Ndugai: JOHO LA SPIKA LINAKUPWAYA

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Kama kiongozi wa Bunge nilitarajia Ndugu Job Ndugai awe Neutral na Asimamie Kanuni bila Kujali Mbunge anatoka Chama Gani. Ndugai ametetea Maneno ya kuudhi yaliyotolewa na Sitta dhidi ya Wabunge wa Upinzani, Ndugai ameyaunga mkono na kuyapa Uzito maneno hayo ( Namuomba tu asiwe Mkali akisikia Maneno kama hayo kutoka Upande mwingine wa Chama).

Ndugai aidha hajui majukumu ya Speaker au Amelewa Ukada lakini Namuambia Ndugai Wananchi wanaangalia Bunge na wanaona Namna gani ulivyojika Userikali na Kutetea Kila Uozo unaotolewa na CCM

Ndugai analifanya bunge kukosa Staha kabisa.

Ndugai Joho la Speaker linakupwaya ni Bora Ulivue
 
Ccm hakuna msafi,haupaswi kutarajia lolote toka kwa huyo naibu spika mwenyewe,spika na hata wenyeviti.
 
Unajua hawa ccm wanaona 2015 ni mbali sana, na wanahisi haitafika. Wanadhani baada ya bunge la bajeti wataendelea kuishi humo humo bungeni. Wanadhani tutasahau huu uozo itakapofika 2015 wakati huo wanapiga magoti kuomba kura.

Wacha tujenge uvumilivu ingawa inauma sana. Mzee wa Urambo 6 naye sijui kawaje, anawaita wenzake wanafiki!! eti watafia upinzani!! Yeye wakati anaanzisha CCJ si alitegemea awe mpinzani, kwa hiyo angekuwa mnafiki kwa kutofautiana na ccm??

Mzee 6 heshima yako imeporomoka ghafla kuliko wewe unavyodhani, and it ia too late. Subiri 2015.
 
Bunge lililopita (namaanisha lile ambalo Sitta alikuwa speaker) lilivutia sana na sikupenda kupitwa na mijadala iliyokuwa inaendelea mule ndani. Tofauti na leo ambapo kila siku ya Mungu kuna kituko. Bunge limekuwa kama primary school vile ambapo mbabe anaweza kumkaba mwenziye,, kisa.....yeye mtemi.
Sasa sijui sababu ni speaker kuzidiwa, au wenyeviti nao kuzidiwa? Lakini pia pengine tuliamini kuingiza vijana bungeni kwa vyama vyote kungeleta tija na kasi ya haraka kuelekea mageuzi ya kweli ya maendeleo?? Nadhani hali imekuwa kinyume,, tuliyoyashuhudia kipindi hiki, ni aibu kuu na ni utovu wa nidhamu kutoheshimu kanuni za Bunge. Bunge linaendeshwa kwa kanuni na si kiholela kama wengine wanavyotaka liende. Nilitamani siku za mbele nigombee lakini sasa sitaki tena, nafsi imeingia jivu, bora niendele na umachinga tu.
 
unajichanganya .....! yaani hueleweki upo upande gani! but unaonekana unawatete akinaMagamba...!
 
unajichanganya .....! yaani hueleweki upo upande gani! but unaonekana unawatete akinaMagamba...!
Naona wewe umeingia kwa fujo humu, na kwa vile unalipwa basi kila post yako unataka ionekane ime base wapi hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo. Wengine tunatoa maoni tu na hoja bila kujali tumeegemea wapi. Post 24 so far..........you need to work hard kid ili ulipwe. kazi ni kwako
 
Mkuu kweli Bunge ni HUNI. Na siyo Bunge letu na Uhuni. Bunge ndilo HUNI. Mimi nimekuwa nikifuatilia vikao vya bunge na kugundua kuwa mkusanyiko wa Wabunge ni UHUNI mtupu. Kama si uhuni inakuwaje watu wanafanya maamuzi makubwa ya kitaifa kwa kwa makelele ya NDIYOOOOOOOO au SIYOOOOOOO! Huo si uhuni ni nini? Hivi ukisimama bila kuwasha kipaza sauti ili speaker ama Mwnyekiti akuone asipokuona ama akijifanya hakuoni utafanya nini? Mimi nitapiga kelele ili anione. Ukipiga kelel ili uonekane unatolewa nje!! Huo ni UHUNI tu.

