KIMBURU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 210
- 189
Katika harakati za kuzima moto uliowashwa jimboni Kongwa na wabunge wa CHADEMA ambao naibu spika huyo aliwafukuza bungeni (Sugu, Msigwa, Wenje etc), Jobu Ndugai amekutana na zomea zomea karibu kila sehemu aliyokwenda kuhutubia. Kwamasikitiko N.Spika huyo alisikika akiwaambia wananchi "Jamani mbona muda wote tulikuwa tukiishi vizuri, iweje leo mkubali kushawishiwa na watu wa kupita?" (sio nukuu rasmi). Ndugai alionekana kuchanganyikiwa kabisa hadi baadhi ya wazee walipokuja kumtuliza na kumwambia ajirekebishe alipokosea ili kurudisha imani kwa wanakongwa. Kuna kijiji kashindwa kabisa kuhutubia baada ya wananchi kumkataa kabisa 100%. For sure Kongwa imebadilika sana tangu wabunge waliofukuzwa bungeni na Ndugai walipokuja hapa na kutangaza kuwa jimbo hili halina mbunge.
My take: Nimefurahishwa sana na jinsi CHADEMA wanavyojua kuyatumia makosa ya CCM.
My take: Nimefurahishwa sana na jinsi CHADEMA wanavyojua kuyatumia makosa ya CCM.