Ndugu wa Tanzania Mnakielewa chanzo cha Misukosuko ya Nchi? (Ali H. Mwinyi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu wa Tanzania Mnakielewa chanzo cha Misukosuko ya Nchi? (Ali H. Mwinyi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Black Jesus, Dec 29, 2009.

 1. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alipoleta Azimio lake la zanzibar ndio ilikuwa mwanzo na mwisho kwa viongozi wa TZ kutokuwa na huruma zidi ya nchi na mali za uma ,hata mwalimu alipiga kelele sana ,kwa kiasi fulani mzee mwinyi hakuiletea mema TZ kama tunavyomsifia.alichokifanya baada ya kuwa Rais wa Tanzania ni Hadaa ya panya anakungaka unapokuwa umelala huku anakupuliza.
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Black Jesus unaufahamu msemo wa 'Shukurani za Punda mateke?' Basi ndio baadhi yenu nyinyi.

  Enzi zile kila kitu ilikuwa foleni foleni foleni - sabuni ya mawingu kwa foleni, vitenge TZ yote inavaa aina moja nayo ni kwa foleni. Watu walifikia hata kuvaa mifuko ya unga ngano (enzi zile mifuko ya kg 50 ilikuwa ya vitambaa), kuwa na TV au friji ni haramu, gari kuendesha mwisho saa nane mchana siku za jpili, kuwa na dola za kimarekani au foreign currency yo yote ni uhaini.

  Sera ya ujamaa na kujitegemea ni nzuri kinadharia lakini kiuhalisia haifanyi kazi. Na huo ni ukweli nyinyi vijana wa leo mubaki kuimba tu na kukumbuka mabaya badala ya kushukuru kwa yale maendeleo yaliyofanyika kwa kubadilisha sera zile.

  You are taking too many things for granted.
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  chanzo cha misukosuko nchini ni watanzania wenyewe.Acha kumsingizia Mwinyi.
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwinyi ni Great thinker! aliibadisha nchi kuipeleka kwenye right direction ambapo wakati ule Nyerer nchi ilikuwa imeshamshinda kuanzia:

  1. Ufisadi kwenye mashirika ya umma
  2. Economy meltdown
  3. Barabara hazipiptiki
  4. X-mass uwezi kwenda kwenu mabasi/gari hakuna
  5. Elimu mwisho darasa la saba only 25% waliendelea na masomo ya juu
  6. Zero justice, mgambo, mjumbe mwenyecheo anakuweka ndani bila kesi
  7. Nguvu kazi
  8. Kodi ya maendeleo
  9. Kula kwa kaya
  10. Wahindi na waasia ndio walio control biashara
  11. Wahizi walianza kuchomwa mote kwa kukosekana justice
  12. Nyere haambiliki
  13. Bunge halina sauti
  14. Wasomi na wanasiasa walikimbia nchi
  15. Kukosekana amani
  16. Vita na Uganda
  17. Uadui na majirani zetu(kenya, uganda, n,k)
  18. Nchi ilitaka kupindiliwa kipindi chake
  19. Ukifanya biashara unaitwa mlanguzi
  20. Ukabila, Jeshini na usalama wa nchi kaweka ndugu zake wakurya
  21. ubaguzi wa madaraka(wananchi wengine walisikia na kujiona isolated kwenye nchi yao)
  22. Naweza kukesha hapa kwenye keybord!!!!!!!!

  .
  . Utaacha nitowe machozi, bora kaa kimya kama umezalia 70s
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Vipi kati ya Mh. Kikwete, Mkapa na Mwinyi, yupi unamwona bora zaidi kwako na kwa Taifa la Tanzania ukimwacha Nyerere?!

  (Btw...Tafadhali usitoe machozi, kufanya hivyo ni hatari kwa computer yako - hayachelewi ku-short circuit keyboard yako!)
   
 6. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe binti mkongwe umeamua kuandika uwongo, nami sitauruhusu uwongo huu ubaki kama ulivyo. Si kweli kwamba ilikuwa haramu kuwa na TV au friji. Binafsi nawafahamu Watanzania wengi waliokuwa na TV enzi za Mwalimu na walikuwa wanaangalia station ya Zenj au Kenya kwa wale walio kaskazini. Kulikuwa na makampuni kama DABCO na RTC ambayo yalikuwa yanauza friji.

