Mh. Spika Ndugai alijiapiza kukomesha tabia ya wabunge hasa wa UKAWA kutoka bungeni

laurent Msembeyu

Senior Member
Oct 5, 2015
121
225
Mh. Mbunge huyo wa Kongwa mwenye matumizi makubwa yanayogharamiwa na bungeki-indirect mfano kuhudumia wake wawili ambao ni ghali sana (mchaga na Mapare)baada ya rais kumaliza kuhutubia hotuba ya kufungua bunge alijiapiza kwambasuala la wabunge kutoka bungeni kwa nia ya kufikisha ujumbe Fulani halitorudiwatena ndani ya utawala wake.


Kwa bahati mbaya sana kiapo chake hicho hakiendani hata kidogo na kasi yautendaji wa kazi wa Mh. Rais wa awamu ya5. Mh. John Pombe Magufuli. Kumbe ilikuwa aape kwamba ndani ya utawala wake mswada utatayarishwa kwa haraka ili kuwezesha bunge kukatazwa wasijipangie malupulupu yao kwani kufanya hivyo ni sawa na machezaji huyo huyo kuwa pia refa maana nilazima atajipa penalty. Kuzuia wabunge kutoka ili kufikisha hisia zao kuna tija gani kwa Mh. Ndugai kutumia nguvu kubwa kuzuia? Maana kwa sheria za sasa ukitoka na posho ya makalio hupati sasa nani anakula hasara?


Pili Mh. Mbunge huyo machachali wa Kongwa ambaye hupiga wenzie na Nkwizu (fimbo ya kigogo yenye nundu mwishoni) wakati wa kampeni za kura za maoni jana alisikika aking`aka kwamba ofisi ya bunge haiwezi kumlipa mtu asiyekuwa mtumishi wa bunge akijibu hoja ya mbunge wa Singida magharibi Mh Kingu ambaye pesa yake ya posho ya makalio ameamua walipwe kamati Fulani aliyoiteuwa ili pesa hizo ziwe mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuendeleza jimbo lake. Pia kung`aka kwake huko Mh. Mbunge huyo wa kongwa nako kunaenda kinyume kabisa na msimamo waRais wa awamu ya 5 Mh. John Pombe Magufuli ambaye anasisitiza kubana matumizi yasiyo ya lazima kama vile malipo ya seating allowance ya mbunge ambae teyari ana stahiki ya kupata mshahara wa kila mwezi na posho ya usumbufu (distabanceallowance) pindi awapo kwenye vikao vya bunge.


Cha kushangaza zaidi Mh. Mbunge huyo wa kupiga wenzie na nkwizu alitetea malipo hayo kwa kudai wabunge wanastahili kukaa hoteli nzuri zenye TV naViyoyozi kwa ajili ya kutafakari kazi ya kesho maana kazi ya mbunge ni ngumu sana kuliko kulima na jembe la mkono.


Falsafa ya Mh. Rais huku, falsafa ya Spika wa bunge la 11 kule.
 

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
Sijaona kosa la Ndughai, ilimradi tu malipo hayo yasiwe makubwa kiasi cha wananchi kuyalalamikia.
 

simanyane

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
2,251
1,500
Hatujawaona mkilalamikia wakuu wa wilaya kwamba wanatumia pesa ya umma na magari bila kufanya kazi
 
Top Bottom