Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

Ndugai anusurika kupigwa na wananchi

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,982
Reaction score
25,371
Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana waliokuwa wakipinga ongezeko la ushuru wa mazao na kuvamia ukumbi wa mkutano wa Kilimo uliopo Kibaigwa, wilayani Kongwa.

Katika vurugu hizo, ambazo zililazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji, pia mali mbalimbali ziliharibiwa, likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema vurugu hizo zilitokea juzi saa 7.30 mchana katika Mji mdogo wa Kibaigwa. Alisema jumla ya watu 34 wanashikiliwa wakihusishwa na vurugu hizo.

Misime alisema vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 300, wakishirikiana na wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa walifanya maandamano bila kibali na kung'oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.

Alisema bango lililong'olewa ni la tangazo la kuzuia wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

Kamanda huyo alisema viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu Julai Mosi mwaka jana. Kwa mujibu wa viwango vipya, ushuru wa gunia la kilo 100 za karanga ulipanda kutoka Sh1,000 hadi Sh3,000, gunia la mahindi kutoka Sh500 hadi Sh1,000, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Sh500, gunia la mashudu Sh1,000 na gunia la alizeti Sh1,000. Viwango hivyo vinapingwa na wabeba mizigo.

"Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga Barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi, pia walivamia maduka na baa za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu na kusababisha uharibifu mkubwa," alisema Misime.


Source:
Mwananchi

MAONI YANGU:
Ndugai amekuwa akifanya ubabe sana akiwa bungeni. Ikiwa ataendeleza ubabe wake hadi jimboni kwake, wananchi watampasua kichwa. Lakini suluhisho la kudumu kwa wabunge wababaishaji kama hawa ni kuwanyima kura ktk uchaguzi mkuu ujao. WanaKongwa mtoseni huyu adui yenu wa maendeleo ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Wangelipopoa hilo dudu lilidhani liko bungeni likiwaongoza maccm wenzake alah watu wa namna hiyo hawana nafasi ktk umma wa watanzania.

BACK TANGANYIKA
 
Daah, yamefika hapo tena? Ataanza kutembea na gari zenye tinted
 
Wananchi hasa wapiga kura wanatakiwa kusoma alama za nyakati lakini wamgemtia hata alama kidogo ikawa ukumbusho kwake ndugai.
 
Ndo tatizo la kushiba hilo. Ukiambiwa mtu hana mkate unailiza hata cake amekosa?
 
Binafsi hua nashangaa sana. Utakuta mtu kama huyo ukifika wakati wa uchaguzi wananchi wanampa kura za kutosha kabisa kuwa mbunge baada ya kuwapa mlungula wa khanga, vitenge, fulana, kofia, chumvi na sukari lakini mara tu baada ya uchaguzi wananchi haohao wanageuka na kuanza kulalamika.

Mimi nawashauri wananchi wanaobahatika kupiga kura siku ya uchaguzi wachague mwakilishi bila kuangalia chama wala kujali milungula wanayopewa, kisha walinde kura zao mpaka matokeo kutangazwa.

Kuhusu kukoswakoswa kwa mbunge wa Kongwa liwe fundisho kwa wabunge wengine wa aina hiyo.

Namalizia kwa kunukuu kauli ya waziri mkuu wa Tanganyika pamoja na kuiboresha kidogo, "Wale wabunge wanaokaidi matakwa ya wananchi waliowachagua wapigwe tu maana tumechoka sasa, nami nasema wapigwe tu, ee wapigwe"
 
Hao waamdamanaji hawakupaswa kuharibu mali za walala hii wenzao ni ujinga tu.
 
leo mnapinga ongezeko la viwango vya ushuru. kesho mnalalamika serikali haiwaletei maendeleo jimboni. idiot
 
Back
Top Bottom