Naam, kuishi kivyako ndo kwenyewe.
Laiti watu wengi wangekuwa na falsafa kama yangu ya 'live and let live', basi mitafaruku ingekuwa michache sana hapa duniani.
Bahati mbaya uhalisia wa maisha hauko hivyo!
Kuna baadhi ya ndugu ni mtihani sana, hawezi kukutendea wema akanyamaza. Lakini tuvumiliane, hakuna mkamilifu, huenda hao tunaohisi wanatukwaza nao kwa namna moja au nyingine tunawakwaza pia bila kujijua.Ndugu wa hivi siwezi kabisa, miaka hii ni bora kuishi kivyako tu coz wenye uwezo wanalalamika, wasio na uwezo wanalalamika. Ya nini kumtembelea mtu ambaye atakutangaza kuwa ulienda kula ubwabwa kwake?
Hhahahah[emoji102] [emoji102] [emoji102] [emoji102] [emoji102]Mi ndugu zangu ni kulalamika tu eti siwapigii simu,wakati wao wenyewe wana simu na hawanipigii.
Kuna baadhi ya ndugu ukitaka amani mkutane kwenye harusi...ugonjwa na misiba tu....Ndugu wengi sana mimi nimewapotezea....
Nna ndugu yangu mmoja huyo sasa hivi kutwa ananiomba hela
nikimtafutia kazi anaanza kusema subiri kwanza sijui nini
ila hela kuomba haachi
ndugu mzigo
Ndugu ni ndugu na ndiyo undugu wenyewe huo mmoja akitoka, basi inaaminika kwamba umefungua njia.
Mimi ndugu zangu hua wanastukia tu kuniona nipo around na ntakuwa na ratiba zangu.
Huwa nawaambia kwamba msaada mkubwa kutoka kwangu ni kukusaidia ada ya kozi (ku-top up) unayosoma yenye kuja kukusaidia maishani au kunisaidia shughuli zangu za shamba au kukusaidia mawazo ya ujasirimali.
Halafu wanafahamu siwezi kukusaidia tu bila kuja na business plan, kama kuwa na Barber shop, hair dressing saloon, grosery shop na aina yoyote ile ya biashara.
Lakini mimi sio benki kwani wengine wanaomba hata mitaji kabisa kama 10,000,000 hivi.
Sasa hii si anaweza kuipata akienda benki na business plan yake?
Ila siwasahau ndugu zangu kwa vitu vidogovodogo ambavyo ukiwapa anaweza kuwa nacho wakati wote kama kofia, top original ya Arsenal na handset ya kawaida.
Akiwa nacho anakuwa akikukumbuka kwamba ndugu upo.
Halafu mkuu NN, jaribu kuwaunganisha ndugu zako kwenye WhatsApp Group ndiyo utaona hizo feeds za maombi na utaweza kuchuja zipi za kuzingatia.
WhatsApp inaleta togetherness baina ya ndugu na mnakuwa mkiwasiliana kila mara.
Hizo feeds zingine unapotezea tu.
Ndugu wengi sana mimi nimewapotezea....
Nna ndugu yangu mmoja huyo sasa hivi kutwa ananiomba hela
nikimtafutia kazi anaanza kusema subiri kwanza sijui nini
ila hela kuomba haachi
ndugu mzigo
Huwa unawaambia lakini au ndio unakuja kumalizia machungu JF?
Ohoo mimi tena? Sinaga simile hata kidogo.
Ni makavu bila vilainishi.
Atakayenichukia na anichukie.
Kwanza napenda kuchukiwa.
Hususan pale yule anayenichukia anapokuwa hawezi kufanya lolote zaidi ya kulialia kwa watu.
Wewe si ulisema ni msukuma? Ndivyo mlivyo wasukuma.Hivi na nyie wengine mnao ndugu wasio na shukrani?
Ndugu ambao hukukumbuka wakati wa shida zao tu?
Huwa mnakabiliana nao vipi watu wa aina hiyo?
Mimi wananikera sana kwa kweli.
Mtu anakuja na kukulilia shida zake lukuki, nawe kwa moyo mweupe kabisa unamsaidia.
