Ndugu kanyanyuka kitandani, anatembea huku akiwa usingizini

Ndugu kanyanyuka kitandani, anatembea huku akiwa usingizini

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Wakuu kuna jamaa yangu nilikua nimelala nae mara imefika mida ya saa saba usiku ghafla akanyanyuka kitandani uku yupo usingizini tena anakoroma akaenda mpaka nje uani mara akarudi ndani akachukua maji kwenye friji akanywa uku bado yuko usingizini tena anakoroma mara akawasha radio na kurudi kitandani yaani ajabu yenyewe anafanya yote haya akiwa yupo usingizi anakoroma wala hajikwahi wa kujigonga sehemu yoyote. wakuu nataka nimpeleke hospital lakini nataka ushauri wenu labda kuna mwenye idea yoyote na hii kitu. karibuni
 
Hahahahaaaaaaaa,jini hilo ila halina madhara kwako kwani zimwi likujualo,halikuli ukakwisha,

Cc:Maalim MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Ni kawaida kuna watu wa namna hiyo

Hakikisha kabla ya kulala silaha zote umefungia
 
Nenda jukwaa la Intelijensia kule kuna manguli wa mambo ya ndoto na yanayoendana tena kuna mtu ana tatizo kama hilo la swahiba wako na kaelimishwa vizuri sikumbuki uzi unaitwaje ila upo.
 
Nenda jukwaa la Intelijensia kule kuna manguli wa mambo ya ndoto na yanayoendana tena kuna mtu ana tatizo kama hilo la swahiba wako na kaelimishwa vizuri sikumbuki uzi unaitwaje ila upo.

ngoja niwatembelee mkuu
 
mkuu una maanisha anaweza kugeuka janjawidi usiku?

Anamaanisha kwamba anaweza kuota yuko anang'oa visiki sasa kama upo karibu kichwa chako kinaweza geuka moja ya visiki anavyo ving'oa ohoo!
 
Nna mdogo wangu tulikuwa tunalala chumba chetu nje Tu pana choo Cha public sasa ilitokea siku moja. Alitoka na kuingia chumba cha wazazi usiku akiwa amelala na kujibanza nyuma ya mlango na kukojoa kama vile Yupo kichakani,kesho yake mama kudeki chumba anakutana na Nyoka mweusi tulikisia alipita dirishani na kukaa ndani akila mijusi na mende.mwisho tulimuuwa Lakin ni maajabu.
 
Wakuu kuna jamaa yangu nilikua nimelala nae mara imefika mida ya saa saba usiku ghafla akanyanyuka kitandani uku yupo usingizini tena anakoroma akaenda mpaka nje uani mara akarudi ndani akachukua maji kwenye friji akanywa uku bado yuko usingizini tena anakoroma mara akawasha radio na kurudi kitandani yaani ajabu yenyewe anafanya yote haya akiwa yupo usingizi anakoroma wala hajikwahi wa kujigonga sehemu yoyote. wakuu nataka nimpeleke hospital lakini nataka ushauri wenu labda kuna mwenye idea yoyote na hii kitu. karibuni
Mkuu pole sana ana Jini huyo ndie anaye mfanya awe hivyo. Mtafute Mchungaji kama wewe ni Mkristo amfanyie maombi,la kama ni Muislam mtafute Sheikh amsomee dua ampatie dawa. Au kama unanihitaji mimi nitafute mimi kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
Back
Top Bottom