Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

huyu jamaa asipojirekebisha atachezea kichapo cha umma si siku nyingi !
 
5/07/2014 habari za kitaifa

Vurugu kubwa Kibaigwa mkoani Dodoma.....Gari la mbunge lapigwa mawe, Maduka yavunjwa...Gari la Polisi nalo lavunjwa vioo, Watu 34 wakamatwa

Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 34 wakazi wa Mji mdogo wa Kibaigwa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali tukio lililotokea tarehe 05/05/2014 majira ya saa 13:30Hrs.

Kamanada wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya miatatu wakishirikiana na Wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa, walifanya maandamano bila kibali na kung'oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa lenya tangazo la kutoruhusu wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

Viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu tarehe 01.07.2013 ambapo gunia la Kg. 100 za karanga zilipanda kutoka Tshs. 1000/= hadi Tshs 3000/=, guina la mahindi lilipanda kutoka Tshs. 500/= hadi Tshs. 1000/=, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Tshs. 500/=, gunia la mashudu lilianza kutozwa Tshs. 1000/=, gunia la alizeti lilianza kutozwa Tshs. 1000/= ushuru ambao unapingwa na wabeba mizigo.

Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma mataili, pia walivamia maduka na bar za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.

Kamanda MISIME amesema katika vurugu hizo walisababisha uhalibifu wa mali kwa kushambulia magari kwa mawe likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mh. OMARI NUNDU lenye namba za usajili T.419 CWC Land Cruiser Prado ambaye aliyekuwa akienda Bungeni Dodoma, pia gari la Polisi namba PT. 0960 Land Rover lilivunjwa kioo cha mlango wa mbele kulia na basi la Kampuni ya Shabaha lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam lilivunjwa kioo cha mbele.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao kibaigwa kupinga kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba linawakosesha kufanya kazi zao kwani wateja wanashindwa kuingiza mazao sokoni na wao kukosa kazi.


source: MPEKUZI

 
Tusipoziangalia vizuri hizi CIVIL UNREST - na wakati tunawapa wajumbe wa BUNGE zaidi ya Sh. 300.000.00 kwa siku

Tutaelekea kule tusikokutaka hata JESHI litashindwa...
 
Haki ya mtu hudaiwa na kudai lazima damu imwangike hivyo hacha wapige tu maana mizengo peter pinda kashasema wapige tu,nawaunga mkono kabisa maisha ni magunu huku mtaani na kazi hamna then mh ni 300000 per day it's right for that...
 
Watapigwa tu mpaka kielweweke--na bado! Yaani hawa wajinga wanakaba mpaka penati wakati kuna mishahara hewa ya Tsh 1.5 trilion imeibiwa na mafisadi wa CCM na hakuna mtu aliyesurubishwa mpaka sasa? Walaaniwe viongozi wote wanaochumia matumbo yao badala ya kuchuma kwa ajili ya maendeleo ya nchi! Wakati wananchi wanakufa kwa njaa, yenyewe yananenepeana kama nguruwe!!! Haya majamaa ni zaidi ya mafisi, maana fisi akila anasaza mifupa--lakini yenyewe yanakula hadi mifupa, huku wananchi wakizidi kukamuliwa kila uchao! Ipo siku kitaeleweka tu.

CCM wataiua nchi.jpg


magamba yamenenepeana.jpg


fisi.jpg
 
Watapigwa tu mpaka kielweweke--na bado! Yaani hawa wajinga wanakaba mpaka penati wakati kuna mishahara hewa ya Tsh 1.5 bilion imeibiwa na mafisadi wa CCM na hakuna mtu aliyesurubishwa mpaka sasa? Walaaniwe viongozi wote wanaochumia matumbo yao badala ya kuchumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi! Wakati wananchi wanakufa kwa njaa, yenyewe yananenepeana kama nguruwe!!! Haya majamaa ni zaidi ya mafisi, maana fisi akila anasaza mifupa--lakini yenyewe yanakula hadi mifupa, huku wananchi wakizidi kukamuliwa kila uchao! Ipo siku kitaeleweka tu.

View attachment 156564


View attachment 156562


View attachment 156563


Umasikini ulionao hautaondoka kwa wivu na kupiga demo kijana fanya kazi kwa bidii
 
Watapigwa tu mpaka kielweweke--na bado! Yaani hawa wajinga wanakaba mpaka penati wakati kuna mishahara hewa ya Tsh 1.5 bilion imeibiwa na mafisadi wa CCM na hakuna mtu aliyesurubishwa mpaka sasa? Walaaniwe viongozi wote wanaochumia matumbo yao badala ya kuchuma kwa ajili ya maendeleo ya nchi! Wakati wananchi wanakufa kwa njaa, yenyewe yananenepeana kama nguruwe!!! Haya majamaa ni zaidi ya mafisi, maana fisi akila anasaza mifupa--lakini yenyewe yanakula hadi mifupa, huku wananchi wakizidi kukamuliwa kila uchao! Ipo siku kitaeleweka tu.

