Ndugai: JOHO LA SPIKA LINAKUPWAYA

....................Mkuu huyu naibu spika nilitaka hata kulia leo wakati anawatoa wabunge wa CDM...ni muhuni kabisa,anaonenya upendeleo wa wazi wakati hakuna haki kabisa....nina hasira na huyu mtu ile mbaya.Mungu nisaidie!!!
 
Soma post kwa umakini siyo unakimbilia kujibu tu. Kwa hiyo kama mimi ni magamba unashitaki kwa nani? Huu ni mtandao wa kijamii na watu tunabadilishana mawazo humu na si mtandao wa Chama chochote uwe na chama usiwe na chama unaingia tu huulizwi!!
Yashangaza sana anashtaki kwa nani? Ili iweje? jituuu kuubwa bure tu...kama una hoja mwenyewe ya kumpinga Kimbunga si uandike tuone na si kukimbilia ku single out oooh wewe magwanda huyu vile....grow up
 
Bunge lililopita (namaanisha lile ambalo Sitta alikuwa speaker) lilivutia sana na sikupenda kupitwa na mijadala iliyokuwa inaendelea mule ndani. Tofauti na leo ambapo kila siku ya Mungu kuna kituko. Bunge limekuwa kama primary school vile ambapo mbabe anaweza kumkaba mwenziye,, kisa.....yeye mtemi.
Sasa sijui sababu ni speaker kuzidiwa, au wenyeviti nao kuzidiwa? Lakini pia pengine tuliamini kuingiza vijana bungeni kwa vyama vyote kungeleta tija na kasi ya haraka kuelekea mageuzi ya kweli ya maendeleo?? Nadhani hali imekuwa kinyume,, tuliyoyashuhudia kipindi hiki, ni aibu kuu na ni utovu wa nidhamu kutoheshimu kanuni za Bunge. Bunge linaendeshwa kwa kanuni na si kiholela kama wengine wanavyotaka liende. Nilitamani siku za mbele nigombee lakini sasa sitaki tena, nafsi imeingia jivu, bora niendele na umachinga tu.

Tatizo sio bunge la Spika Sitta hapa? Tangu huyu mama kuchukua uspika na huyu Ndugai sijui,watu walionyesha wasiwasi wao kuwa ni njama za CCM kutafuta mtu wa kulinda maslahi yao baada ya kuona CDM na wapinzani wameongezeka bungeni....kinachoendelea bungeni sio utoto kama unavyosema bali ni matokeo ya CCM na maspika,wenyeviti wao kulinda maslahi ya CCM.........Ninawapongeza sana wabunge wa NCCR na CDM kwa kazi nzuri...
 
Back
Top Bottom