  Mwaka 73 kulitokea matatizo makubwa ya upatikanaji wa Petroli na hii ilisababisha bei ya petroli duniani kupanda kwa kasi sana na hata nchi za magharibi ziliathirika sana. Nakumbuka US kulikuwa na foleni za kutisha za wenye magari wakisubiri petroli kwa masaa chungu nzima na halii hii pamoja na uchumi kuanguka kutokana na athari za bei ya mafuta na kuwa adimu kulisababisha Jimmy Carter akae madarakani kwa kipindi kimoja tu.

  Kutokana na matatizo hayo ya mafuta Serikali ikaamua kubana matumizi ya magari ya Serikali na ya mashirika ya umma kila siku ya Jumapili kuanzia saa nane mchana lakini wenye magari binafsi waliruhusiwa kuyaendesha (kama nakumbuka vizuri) lakini wakati huo Watanzania waliokuwa na magari yao binafsi walikuwa wachache mno.

  Pia ni lazima ukumbuke jinsi Sera za Nyerere zilivyopigwa vita na nchi za magharibi. Hivyo hii iliathiri kwa namna moja au nyingine kupatikana kwa bidhaa mbali mbali

  Swali kwako baada ya kuzikumbatia sera za kibepari tangu wakati wa Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete je Watanzania tumeona maendeleo yoyote ya kuridhisha ukilinganisha na enzi za Mwalimu? au tumeona jinsi wageni wakishirikiana na wateule wakifanya wizi wa mapesa chungu nzima na kupora rasilimali zetu?
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ondoka Bana We! Mzee kifimbo alishakufa? Au la Azimio la Arusha aliona aibu lakini la serikali tatu alikuja juu!
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi nampenda asieruhusu uongo lakini pia simpendi asiesema kweli kama wewe.
  Hili la TV (Kabla ya kuendelea ningeomba umri wako pengine hayo mambo umehadthiwa) linaukweli na aliloandika huyo unaemsuta. Naomba unijibu TV wakati huo zilikuwa zinauzwa duka gani? Kwa faida ya wanataka ukweli ni kuwa zilikuwa TV za magendo zilizoibwa Zanzibar.
  Jambo la pili jee unakumbuka suwala la Wahujumu? Uliza watu watakueleza jinsi gani watu walivyotupa majalalani MaTV, sasa wakiogopa kitu gani kama ilkuwa ruksa?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyo huyo Great Thinker ndiye aliyeuza mbuga zetu za Loliondo kwa Waarabu. Alaaniwe!
   
 10. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2009
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Ama kweli, tunasahau mno upesi! Sera ya soko huria ilipitishwa 1984, Mh Alhaji Mwinyi alichaguliwa kuongoza nchi 1985! Uamuzi wa watanzania wa au kuwa na sera ya vyama vingi ama la ulipigiwa kura (referandum) na wengi wakataka wabaki na chama kimoja, Nyerere akalazimisha pamoja na haja ya kuheshimu demokrasia, nchi haikuwa na budi walau wakati ule kuupa uzito uamuzi wa wachache yaani kuchagua kuwa na sera ya vyama vingi. Ni pale Zanzibar tu ambako hatujui kilichojiri, hakuna sera yeyote iliyowekwa wazi pale, ni vurugu tu! Sasa wewe Bimkonge na wengine, mnawezaje kudhani Mwinyi ndiye aliyeboresha sera wakati unaona kabisa Nyerere akiwa ni kinara wa kuleta soko huru (1984) na sera ya vyama vingi(1991)?

