Ujengelele
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 1,253
- 22
Mimi nampenda asieruhusu uongo lakini pia simpendi asiesema kweli kama wewe.
Hili la TV (Kabla ya kuendelea ningeomba umri wako pengine hayo mambo umehadthiwa) linaukweli na aliloandika huyo unaemsuta. Naomba unijibu TV wakati huo zilikuwa zinauzwa duka gani? Kwa faida ya wanataka ukweli ni kuwa zilikuwa TV za magendo zilizoibwa Zanzibar.
Jambo la pili jee unakumbuka suwala la Wahujumu? Uliza watu watakueleza jinsi gani watu walivyotupa majalalani MaTV, sasa wakiogopa kitu gani kama ilkuwa ruksa?
TV hazikuwa zinauzwa Tanzania na kuna vitu chungu nzima ambavyo vilikuwa haviuzwi Tanzania watu waliruhusiwa kuviingiza kama walifuata taratibi zilizowekwa. Hao wote walioamua kutupa TV zao waliziingiza kwa njia za panya ili kukwepa kulipa ushuru waliostahili kulipa, hivyo walikuwa hawana documents zozote za kuthibitisha kama TVs zao waliziingiza nchini kihalali. Nakumbuka kuhusu Wahujumu na kweli kulikuwepo wahujumu wa uchumi ambao walikuwa wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha Serikali mapato ya mabilioni. Walikuwa wanahodhi bidhaa mbali mbali adimu na kuziuza kwa bei mbaya sana ili kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka. Walioingiza TVs zao kwa kufuata taratibu zilizowekwa ikiwa na pamoja na kulipia ushuru hawakutupa TVs zao. Wakati mwingine muwe mnaandikia ukweli badala ya kuandika uzushi ambao hauna ukweli hata kidogo.