Mimi nadhani kanuni za Bunge ndio mwanzo wa UHUNI kwa kuwa hazitoi haki sawa. Ili kuondoa UHUNI wa speaker na Wabunge inabidi watu waketi chini waangalie kanuni upya vinginevyo hakuna namna Bunge litaendelea kuwa HUNI.
 
Nimesoma michango yako mingi mkuu inaonekana ww ni mwana Magamba mzuri sana kama natania wenzangu jaribuni kusoma kazi za wengine mtamuona huyu jamaa,Magamba ndio wanaleta utumbo huo unaouliza hapa,kila kitu ndiyoooooooooooo kazi mnayo nyie watu
 
Bunge lililopita (namaanisha lile ambalo Sitta alikuwa speaker) lilivutia sana na sikupenda kupitwa na mijadala iliyokuwa inaendelea mule ndani. Tofauti na leo ambapo kila siku ya Mungu kuna kituko. Bunge limekuwa kama primary school vile ambapo mbabe anaweza kumkaba mwenziye,, kisa.....yeye mtemi.
Sasa sijui sababu ni speaker kuzidiwa, au wenyeviti nao kuzidiwa? Lakini pia pengine tuliamini kuingiza vijana bungeni kwa vyama vyote kungeleta tija na kasi ya haraka kuelekea mageuzi ya kweli ya maendeleo?? Nadhani hali imekuwa kinyume,, tuliyoyashuhudia kipindi hiki, ni aibu kuu na ni utovu wa nidhamu kutoheshimu kanuni za Bunge. Bunge linaendeshwa kwa kanuni na si kiholela kama wengine wanavyotaka liende. Nilitamani siku za mbele nigombee lakini sasa sitaki tena, nafsi imeingia jivu, bora niendele na umachinga tu.

Kama kuongea ukweli na kutoa hoja ambazo zinagusa na zinatetea maisha na haki ya wananchi wengi wanyonge na maskini ni uhuni basi acha huo uhuni uendelee. Hiyo ni strategy ya nyie magamba, kujifanya mnafata kanuni kumbe mnazima hoja za msingi. The more you do that ndio mnavozidi kuwapa point CDM. Aluta Continua!!!
 
Kazana mkubwa hii ndio ajira yako uliopewa na nape,uraiani magamba yamebana ajira zetu so kazana kupost ili ulipwe.
 
Nimesoma michango yako mingi mkuu inaonekana ww ni mwana Magamba mzuri sana kama natania wenzangu jaribuni kusoma kazi za wengine mtamuona huyu jamaa,Magamba ndio wanaleta utumbo huo unaouliza hapa,kila kitu ndiyoooooooooooo kazi mnayo nyie watu

Soma post kwa umakini siyo unakimbilia kujibu tu. Kwa hiyo kama mimi ni magamba unashitaki kwa nani? Huu ni mtandao wa kijamii na watu tunabadilishana mawazo humu na si mtandao wa Chama chochote uwe na chama usiwe na chama unaingia tu huulizwi!!
 
Nimesoma michango yako mingi mkuu inaonekana ww ni mwana Magamba mzuri sana kama natania wenzangu jaribuni kusoma kazi za wengine mtamuona huyu jamaa,Magamba ndio wanaleta utumbo huo unaouliza hapa,kila kitu ndiyoooooooooooo kazi mnayo nyie watu

Afadhali mshamgundua..halafu akiishiwa hoja anaanza kutukana. Njaa hizi, acha tu. Mtu mzima anatumikishwa kama robot isiyojua kufikiri
 
Kuna kanuni mkuu mule ndani, la sivyo kila mtu angekuwa anajiwashia tu si ingekuwa mnada?

Mkuu naona umeng'ang'ania kanuni tu hebu toa ufafanuzi kanuni zipi hizo?, tuone je kama zinakuwa applied impartial. Unajua ninaamini kabisa ndani ya CCM kuna watu makini sana wanaojua kuwa bunge hili limeharibiwa na kutokuwepo kwa impartiality on parlimentary leadership. Siku zote ukitaka kufanikiwa katika kuongoza viumbe wenye akili kama zako na hata kushinda zako usioneshe kabisa kuwa unaegemea upande gani. Speaker wa bunge alitakiwa ajipatie neutral position na kuacha politics zichezwe na vyama husika. Inapotokea speaker anaegemea upande mmoja wazi wazi ana create mazingira yafuatayo.

