratiba zako wamekutenda vya kutosha. huyo mama wa ajabu sana anamrudisha nyuma maendeleo ya mwanae..
 
anza kufanya mambo yako mwenyewe wasalimie tu hao ndugu zako ila wasiione hata senti moja yako,ingawa ningekuwa mimi ningewapotezea wote moja kwa moja hadi nafa.
 
Pole Sana Miss Jay. Mama ni mama tu hata awe na mapungufu gani ww jitahidi huyakubali tu. Msamehe bure ipo siku atagundua wapi alitenda kosa lake. Kuwaweka katika matabaka anakosea Sana . cha msingi Kama wadau wengine walivyochangia, jitahidi Sana kufanya mambo yako jirani na maeneo ambayo ni rahisi ww MWenyewe kufika na kusimamia kwa u karibu zaidi.
Nilitengwa hivyo na kaka zangu baada ya mama kufariki, sikupewa msaada kielimu tangu darasa la4. Baada ya kuhitim darasa la7 nikakaa miaka2 bila kuendelea na shule zaidi ya wao kunitumia kwa shughuli zao tu. Nikapigania mwnyewe na nikaanza shule 2008(secondary), 2012(diploma), ss nipo mwana wa2 degree ya irrigation na civil (Arusha technical college).
My take: usiache kumsaidia mama yako pale anapohitaji na pale utakapoweza. Pia usiache kuwaombea mema siku zote.
Maendeleo yako yapo mikononi mwako.
 
Hebu simama mwenyewe, fanya hao hawapo kabisa.....
 

Maisha ni darasa. Mshukuru Mungu umehitimu hiyo level na cheti umekabidhiwa.
Sasa ingia mzigoni maana wamekudhulumu pesa ila nguvu, akili uhai bado.

Piga kazi utatoka vizuri tu tena usiwachukie
 
Pole sana dear, wasamehe ila kuanzia wakati huu usiwashirikishe kwenye mambo yako ya maendeleo. Kaa mbali nao. Uende kuwaona mara moja moja tu tena kwa surprise.

Usiwang'ang'anie watu wasiokupenda na kukuthamini. Mkaribie Mungu...atakutetea atakupigania na kukusimamia issue zako pasipo ndugu zako.
 
Masikini weee fanya yako km ww usiendekeze ndugu zako maisha popote na silazima ujenge ulipo kulia unaweza ukaanza hapo ulipo na biashara ukaanza hapohapo ulipo
Unakofanyia kazi unapoona ndugu kikwazo kwako usiwaendekeze fanya yako
 
Mungu awabariki wote mlionishauri na kunipa moyo,,asanteni sana
 
 
Fanya yako kivyako watakutia umasikini.Tafuta sehemu ambayo una uhakika kama utaweza kuja kuishi jenga hapo.Mweke mungu mbele na usimwamini ndugu wala rafiki.Mambo yako yatakuwa unanyotaka pale utakaposimamia wewe mwenyewe
 
''..ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa..''
Nakupa pole kwa unayopitia ila mama yako sio ndugu yako
 
Pole sana dada yangu, fanya mambo yako achana nao hondoa mikono yako kwa. Na waangalie tu, na kaa kimya ukifanya mwenywe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…