Ndugai tena na mitaala ya elimu

Ndugai tena na mitaala ya elimu

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
4,781
Reaction score
3,213
Katika hali ya kushangaza leo naibu spika ametangaza kuwa serikali imetekeleza wajibu wake wa kuleta ile mitaala ya kichina bungeni kama walivyoagizwa kuwa iwasilishwe leo tarehe 06.02.2013 na baada ya kuwasilishwa kwa Spika , eti ameunda kamati ya kuchunguza kama mitaala hiyo ni halali ama laa.

Swali, kama imeletwa na serikali inakuwaje Bunge lisiiamini serikali kiasi kwamba mpaka wachunguze kama hiyo mitaala ni halali ama laa, na ni kwanini isingegawiwa kwa wabunge ili aliyetoa hoja aseme kuhusiana na kadhia hiyo?

Ina maana SPika haiamini serikali na nyaraka za serikali ?
Itakuwaje kuhusu nyaraka nyingine za serikali Bungeni , kila moja itaundiwa kamati ya kuchunguza uhalisia wake?
Nini tafsiri ya hatua hii mpya ya Bunge kukosa imani na nyaraka za serikali mpaka wazichunguze kwanza kabla ya kuwasilishwa Bungeni?
Hii kamati yake si inaenda huko huko serikalini kuhoji , kuhusiana na uhalali wa mitaala hiyo?
Kama leo ndio tunachunguza uhalali wa mitaala , vipi kuhusiana na wanafunzi ambao wamelishwa mitaala ambayo hata Bunge halina imani nayo , watapewa fidia? Waliofelishwa na mitaala hiyo watafidiwa?
 
Ndugai ni janga sugu la wazawa" kesha kuwa chzi mkuu c unajua ukipatwa na aibu lazima uwe na kimuyemuye
 
Ngungai anaogopa kauli ya Mbatia -- alisema kama mitaala ipo basi ubunge basi -- kazi kweli kweli

hiyo kamati haitakaa itoe majibu -- hence hoja pending kama zingine..... "mwenye swali???? ---- tunaendeleaa...."
 
Hebu tufike ,mahali tuachane na hizi sarakasi za ndugai. Wakati mwingine unajiuliza hii jeuri ya kulichezea bunge huyu mjinga anaipata wapi?
 
Tukimwacha ni sawa na kususia bucha kwa fisi wenye njaa kali......unategemea jioni wakupe fedha za mauzo ya nyama .....
 
Kwani huyu Ndugai analala wapi hapo Dodoma? Barlow alifanywa nini? TAFAKARI
 
Suspended Domain

This account has been suspended.
Either the domain has been overused, or the reseller ran out of resources.
 
Kuna mwenye SoftCopy aiweke huku tuipitie????

Am sure utakuta ni Copied toka "Inji" nyingine.
 
Hivi hakuna jinsi yoyote ya sie wananchi kupinga hizi mambo pale mjengoni? Anaejua anisaidie jamani kama tunauwezo wa kumwadabisha huyu ndugai in any ways.
 
Kuna mwenye SoftCopy aiweke huku tuipitie????

Am sure utakuta ni Copied toka "Inji" nyingine.

Hard copy yenyewe imechukua wiki kutafutwa , na baada ya kutafutwa ndio inaenda kukaguliwa kama ni sahihi ama feki, hiyo soft itapatikana wapi? Banana Republic........
 
Huyu Ndugai ni mwehu kweli, nimemsikia akisema kuwa kwa kuwa leo ni siku ya ukeketaji duniani , yeye Jimboni kwake huwa wana utamaduni wa kukeketa na wanawake wamesafiri kutoka Jimboni kwake na kumtaka awafundishe wabunge umuhimu wa kukeketwa kwa wanawake .

Huyu jamaa kumbe anaunga mkono ukeketaji wa wanawake , sasa ndio naibu Spika, mnategemea Bunge litunge sheria ya kuzuia ukeketaji kweli hapo? Hivi wanaharakati hawawezi kuandamana kupinga kauli hii ya naibu Spika? Uko wapi ueledi wa naibu spika?
 
Katika hali ya kushangaza leo naibu spika ametangaza kuwa serikali imetekeleza wajibu wake wa kuleta ile mitaala ya kichina bungeni kama walivyoagizwa kuwa iwasilishwe leo tarehe 06.02.2013 na baada ya kuwasilishwa kwa Spika , eti ameunda kamati ya kuchunguza kama mitaala hiyo ni halali ama laa.

Swali, kama imeletwa na serikali inakuwaje Bunge lisiiamini serikali kiasi kwamba mpaka wachunguze kama hiyo mitaala ni halali ama laa, na ni kwanini isingegawiwa kwa wabunge ili aliyetoa hoja aseme kuhusiana na kadhia hiyo?

Ina maana SPika haiamini serikali na nyaraka za serikali ?
Itakuwaje kuhusu nyaraka nyingine za serikali Bungeni , kila moja itaundiwa kamati ya kuchunguza uhalisia wake?
Nini tafsiri ya hatua hii mpya ya Bunge kukosa imani na nyaraka za serikali mpaka wazichunguze kwanza kabla ya kuwasilishwa Bungeni?
Hii kamati yake si inaenda huko huko serikalini kuhoji , kuhusiana na uhalali wa mitaala hiyo?
Kama leo ndio tunachunguza uhalali wa mitaala , vipi kuhusiana na wanafunzi ambao wamelishwa mitaala ambayo hata Bunge halina imani nayo , watapewa fidia? Waliofelishwa na mitaala hiyo watafidiwa?

