Ndugu wananiita mchawi wakati walilelewa na baba yangu mzazi

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi ni kijana wa miaka 37 kwetu tumezaliwa 2 tu, ila kuna ndugu zangu kama wanne (4) walilelewa na baba yangu mzazi katika makuzi yao, baada ya baba yangu kunifukuza nyumbani miezi 5 sasa imepita kisa tu nilimbembeleza kujiunga na chama changu cha mapinduzi, vile vile kupelekea kumfukuza na mama yangu pia ambaye alikuwa mara kwa mara uenda kudhuria vikao vya chama chetu cha mapinduzi, mimi nilimshauri mama yangu aende mahakaani kudai taraka ili waachane na baba wagawane mahari ili mimi na mama tukatafute sehemu yetu tukae tuepukane na manyanyaso ya baba

Mama baada ya kuondoka kwa baba alikuwa akikaa kwa dada yake ambaye anaishi maeneo ya Kijichi, sasa siku ya Jumamosi mama alinipigia simu kuwa anaenda kwa baba kudai taraka, baba akikataa kumpa taraka moja kwa moja anaenda mahakamani, siku ya Jumapili mama alienda moja kwa moja nyumbani kwa baba kudai taraka, ila kilichotokea ni kuwa mama tangu aende kwa baba pale nyumbani hajanijulisha chochote kile na nilikuwa nikipiga simu hapokei, jana jioni ndio aliniambia kuwa basi ameghailisha mambo ya taraka, ndugu zangu niliishiwa nguvu sana maana mama huwa ananisikiliza sana kwa kila kitu, nikahisi ndugu zangu watakuwa wanamchezea kiuchawi

Kumbukeni ndugu zangu sina kazi wala kibarua nahishi kwa marafiki tu, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yeyote yale nina degree ya marketing nimesoma pale UDSM-UDBS, nilitegemea hiyo hela ya mama akigawana mali na baba baada ya kupewa taraka na mimi nipate mtaji, nimeumia sana ndugu zangu, mpaka kupelekea ndugu wa upande wa baba kuniita mimi mchawi

Naombeni mwenye kazi yeyote anisaidie ndugu zangu napitia hali ngumu sana kimaisha na baba hanitaki kabisa kwake kisa tu nipo chama cha mapinduzi na alinitimua wakati mimi ni mtoto wa pekee wa kiume kwake, nilishamshtaki ofisi za kata ila kata wakasema mimi sina akili timamu, na najua baba aliwapa pesa wale viongozi wa ofisi ya kata ili kunikomoa na kuto kunisikiliza malalamiko yangu

Kwa sasa nipo Dar es Salaam Boko. Mwenye connection anisaidie
 
Sasa kwanini uhami hicho chama umekua mzee? Yaani hata baba ako anakuzidi fikra na degree yako. Yaani unang'ang'ana na Lichama limetuongoza miaka nenda rudi na hapo ulipo hata ajira huna eti wewe ni mwanachama wa ccm nenda kwa mwenyekiti wa ccm akupe ajira maana yeye ndio anaongoza nchi.
 
Sasa kwanini uhami hicho chama umekua mzeeee? Yani hata baba ako anakuzidi fikra na degree yako. Yani unang'ang'ana na Lichama limetuongoza miaka nenda rudi na hapo ulipo hata ajira huna eti ww ni mwanachama wa ccm nenda kwa mwentekiti wa ccm akupe ajira maana yy ndo anaongoza nchi.
Mkuu naomba unisaide kama una kazi mkuu
 
Wewe si ni mwanaume unalialia kurudi kwa baba yako ili iweje??

Pambana kutafuta maisha yako mwenyewe achana na mali za baba yako.

Una miaka 37 halafu bado uko kwenu? Bora amekufukuza maana unaonekana huna akili hata kidogo.
 
Wewe ni zaidi ya mchawi yani unataka kuwatenganisha Hadi wazazi wako kwa tamaa za mali je kuwauwa utashindwa?
Hufai hata kusaidiwa wewe Kwanza unaonekana ni mfitinishaji kama unawafitinisha Hadi wazazi wako ni nani atakae kusaidia na usimfanyie fitina?
Hapana mkuu mimi sina tabia ya ufitinishaji
 
Miaka 37 ila bado una utoto mwingi sana.

Punguza mihemko kijana!

Mambo ya siasa na family unataka kupeleka mji sisi wako (Nyumbani kwa baba yako)
 
Hakika wewe ni zaidi ya mchawi.Kama umefikia mahali pa kuvunja ndoa ya wazazi wako ili upate mali wewe ni mbaya kuliko shetani.Isitoshe umri wako si wa kuwa tegemezi tena.Baba yako ana haki ya kukufukuza kwake.Mtakaaje wanaume wawili ndani ya nyumba moja.Pumbavu sana wewe!Endelea kusota maana sidhani kuna mtu atakuajiri wewe.
 
hawajakosea, ni kweli wewe mchawi! Yaani ulikuwa unataka wazee waachane ili upate pesa? Yawezekana uchawi wako ulokuwa nao ndio unakuzibia riziki. Sijui kama kuna mtu humu anaweza kuajiri mtu ambae yupo tayari kufarakanisha ilimradi yeye apate chochote tu.

Sijui lakini.
 
Cjawah kuona ji2 jinga km hili.. hv unamshawish mamako aachane na babako 4 ur own benefit.? N then upo na miaka 37 n still upo home.. hayo matatzo ungenda kuyapeleka kwenye chama chako coz kuna ajira kbao hapo UBUNGE UDIWANI URAIS zote hzo umekosa mzee wangu NB: Huyo babako n mzazi au wakambo..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom