Ndugu wana JF, mwanangu ana kitu. Mko tayari kumsapoti?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Habari wana JF, ni mimi hapa nguli wa mapenzi, a.k.a mzee wa ovyo, hapa kitaani ukiulizia nyumbani kwa mzee wa matikiti kudondokeana unaletwa hapa mlangoni kwangu

Basi bhana, miezi miwili iliyopita nalisikia sauti kali mithili ya malaika wa peponi ikichomoza kutoka bustanini mida ya alfajiri. Hakuwa mwingine, bali mwanangu wa kiume ambaye ni mhitimu kidato cha nne. Japo nilivutiwa na kipaji chake, nilimkaripia vikali huku nikimtaka aandae akili yake akasome Pre Form Five

Mwanangu hana imani kabisa na elimu ya Tanzania. Ni vile tu baba yake sina pesa ya kumpeleka nchi ya nje. Hivyo anaamini katika kile kitu alichonacho kumkichwa. Ili kuthibisha hilo, nalisikia wimbo wake kwenye bars za sebureni kwangu ambazo huwa nazitumia kupigia nyimbo za urabu

Vipi wana JF, nimuendeleze kipaji chake ama niachane nacho? Kisije kuwa hakina manufaa kama elimu ya vyuo vikuu nikajutia!
 
😂😂Nahisi ni kitete tu, ama ni changamoto wanazokutana nazo huko kwenye mavyombo yao. Lakini kimazungumzo anazungumza vizuri sana, tena kiswahili kilichonyooka

Au huenda alirekodi kipindi TANESCO wanakata kata umeme. Hii nchi bhana😂
apo thawa mambie aimbe amapiano atatoka chaap aachane ba hz ngumu kumeza hip hop atotoka
 
Habari wana JF, ni mimi hapa nguli wa mapenzi, a.k.a mzee wa ovyo, hapa kitaani ukiulizia nyumbani kwa mzee wa matikiti kudondokeana unaletwa hapa mlangoni kwangu

Basi bhana, miezi miwili iliyopita nalisikia sauti kali mithili ya malaika wa peponi ikichomoza kutoka bustanini mida ya alfajiri. Hakuwa mwingine, bali mwanangu wa kiume ambaye ni mhitimu kidato cha nne. Japo nilivutiwa na kipaji chake, nilimkaripia vikali huku nikimtaka aandae akili yake akasome Pre Form Five

Mwanangu hana imani kabisa na elimu ya Tanzania. Ni vile tu baba yake sina pesa ya kumpeleka nchi ya nje. Hivyo anaamini katika kile kitu alichonacho kumkichwa. Ili kuthibisha hilo, nalisikia wimbo wake kwenye bars za sebureni kwangu ambazo huwa nazitumia kupigia nyimbo za urabu

Vipi wana JF, nimuendeleze kipaji chake ama niachane nacho? Kisije kuwa hakina manufaa kama elimu ya vyuo vikuu nikajutia!
HII NI BIG HIT SANA, MWANAO KWELI ANA KIPAJI.

Kwa ujasiri wako na jitihada za kumuunga mkono mwanao, ni wazi kwamba unamthamini sana na unataka kumsaidia kufikia mafanikio yake. Kipaji chake cha muziki kinastahili kuheshimiwa na kuendelezwa, kwani inawezekana kuwa ni njia yake ya kipekee ya kufikia malengo yake kama ilivyo kwa wasanii wengine waliofanikiwa hapa nchini kama Diamond Platnumz na Harmonize. Hata hivyo, ni muhimu pia kumpa mwongozo sahihi kuhusu umuhimu wa elimu na jinsi inavyoweza kumfungulia milango mingi katika maisha.

Ni vyema kumhimiza mwanao kuendeleza kipaji chake cha muziki, lakini pia kumpa msukumo wa kusoma na kujifunza kwa bidii. Kwa kufanya hivyo, anaweza kutumia elimu yake kama msingi wa kuimarisha kipaji chake cha muziki na kufanikiwa zaidi katika tasnia hiyo. Kumsifu kwa juhudi zake na kumwunga mkono katika safari yake ni hatua muhimu ya kujenga ujasiri wake na kumtia moyo kuendelea kufuata ndoto zake.
 
Shukhrani mkuu, nitajaribu kukaa naye chini nizungumze naye vyema🙏
 
Wimbo umeniliza, nimelia hadi kwikwi.....
😂😂😂Umenikumbusha wimbo mmoja wa kifaransa, niliusikia kwenye moja ya redio pale msibani, wimbo ulikuwa una melody ya kuuzunisha sana, ukatufanya tuunge machungu na kulia kwa moyo wote na kasi kubwa sana, uzuri ule wimbo nikawa nimeu-shazaam

Baada ya kufika nyumbani, nikautafutia lyrics, nikazipaste kwenye french to swahili web, nikakuta kumbe wimbo unahusu mambo ya kilimo, tena kilimo cha karafuu, kuanzia uandaaji wake hadi mavuno na masoko. Ila french bhana😂

Beat yake imekaa kama wimbo wa celine Dion wa It's all coming back to me
 
Aliyeiba Wimba Mbona Ni Wewe Unavaa Vazi La Mwanao
😂😂😂Awapi, na huu uze wangu mkuu, sauti la bezi lililosheheni urabu, domo kudondokeana na mawazo ya ovyo ya kukimbizana na tubinti twa sekondari, nawezaje kufanya hivi, mimi mzee wa ovyo?

Kwani huko studio huwa wanaingia na msuli? Maake vazi langu kuu ni tisheti yenye picha ya mama pamoja na msuli😂
 
Mwambie abadilishe uimbaji aje na uimbaje wa aina yake mwenyewe. Kwa huo uimbaji ambao huwezi kuutofautisha na wa akina Mboso, Diamond, Harmonize na wengineo ambao wameshajitambulisha hawezi kutoboa. Afanye kila njia ajitambulishe kwa uimbaji wake ambao ni tofauti na wengine. Halafu aache kuimba pitchy kwa kulazimisha
Nitajitahidi kumuelewesha, kwa kuwa ni mbunifu, natumai atabadilika. Wacha nimtafutie pesa niinvest kwenye wimbo wake utakaofuata, nione kama yaliyozungumzwa hapa atajaribu kuyafanyia kazi

Ahsante sana kwa ushauri mkuu🙏
 
Wakuu, nahitaji idea ya video ya huu wimbo. Tayari nimekwisha muandalia pesa ya kichupa

Iwe vipi? Nahitaji kuipeleka kwenye vituo vikubwa vya runinga hapa nchini
 
Back
Top Bottom