  • Kwa upande wa chama anachokipendelea (Hapa ni CCM): Anatengeza mentality kwa wabunge wa upande huu kuwa sisi ndiyo wenyewe na tutafanya chochote kile na kulindwa na mtu wetu, hivyo kuwafanya watu hawa wawazomee wapinzani wawakejeli na kuwadhihaki, hatua hii isipokemewa na speaker inazalisha mentality kama hizo hizo upande wa pili (Yaani upinzani). Kwa kuwa hawa hauna huruma nao unatoa maamuzi yaleyale ya kipuuzi na mwisho wa siku unashindwa kuli-control bunge, ikifikia hapo legitimacy na credibility yako speaker inakuwa imefikia ukingoni.
  • Wapinzani wanapoona kuwa si tu haki haitendeki dhidi yao bali hata wananchi wanaofuatilia mjadala huo wanaona hivyo, unakuwa umewapatia wapinzani political boost na kuona kuwa the only way ni kuzidi ku go-rogue kwa kuwa kila unapowachukulia hatua inakula kwako na chama chako. Unakuwa unaondoa public support, japo kwa chama kama CCM public support is not an issue to them kwa kuwa wanashikilia state organs, hivyo kwao wao wananchi is not their primary concern zaidi ya kuwa-please power tycoons watakao kaa vikao vya kuwapitisha kugombea tena, kwa akili zao wanajua kuwa ukigombea kupitia CCM tayari wewe umeshashinda kwa kuwa watatumia dola kujitangaza washindi. Huu ni ujuha ambao sasa hivi unatakiwa kukomeshwa. Nina hakika kama wabunge wa CCM wangekuwa wanategemea kura za wananchi kwa 100% wangekuwa shocked pale mpinzani anapotamka kitu kuwa ni pro bono publico (kwa manufaa ya umma).
 
Ndugu zangu,

nimemvumilia huyu naibu spika nimechoka, napatwa na hasira na namna anavyojiona yeye ni perfect kuliko wengine na kwa hakika ni mwenye kiburi sana na kujiona kupita maelezo,

mwanzoni alipo Chaguliwa kua N/spika alianza nyodo zake kwa kuwapig vijembe wapinzani kwamba waache hasira na kutoka nje, then alipoendelea kusimamia mijadala ya bunge ndio tukauona upumba wake hasa.

anakandmiza wazi upinzani kisha anatoa vjimaneno vyake vya kebehi " kiti cha spika kinatenda haki" anafikiri wote ni wendawazimu hatuoni kinachotendeka, yeye ni mpendeleaji mkubwa wa CCM na ni mlamba miguu wa serikali kwa hiyo asijidai ni mtenda haki wakati kwa hakika ni mnyonyaji mkubwa wa haki za wabunge hasa wa upinzani/CDM.

ana tafsiri sheria kwa matazamo wake au tuseme kibabe, halafu utamsikia soon akijishaua " hakuna mtu anaependa ubabe, nyie wabunge miaka mitano si mingi". jamani huyu ninahofu ni mbumbu wa sheria zaidi ya kuelekezwa kunyonya haki za wapinzani, ningependa sana kujua CV yake hasa shule yake na kama ana uelewa wa sheria ipasavyo au kawekwa pale kiisadi fisadi kutetea watawala?

ndugu J.Ndugai usifikiri wananchi hatuoni au wote tuna mtazamo finyu kama wako, time will tell utajua kwamba HATUDANGANYIKI, na hata ukizidi ukandamizaji bado wananchi tunaona umuhimu wa wabunge wa upinzani ambao wewe unawakandamiza, jua kwamba unazidi kuwastawisha wapinzani wako bila wewe kujua.
cheo ulichonacho ni dhamna tu na hakidumu milele, wewe endelea kupendelea na kunyonya wengine huku ndg zako wakiendelea kuteseka na hali ngumu ya maisha

SUMU YA UKANDAMIZAJI INAYOFANYWA KWA UPINZANI HASA CHADEMA NI KAMA MBOLEA YA KUWASTAWISHA NA KUWAKUZA MBELE YA UMA SIKU HADI SIKU
 
tena ni spika mwenye mambo ya ajabu kwa kufanya personal attack kwa mtu, mfano kamshambulia mch Msigwa kwa cheo chake cha dini na kujifanya muumini safi, hakika ningekua kiongozi wako wa dini ningemtenga kwa kua yeye ni mnafiki zaidi ya mafarisayo wa enzi za nabii ISSA hafai kua muumini wa kweli kama anavyojidai
 
Back
Top Bottom