Njombe: Tisa wahukumiwa kunyongwa mpaka kufa

VanDon

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
370
645
Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imewahukumu kunyongwa hadi kufa Washtakiwa tisa akiwemo Beatus Salum aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kipengere Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe kwa makosa ya mauaji ya Ndugu wawili mwaka 2020 Kijijini hapo.

Hukumu hiyo ya kesi ya mauaji namba 11 ya mwaka 2019 imetolewa na Hakimu Zabibu Mpangule mbele ya Washtakiwa, Mawakili wa utetezi na Mwendesha mashtaka ambapo amesema kwa kuzingatia makosa ya mauaji ya Watu wawili Francis Chaula na Fabio Chaula ambao ni Mtu na kaka yake Mahakama hiyo imewahukumu Washtakiwa wote kunyongwa hadi kufa.

Mahakama imesema mnamo April 27 , 2020 katika Kijiji cha Kipengere Washatkiwa wote waliwaua Francis Frank Chaula na Fabio Frank Chaula ambapo taarifa za uchunguzi wa miili hiyo iliyotolewa na Daktari ni kuwa sababu vifo vimetokana na kuvuja damu nyingi uliosababishwa kupigwa na vitu vizito.

Hakimu amesema mshtakiwa namba 6,7,8 na 9 ambao walikuwa ni Viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi wao wanaingia katika hukumu hiyo kutokana na kufanya vikao vilivyokuwa vikihusu mauaji kama ilivyoelezwa na mshtakiwa namba 5 kwenye kesi hiyo wakiwa na kisasi cha kumuua Frank Chaula kwasababu amekuwa akiwasumbua katika maeneo tofautitofauti.
#MillardAyoMAHAKAMANI.

FB_IMG_1696688010517.jpg
 
aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kipengere Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe kwa makosa ya mauaji ya Ndugu wawili mwaka 2020 Kijijini hapo.

Hukumu hiyo ya kesi ya mauaji namba 11 ya mwaka 2019 imetolewa na Hakimu Zabibu Mpangule mbele ya Washtakiwa,
Ina maana walifunguliwa kesi kabla ya mauaji au nimeelewaje
 
Back
Top Bottom