Ndugu Mkullo ,Shaffiq & Hannif brothers hawalipi kodi , je ulijua haya ?

Mkuu Lunyungu,
Hawa TRA ni dudu lingine linaloila hii nchi.Mimi nakwambia hakuna kitu ambacho TRA hawakijui ambacho ni potential kwa mapato na wasiwe na mkono.
Kule Arusha wachimbaji wa Tanzanite toka SA wanachimba na kujifungia madini na kisha kuandika ripoti jinsi wanavyotaka wao, huku maafisa wa TRA wakiwa Arusha mjini wanakunywa bia na kusubiri kuletewa hizo ripoti wasaini tu. Wakiambiwa safari hii hawakupata kitu, hamna noma, wakiambiwa tuepata kilo moja tu ni sawa. Ripoti nyingi za kamati ya ulizi na usalama za mkoa ambazo hutumwa wizara husika na ikulu huonyesha kasoro hizo lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa. Haya yalishamiri na kuota mizizi kipindi cha utawala wa awamu ya tatu.
 
Back
Top Bottom