  Lakini yote tisa, sera na mfumo sio miliki ya mtu mmoja!!! Hata huko Marekani, hakuna kinachobadilika eti tu kwa kuwa yupo Obama, yale yale yanaendelea, ni harafu tu ya juu tunayoona kama kihalalisho cha kuwepo aliye katika madaraka....habari ndio hiooo
   
 11. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,720
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  umenikuna hapo kwenye namba 14.

  nakumbuka jinsi tulivyokuwa tukimuimba vibaya marehemu Oscar Kambona kwenye mchakamchaka huko st govt primary school. nikitazama nyuma sioni kosa lake zaidi ya kutofautiana ki-misimamo na mwalimu...pengine sijui sana...niko tayari kuelimishwa.
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nijuavyo mimi hakuna kinara wa mabadiliko bali msimamizi/kiongozi wakati mabadiliko hayo.Kinara wa mabadiliko ni mabadiliko yenyewe yanayoletwa na mfumo wa mazingira.Mwinyi hakulazimisha mabadiliko bali mabadiliko yalimlazimisha kufanya hayo aliyofanya yawe mazuri au mabaya.
  Mkumbuke kuwa historia huandikwa kwa mabaya na mazuri ya mtu/mfumo.
  Alichokifanya Mwinyi,kilimshinda Nyerere hadi kuamua Kung'atuta,Mwinyi kwa ujasiri mkubwa akakubali mabadiliko ili kuendana na mfumo wa dunia.
  After all AZIMIO LA ZANZIBAR LILIHALALISHA UFISADI,RUSHWA NA USHENZI MWINGINE TUNAOUONA LEO?
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wasomi waliokimbia nchi sasa wamerejea na wanaitafuna hazina ya nchi BOT!
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Sijakuelewa eti sera ya soko huria ilipitishwa 1984 lakini Nyerere akaamuwa angatuke? Hakuwa na ubavu wa soko huria?
  Bado alisimamia sera hiyo!
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Common sense is not common
   
 16. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mbona mtei alitofautiana na mwalimu lakini hakukimbia nchi???????

  NI KUTOFAUTIANA GANI UKO KIMSIMAMO KULIMFANYA KAMBONA AKAKIMBIA???
   
 17. m

  matambo JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sera za soko huria na zilizoletwa na mzee mwinyi zilikuwa nzuri kulingana na mabadiliko yaliyotokea duniani kipindi kile,bahati mbaya twaweza sema mzee mwinyi hakupata viongozi waliokuwa na uchungu wa kweli na nchi yetu,wengi walijilimbikizia mali au walishindwa kusimamia miradi waliyopewa hii ndiyo iliyopelekea kudorora kwa uchumi katika miaka ya mwisho ya utawala wake
  lakini yote kwa yote mabadiliko mengi CHANYA yalitokea katika kipindi cha mzee ruksa ana nafasi yake ya kushukuriwa kwa aliyoitendea tanzania, kama vile nyerere alivyo na nafasi yake ya kulaumiwa kwa kuididimiza tanzania,maana laiti angeacha sifa za kuchukua pato na rasilimali za nchi kuzitumbukiza kwenye vita za ukombozi wa afrika labda tungekuwa mbali kwani wale tuliowasaidia kukomboka wanatusaidia nini leo?
   
 18. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hili azimio kwa vile linanuka basi ni la Zanzibar!!!
  Hebu vunjeni huo muungano na murudishe hayo maazimio mema ya Arusha, mutuwachie vijisiwa vyetu wenyewe tujipake mafuta ya karafuu!

  Kelele tupu, kila baya imekuwa Zanzibar ndio chanzo.Lakini cha kufurahisha,kwanini Tanganyika imekuvikumbatia visiwa hivyo?
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  ujue kutofautisha vitu, ndugu. kuna soko huria upande mmoja na azimio la zanzibar upande mwingine. soko huria hatulilaumu bali ni hilo azimio la zanzibar. hata mimi naanza kupata picha hapo kuwa hilo azimio ndio chanzo cha matatizo kwani linawahusu viongozi moja kwa moja
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mkewe ndie aliekuwa great thinker kwa ufahamu wako, ila haya mambo wakati mwingine ni ajali ya kimazingira na muda tu. Nyerere ni mtu wa msimamo na alitaka kusimamia kile kilicho sawa japo hatupingi kuwa alikosea wakati mwingine. haya mambo yana hatua (evolution). mabadiliko yaalikuwa ni jambo la lazima, ila kwa vile Baba wa Taifa hakupenda kuishia kuwa kama akina Kaunda na Mugabe, aliamua kuwaachia wengine wayafanye hayo mabadiliko
   
Loading...