Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

Imekuaje wamemkosa?

Hata mimi nashangaa wamemkosaje! Hivi hawa wanaKongwa hawajui hata kurusha mishale ya sumu? Wanunue pinde wakimkuta tena wakati mwingine wamtungue!
 
Ndugai ana gundu kali sana ! Kila anapokuwepo ni vurugu tu , akawaangukie wazee jimboni kwake apunguze mikosi , vinginevyo ataumia muda si mrefu .
 
leo mnapinga ongezeko la viwango vya ushuru. kesho mnalalamika serikali haiwaletei maendeleo jimboni. idiot

Ongeza kuwa: Keshokutwa mnawapigia kura haohao mnaowagomea leo!
 
tpaul acha uchochezi


Hao vijana ni wajinga sana sasa usilipe ushuru maendeleo yataletwa na nini?


Hivi inaingia akilini mtu kutetea watu wasilipe ushuru? Halafu unashabikia apasuliwe kichwa ili iweje?

mods toeni hii thread imejaa uchochezi na chuki

Issue si kutokulipa ushuru, tatizo ni ushuru kulipwa zaidi ya mara nne kwa kitu kile kile kwenye halmashuri ileile.

Mahindi wanapoyatoa shamba karibu kila kila kijiji wanapoyapitisha kila gunia linalipiwa ushuru wa TSh 1,000. Wakifika kwenye soko kuu la mahindi Kibaigwa getini wanalipa ushuru, wakipima mzigo mizani unalipia tena ushuru kwa mahindi hayohayo, na mwsho atakayenunua hayo mahindi akitaka atoke nayo sokoni analipia pia tena ushuru. Kwa mtindo huu kwa nini wasilalamike?
Tatizo ni njia tu waliyotumia kudai madai yao.
 
Last edited by a moderator:
hao wanaoshikiliwa cha moto watakiona

tatizo ni ndugai kweli na sio wewe? Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Nyie wenyewe mmewajengea kiburi ndio maana wanawarudi. Wewe unajiita ccm au chadema, kweli wewe ni chadema au ccm? Wewe ni mtawaliwa tu, usipojenga musitakabali wako utanyanyasika hadi siku ya kuanza kuoza. Document ya warioba tulidhani ndio ungekuwa mwanzo wa kubadilika tumerubuniwa tunabishana wenyewe kwaa wenyewe eti serikali mbili serikali tatu, wao wanapeta. Ndugai huyo huyo ni spika, mbunge, diwani, sijui nani ccm, sijui mjumbe kamati gani wewe hata chai huna lakini ndiye wa kwanza kujiita mimi ccm unapata nini? Kwa hali hii hata wakija cuf au chadema wataendeleza mlo huo huo. Ndugu zangu tubadilike. Kweli wewe unaijua tanzania kuliko warioba, jaji ramadhani, salim ahmed salim, butiku, nk? Wao wanatafuta nini mnadanganywa na wenye madaraka mnakubali!
 
Hapa tatizo la ndugai liko wapi sijaona kuhusika kwake yeye hafanyi kazi kwenye halmashauri kwamba yeye ndiyo kaweka viwango vya ushuri.
Hawa wafanyabiashara walipe kodi wanataka kuingiza mali zao sokoni bure hii siyo sawa hata chembe.

Mkuu, mbona unajitoa akili? Wananchi hawakatai kulipa kodi---wanachokataa ni kuongezewa kodi kinyemela ambazo haziendani na thamani ya mazao yao. Unajisikiaje pale mabwanyenye wanaposamehewa kodi yenye thamani ya tsh bilioni 1.8 huku walalahoi wakikomaliwa kulipa tsh 1,000 tu?
 
Issue si kutokulipa ushuru, tatizo ni ushuru kulipwa zaidi ya mara nne kwa kitu kile kile kwenye halmashuri ileile.

