Maisha ya kuwa na shauku ya kutimiza ndoto ni udanganyifu wa ulimwengu na kumuasi Mungu.
Hatupo kutimiza ndoto zetu katika hii Dunia. Hatukujiumba na wala Dunia si mali yetu hata tupange mambo yetu binafsi.
Maisha halisi ni kumtumainia Mungu pekee. Ndoto zako ziwe ni kumpendeza Mungu na kufuata maelekezo yake kama Kitabu chake (BIBLIA) Kinavyoelekeza kuishi. Kitabu hiki chenye maelekezo ya Mungu kinasema" Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa". Hayo yote ikimaanisha chakula, mavazi n.k (Kiufupi ni mahitaji ya mwili).
Maisha ya kufuata ndoto zetu(Wanadamu) si mpango wa Mungu. Ni uasi wa Wanadamu kwa Mungu. Kuishi kwa kutimiza ndoto binafsi ni kumuasi Mungu, kwa sababu inakufanya kufanya lolote hata lililo kinyume na Mapenzi ya Mungu ili kufikia ndoto zako.
Maisha sahihi ni kumjua Mungu. Kumuabudu yeye. Baada ya hapo sasa unamwambia haja zako na unasubiri mapenzi yake yatimizwe na siyo kulazimisha maono yako binafsi yatimie au kufanyika. Huko ni sawa na kumpangia Mungu kazi. What if kama siyo mapenzi ya Mungu kwako kufanya kazi CRDB? . Simaanishi ukae bila kufanya kazi. Namaanisha kumtanguliza Mungu kwanza katika mapito yako. Kisha kumsikiliza Mungu kuhusu mpango wake kuhusu maisha yako.
Ukimfuata Mungu sawa na neno lake, hutakosa namna ya kula wala kuvaa. Maana yeye hufanya njia pasipo na njia. Ni hayo tu ndugu. Kubali kubadilika. Ujanja wa mwanadamu wa Fikra ikiwemo mafundisho mapotofu ya kutimiza ndoto zetu yasikufanye mpofu na kudhani hayo ndiyo mpango wa Mungu katika maisha yako. Huu ni ushauri tu, ushauri hukubaliwa au kukataliwa. Siyo lazima ukubali nilichosema. Ila kweli ya Mungu itabaki paleplae siku zote. Hautobadilika.!