Kitu kidogo kamati,mnatafuna pesa zetu tu yaani kila mkikaa mnawaza kamati tu.Mitaala KAMATI!!!!!!?
 
Huyu Ndugai ni mwehu kweli, nimemsikia akisema kuwa kwa kuwa leo ni siku ya ukeketaji duniani , yeye Jimboni kwake huwa wana utamaduni wa kukeketa na wanawake wamesafiri kutoka Jimboni kwake na kumtaka awafundishe wabunge umuhimu wa kukeketwa kwa wanawake .

Huyu jamaa kumbe anaunga mkono ukeketaji wa wanawake , sasa ndio naibu Spika, mnategemea Bunge litunge sheria ya kuzuia ukeketaji kweli hapo? Hivi wanaharakati hawawezi kuandamana kupinga kauli hii ya naibu Spika? Uko wapi ueledi wa naibu spika?

kesha jisahau anaamini anaweza fanya lolote na kufanya chochote na asitokee mtu wa kumuajibisha ,ndiyo maana aliwaita wabunge hawajabarehe!na hakuna aliye mwajibisha!
 
wandugu ni sarakasi hiyo,ulizeni walimu huo mtaala una rangi gani? Hawajui
 
Ili janga Watanzania tulitaka wenyewe kwa kuchagua watu bila kuhoji uwezo wao hata kidogo!eti kuna jinga moja tena ni lisanii la kike liliwahi kupost kwy facebook page yake kua tumchague m.k.w.e.r.e kwa kua ni handsome!useless kabisa!hviongozi wamejaa sanaa tupu!hv ni nani asiyejua kua mtaala wa elimu ulianza kupotea enzi za Joseph Mungai?waliofuata ndio wakaja kuharibu kabisa!na wanaotharika na ilo ni wadogo zetu na watoto zetu,si watoto wa Mbatia,Zitto,Makinda wala Mbowe,lakini bado yapo majitu tena mengine ni graduates (wasomi vyeti bila uelewa) yanashabikia na kusupport ujinga huo kwa kigezo cha chama!bure kabisa
 
Wamekesha kuuchapa huo weekend yote mpaka jana usiku leo ndio wameuleta,waache waendelee na sarakasi tunawasubiri kitaa!!!!!!!!!
 
Katika hali ya kushangaza leo naibu spika ametangaza kuwa serikali imetekeleza wajibu wake wa kuleta ile mitaala ya kichina bungeni kama walivyoagizwa kuwa iwasilishwe leo tarehe 06.02.2013 na baada ya kuwasilishwa kwa Spika , eti ameunda kamati ya kuchunguza kama mitaala hiyo ni halali ama laa.

Swali, kama imeletwa na serikali inakuwaje Bunge lisiiamini serikali kiasi kwamba mpaka wachunguze kama hiyo mitaala ni halali ama laa, na ni kwanini isingegawiwa kwa wabunge ili aliyetoa hoja aseme kuhusiana na kadhia hiyo?

Ina maana SPika haiamini serikali na nyaraka za serikali ?
Itakuwaje kuhusu nyaraka nyingine za serikali Bungeni , kila moja itaundiwa kamati ya kuchunguza uhalisia wake?
Nini tafsiri ya hatua hii mpya ya Bunge kukosa imani na nyaraka za serikali mpaka wazichunguze kwanza kabla ya kuwasilishwa Bungeni?
Hii kamati yake si inaenda huko huko serikalini kuhoji , kuhusiana na uhalali wa mitaala hiyo?
Kama leo ndio tunachunguza uhalali wa mitaala , vipi kuhusiana na wanafunzi ambao wamelishwa mitaala ambayo hata Bunge halina imani nayo , watapewa fidia? Waliofelishwa na mitaala hiyo watafidiwa?

Kweli Serikali imekuwa na ubabaishaji,Mitaala imefuatwa Dar Es Salaam?!!,kwani kama ilikuwepo wangeenda kwenye idara ya Elimu hapo Dodoma,au waende Sekondari au Shule ya Msingi yoyote iliyopo Dodoma ili kupata nakala inayotumika mashuleni iletwe BUNGENI kama ushahidi wa kuwepo na kutumika kwa Mitaala mashuleni.?

Inawezekana kuna changa la macho,Bunge linasubiri Mtaala utoke DAR? kwani Mtaala hautumiki kwenye shule zilizopo hapo DODOMA? yaani kila kitu kipo Dar?hata huo Mtaala unatumika Dar? siyo kwa nchi nzima?!
 
Yaani,kweli Spika anashindwa kutafakari,Mtaala mpaka ufuatwe Dar?,kwani Dodoma Mtaala haupo mashuleni?!!
Mtaala uliopo katika shule za hapo Dodoma ndio ingekuwa ushahidi wa kuwepo na kutumika kwa Mitaala mashuleni.
Sasa wabunge,wanasubiri Waziri alete Mtaala kutoka Dar?
 
wanaweza kutuletea mtaala wa mwaka 1958.mpaka naibu spika ameutilia shaka? Mhhh tusubirie
 
Siyo kuifuata Dar tu Hiyo mitaala!ajabu imechukua karibia wiki kuifuata utafikiri
alikuja Dar kwa baiskeli!,kwanini mtu kwenye akili timamu asiamini kuwa Kuna
namna?,binafsi hawa Watu nilishawaona uwezo wao kamwe hawawezi kunidanganya uwa nashangaa kwa wale ambao bado wanafikiri kuwa wanajipya!
 
Back
Top Bottom