Mahindi wanapoyatoa shamba karibu kila kila kijiji wanapoyapitisha kila gunia linalipiwa ushuru wa TSh 1,000. Wakifika kwenye soko kuu la mahindi Kibaigwa getini wanalipa ushuru, wakipima mzigo mizani unalipia tena ushuru kwa mahindi hayohayo, na mwsho atakayenunua hayo mahindi akitaka atoke nayo sokoni analipia pia tena ushuru. Kwa mtindo huu kwa nini wasilalamike?
Tatizo ni njia tu waliyotumia kudai madai yao.

Acha uongo na unafiq wewe
 
tpaul acha uchochezi


Hao vijana ni wajinga sana sasa usilipe ushuru maendeleo yataletwa na nini?


Hivi inaingia akilini mtu kutetea watu wasilipe ushuru? Halafu unashabikia apasuliwe kichwa ili iweje?

mods toeni hii thread imejaa uchochezi na chuki

umezoea kila siku kuwaamrisha mods wanafuta nyuzi zangu? wewe ni kilaza sana. kaa utulie sindano iingie. unauliza maendeleo yataletwa na nini? maendeleo yataletwa na tsh bilioni 1.8 zinazopotea kupitia misamaha ya kodi kwa mabwanyenye. wewe unaona tsh 3,000 ndio zinazoleta maendeleo zaidi kuliko tsh 1.8 bilion? Ndugai apigwe tu!
 
Last edited by a moderator:
Utaona uongo na unafiki kwa kuwa wewe unaeleza ulichosimuliwa, mimi naeleza ninachokiona na kukijua.

mkuu, lipuuze hilo likasuku Lusungo, linabishia hata jambo ambalo liko wazi kabisa.
 
leo mnapinga ongezeko la viwango vya ushuru. kesho mnalalamika serikali haiwaletei maendeleo jimboni. idiot

Kwani ushuru umeanza kukusanywa leo mkuu?tatizo fedha zinazopatikana zinaenda kushibisha matumbo ya watu, ushawahi kufika wilaya ya kongwa uone ilivyo?its pathetic ndo maana watu hawa hawataki tunu za taifa kama uwazi na uwajibijikaji kwa ulaji wao hata mchwa ana afadhali.
 
Nchi hii bana, wawekezaji wenye mapesa mengi wanasamehewa ushuru wanyonge wanaokula mlo mmoja kwa siku wanazidi kukamuliwa. Ama kweli naungana na wanaosema Tanganyika iingizwe kwenye maajabu ya dunia.
 
Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana waliokuwa wakipinga ongezeko la ushuru wa mazao na kuvamia ukumbi wa mkutano wa Kilimo uliopo Kibaigwa, wilayani Kongwa.

Katika vurugu hizo, ambazo zililazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji, pia mali mbalimbali ziliharibiwa, likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema vurugu hizo zilitokea juzi saa 7.30 mchana katika Mji mdogo wa Kibaigwa. Alisema jumla ya watu 34 wanashikiliwa wakihusishwa na vurugu hizo.

Misime alisema vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300, wakishirikiana na wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.

Alisema bango lililong’olewa ni la tangazo la kuzuia wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

Kamanda huyo alisema viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu Julai Mosi mwaka jana. Kwa mujibu wa viwango vipya, ushuru wa gunia la kilo 100 za karanga ulipanda kutoka Sh1,000 hadi Sh3,000, gunia la mahindi kutoka Sh500 hadi Sh1,000, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Sh500, gunia la mashudu Sh1,000 na gunia la alizeti Sh1,000. Viwango hivyo vinapingwa na wabeba mizigo.

“Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga Barabara kuu ya Dodoma –Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi, pia walivamia maduka na baa za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu na kusababisha uharibifu mkubwa,” alisema Misime.
 
Siungi mkono fujo ila ni kama vile serikali inaelekea kuelewa vurugu zaidi kuliko malalamiko ya wananchi!!!!

Huu sio mwendo mzuri asilani ukizingatia wengine wanalipwa vizuri bila kulipa kodi
 
Back
Top Bottom