View attachment 156564


View attachment 156562


View attachment 156563

KWA NIABA YA FAMILIA YANGU NAOMBA nikUSHUKURU KWA PICHA , HASA HIYO YA FISI !
 
Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana waliokuwa wakipinga ongezeko la ushuru wa mazao na kuvamia ukumbi wa mkutano wa Kilimo uliopo Kibaigwa, wilayani Kongwa.

Katika vurugu hizo, ambazo zililazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji, pia mali mbalimbali ziliharibiwa, likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema vurugu hizo zilitokea juzi saa 7.30 mchana katika Mji mdogo wa Kibaigwa. Alisema jumla ya watu 34 wanashikiliwa wakihusishwa na vurugu hizo.

Misime alisema vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300, wakishirikiana na wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.

Alisema bango lililong’olewa ni la tangazo la kuzuia wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

Kamanda huyo alisema viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu Julai Mosi mwaka jana. Kwa mujibu wa viwango vipya, ushuru wa gunia la kilo 100 za karanga ulipanda kutoka Sh1,000 hadi Sh3,000, gunia la mahindi kutoka Sh500 hadi Sh1,000, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Sh500, gunia la mashudu Sh1,000 na gunia la alizeti Sh1,000. Viwango hivyo vinapingwa na wabeba mizigo.

“Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga Barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi, pia walivamia maduka na baa za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu na kusababisha uharibifu mkubwa,” alisema Misime.


Source:
Mwananchi

MAONI YANGU:
Ndugai amekuwa akifanya ubabe sana akiwa bungeni. Ikiwa ataendeleza ubabe wake hadi jimboni kwake, wananchi watampasua kichwa. Lakini suluhisho la kudumu kwa wabunge wababaishaji kama hawa ni kuwanyima kura ktk uchaguzi mkuu ujao. WanaKongwa mtoseni huyu adui yenu wa maendeleo ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Maskini ndugai anafikiri wananchi wana mkataba naye. Watu wamechoka. Angekuwa Mbeya wangekuwa wameshamrekebisha kabisa.
 
Binafsi hua nashangaa sana. Utakuta mtu kama huyo ukifika wakati wa uchaguzi wananchi wanampa kura za kutosha kabisa kuwa mbunge baada ya kuwapa mlungula wa khanga, vitenge, fulana, kofia, chumvi na sukari lakini mara tu baada ya uchaguzi wananchi haohao wanageuka na kuanza kulalamika.

Mimi nawashauri wananchi wanaobahatika kupiga kura siku ya uchaguzi wachague mwakilishi bila kuangalia chama wala kujali milungula wanayopewa, kisha walinde kura zao mpaka matokeo kutangazwa.

Kuhusu kukoswakoswa kwa mbunge wa Kongwa liwe fundisho kwa wabunge wengine wa aina hiyo.

Namalizia kwa kunukuu kauli ya waziri mkuu wa Tanganyika pamoja na kuiboresha kidogo, "Wale wabunge wanaokaidi matakwa ya wananchi waliowachagua wapigwe tu maana tumechoka sasa, nami nasema wapigwe tu, ee wapigwe"

kuwa mtanzania ni kutojitambua, ndani ya tanzania wote ni wageni na hakuna raia mwenye haki, turudi kwetu tanganyika, tutajua haki zetu, tutazipigania na hatutakubali kuongozwa na wasanii kama hao.
 
Haiyaaaaaaaaaa, Hajapigwa? Da bahati mbaya, manake Pinda alisharuhusu wapigwe.
 
Umasikini ulionao hautaondoka kwa wivu na kupiga demo kijana fanya kazi kwa bidii

nifanye kazi kwa bidii kwa manufaa ya mafisadi? thubutu! yaani nilime mahindi kwa gharama ya tsh 300 kwa kilo halafu mafisadi wanilazimishe niwauzie kwa tsh 250 kwa kilo na kunizuia kuuza nje? kalime wewe unayeweza kufanya biashara ya kiuwendawazimu kama hiyo! unadhani hata ningelima kwa bidii kiasi gani nitapata faida kweli? acha kutumika kama 22cer mkuu! tumia akili zako binafsi, usitegemee akili za kuambiwa.
 
Back
Top Bottom