Tena unamsaidia kwa kwenda mbali zaidi ya kile alichokiomba.
Cha ajabu [ingawa si ajabu kivile] ukishamsaidia tu, mwenzio anapotea.
Anapotea bila hata kutoa 'ahsante' ya msaada uliomsaidia.
Na akishapotea ndo imetoka hiyo. Kuja kusikia tena toka kwake labda ni awe na shida au kwenye msiba.
Hata salamu tu ya kujuliana hali toka kwake inakuwa tunu.
Naamini katika kutenda wema na kwenda zangu lakini pia sipendi mambo ya kufanyanya wapumb.avu.
Yaani kuniona nakufaa tu wakati wa shida zako. Ukiwa huna shida hata simu zangu hupokei.
Hovyo kabisa hao.....
Kuna baadhi ya ndugu ukitaka amani mkutane kwenye harusi...ugonjwa na misiba tu....
Vinginevyo lawama tu
Hivi na nyie wengine mnao ndugu wasio na shukrani?
Ndugu ambao hukukumbuka wakati wa shida zao tu?
Huwa mnakabiliana nao vipi watu wa aina hiyo?
Mimi wananikera sana kwa kweli.
Mtu anakuja na kukulilia shida zake lukuki, nawe kwa moyo mweupe kabisa unamsaidia.
Tena unamsaidia kwa kwenda mbali zaidi ya kile alichokiomba.
Cha ajabu [ingawa si ajabu kivile] ukishamsaidia tu, mwenzio anapotea.
Anapotea bila hata kutoa 'ahsante' ya msaada uliomsaidia.
Na akishapotea ndo imetoka hiyo. Kuja kusikia tena toka kwake labda ni awe na shida au kwenye msiba.
Hata salamu tu ya kujuliana hali toka kwake inakuwa tunu.
Naamini katika kutenda wema na kwenda zangu lakini pia sipendi mambo ya kufanyanya wapumb.avu.
Yaani kuniona nakufaa tu wakati wa shida zako. Ukiwa huna shida hata simu zangu hupokei.
Hovyo kabisa hao.....
Najua ninachokizungumzia hapa. Sijakurupuka tu bila kufanya na kujifanyia tathmini. Umakini wangu hauna mfano!Kabla ya kupeleka lawama/shutuma kwa ndugu zako hao kwanza jiulize, "Je mimi huwa nawatafuta ndugu zangu kuwajulia hali." Ikiwa jibu ni ndio basi una haki ya kushutumu; ila jibu likiwa ni hapana basi utakuwa na lile tatizo la Kiafrika la umungu mtu.
Kuna msemo unasema "Usichotaka kufanyiwa basi nawe usimfanyie mwenzio"
Kikawaida Waafrika tulio wengi tupatapo kitu (hasa uwezo wa kifedha) huwa tuna tabia ya kujiona kuwa sisi ni bora kuliko ndugu wasionacho na kuwaona kuwa wana wajibu wa kuwatumikia (kama sio kuwanyenyekea) kana kwamba wewe ndiwe Mungu wao duniani.
Ushauri wangu tu Bwana Nyani Ngabu....Kama ulikuwa huwatafuti nduguzo kuwajulia hali kama unavyotaka wakujulie hali basi anza wewe kufanya hivyo ili kujustify your innocence kabla ya kujudge nduguzo
Najua ninachokizungumzia hapa. Sijakurupuka tu bila kufanya na kujifanyia tathmini. Umakini wangu hauna mfano!
What a thought? Nimeipenda hii!Huwezi kumfurahisha kila mmoja, kuna mwezi nilikaa nikawa narekodi kila aliyenipigia simu kuomba hela bila kujali kama nimempa au la, mwisho wa mwezi nikajumlisha zote nikaona ilikuwa ni zaidi ya kipato changu. Hapo ndo nilipothibitisha kuwa siwezi kusaidia kila tatizo linalokuja mbele yangu, mwanzoni nilikuwa napata tabu sana navoona nashindwa kusaidia shida ya ukweli mpaka nakopa ili nimpe mtu mwingine ambao wengi huwa hawalipi au watachelewa sana kulipa