Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

CCM wanatakiwa kujifunza kwa matukio madogo madogo,kuwa kwenye NJAA hakuna AMANI!Na pia wajue WaTanganyika walipoamua kupigania UHURU walikuwa wamechoshwa na mabavu ya wakoloni,na hii ndiyo inayokuja Watanzania wameanza kuchoshwa na mabavu wafanyiwayo na viongozi.Wastuke sasa kumekucha.
 
Hao Bavicha huwa hawana kazi za kufanya badala yake wanakaa vijiweni kupanga wizi, uporaji, ubakaji kama walivyofanya huko.
 
Hao Bavicha huwa hawana kazi za kufanya badala yake wanakaa vijiweni kupanga wizi, uporaji, ubakaji kama walivyofanya huko.

Acha mambo ya kifedhuli hao uvccm ndio wamefanya nn?
 
Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana waliokuwa wakipinga ongezeko la ushuru wa mazao na kuvamia ukumbi wa mkutano wa Kilimo uliopo Kibaigwa, wilayani Kongwa.

Katika vurugu hizo, ambazo zililazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji, pia mali mbalimbali ziliharibiwa, likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema vurugu hizo zilitokea juzi saa 7.30 mchana katika Mji mdogo wa Kibaigwa. Alisema jumla ya watu 34 wanashikiliwa wakihusishwa na vurugu hizo.

Misime alisema vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300, wakishirikiana na wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.

Alisema bango lililong’olewa ni la tangazo la kuzuia wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

Kamanda huyo alisema viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu Julai Mosi mwaka jana. Kwa mujibu wa viwango vipya, ushuru wa gunia la kilo 100 za karanga ulipanda kutoka Sh1,000 hadi Sh3,000, gunia la mahindi kutoka Sh500 hadi Sh1,000, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Sh500, gunia la mashudu Sh1,000 na gunia la alizeti Sh1,000. Viwango hivyo vinapingwa na wabeba mizigo.

“Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga Barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi, pia walivamia maduka na baa za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu na kusababisha uharibifu mkubwa,” alisema Misime.


Source:
Mwananchi

MAONI YANGU:
Ndugai amekuwa akifanya ubabe sana akiwa bungeni. Ikiwa ataendeleza ubabe wake hadi jimboni kwake, wananchi watampasua kichwa. Lakini suluhisho la kudumu kwa wabunge wababaishaji kama hawa ni kuwanyima kura ktk uchaguzi mkuu ujao. WanaKongwa mtoseni huyu adui yenu wa maendeleo ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Wanapaswa wajifunze kwa aliyekuwa diwani wa kisesa ndugu Mabina
 
Hao Bavicha huwa hawana kazi za kufanya badala yake wanakaa vijiweni kupanga wizi, uporaji, ubakaji kama walivyofanya huko.

Wewe ndiyo huna kazi ya kufanya,ndiyo maana usiku kucha unachumia tumbo kwa ma ccm
 
leo mnapinga ongezeko la viwango vya ushuru. kesho mnalalamika serikali haiwaletei maendeleo jimboni. idiot

Maendeleo kwa kodi ya sh 1,000? Hata Nyerere aliwahi kusema 'Serikali corrupt haikusanyi kodi, inakimbizana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani'
 
MAONI YANGU:
Ndugai amekuwa akifanya ubabe sana akiwa bungeni. Ikiwa ataendeleza ubabe wake hadi jimboni kwake, wananchi watampasua kichwa. Lakini suluhisho la kudumu kwa wabunge wababaishaji kama hawa ni kuwanyima kura ktk uchaguzi mkuu ujao. WanaKongwa mtoseni huyu adui yenu wa maendeleo ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hata msipo wachagua, tume ya taifa ya uchaguzi na usalama wa Taifa wapo.
 
Safi sanaa na wapigweee tuuuu tumechoka upuuuz
 
Hapa tatizo la ndugai liko wapi sijaona kuhusika kwake yeye hafanyi kazi kwenye halmashauri kwamba yeye ndiyo kaweka viwango vya ushuri.
Hawa wafanyabiashara walipe kodi wanataka kuingiza mali zao sokoni bure hii siyo sawa hata chembe.
 
tpaul acha uchochezi


Hao vijana ni wajinga sana sasa usilipe ushuru maendeleo yataletwa na nini?


Hivi inaingia akilini mtu kutetea watu wasilipe ushuru? Halafu unashabikia apasuliwe kichwa ili iweje?

mods toeni hii thread imejaa uchochezi na chuki
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom