Naandika JamiiForums "LABDA "ndoto yangu itatimia

GREAT INVESTOR

Senior Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
128
Reaction score
299
Salamu na poleni kwa miangaiko ya kutafuta kutimiza ndoto zenu wana Jamiiforums

Naandika hapa nikiamini kuna watu tofauti tofauti, wapo wenye kuweza kusaidia ndoto yangu kutimia, Ila pia wapo wenye uwezo wa kunishauri nikapiga hatua moja mbele na wapo wenye kukatisha tamaa, KARIBUNI WOTE.

Naanza kama hivi, Nilivyokua form two nilianza kupenda kufuatilia masuala ya biashara na uchumi hapa ni baada ya kuanza kua mjanja hapo hatusomi uchumi (form two) ila nikaanza kupenda nikazidisha kufuatilia, nakumbuka tulikua tunaruhusiwa kuangalia taarifa ya habari saa mbili mimi nikawa nabaki( nakua wa mwisho kutoka DH) mpaka taarifa za biashara na uchumi zifike nijue nini kimejiri.

Baada ya muda kupita(form 3) nikajiwekea malengo ;

* Liwalo na liwe, nitakuja kusoma uchumi kwa malengo ya kuja kuwa mchumi" Bank Kuu ya Tanzania , Wizara ya Fedha au Taasisi yoyote."

Katika malengo yangu haya nilipenda sana kuwa mchumi kwenye upande wa kuandaa policy au kuchambua masuala ya kiuchumi au hata kuwa miongoni mwa waandaa budget ya Nchi.

Nilikomaa na ndoto yangu, nikasoma kwa bidii, nikafauli vizuri ngazi zote namshukuru Mungu nikahitimu DEGREE yangu ya kwanza, BACHELOR OF SCIENCE AGRICULTURAL ECONOMICS and AGRIBUSINESS.

Nikafaulu vizuri pia siyo mbaya saana G.P.A ya 3.7,

Kufupisha ninachoandika ndoto yangu ikawa ni ile ile ya kutafuta sehemu ya kufanya kazi za kichumi, Ila kwa bahati mbaya mpaka leo sijabahatika kupata nafasi hii,

Nilibahatika kupata nafasi ya kufanya kazi na kampuni Y ya kilimo kwa mkataba nikamaliza mkataba ila bado ndoto yangu ni ile ile, sijajua lini na siku gani nitatimiza ndoto yangu Ila naamini iko siku itatimia.

KIFUPI NAFANYA HAYA

Bado nafuatilia sana masuala ya kibiashara na Kiuchumi, Kitaifa na Kimataifa nasoma sana vitabu vya uchumi najaribu kua updated sana sana kwenye hii nyanja Pia najaribu sana kutafuta connections.

KWANINI NIMEANDIKA HAPA.

1. Ni kukutia moyo wewe ambaye unandoto yako na hujui ni jinsi gani utafanikisha, USIKATE tamaa endelea kufukuzia ndoto yako, Mwombe Mungu sana sana pia"IKO SIKU"

2. Ni kuomba kwa mtu yeyote wa Serikalini au private sector mwenye kuweza kunishika mkono nikafikia hii ndoto yangu" NA KUSUDIA KUSEMA NAOMBA "SUPPORT" YAKO

3. Nikuombe mwana JF kama unauwezo wa kumshika mtu mkono ukafanikisha yeye kutimiza ndoto yake, Msaidie pengine kesho atakusaidia pia au utalipwa kwa njia nyingine.

4. Narudia, Usikate tamaa, pambana kutimiza ndoto yako, Ipo siku.

NOTE, Masuala ya kujiajiri usiyalete hapa.
 
Nimekushangaa sana mkuu, yaani with your Degree, unatarajia uajiriwe enzi hizi kweli? Mimi nilidhani unasema ukiona utafute elimu ni that area, ili kusudi uanzishe business company yako kumbe unamtafuta kuajiriwa?

Vijana siku hizi mnakwama kabisa, hamsomi alama za nyakati.
 
Nimekushangaa sana mkuu, yaani with your Degree, unatarajia uajiwe enzi hizi kweli? Mm nilidhani unasema ukiona utafute elimu ni that area, ili kusudi uanzishe business company yako kumbe unamtafuta kuajiliwa? Vijana siku hizi mnakwama kabisa, hamsomi alama za nyakati.
Nashukuru.

Naomba niajiri kwenye kampuni yako uliyoanzisha kiongozi.
 
Nimekushangaa sana mkuu, yaani with your Degree, unatarajia uajiwe enzi hizi kweli? Mm nilidhani unasema ukiona utafute elimu ni that area, ili kusudi uanzishe business company yako kumbe unamtafuta kuajiliwa? Vijana siku hizi mnakwama kabisa, hamsomi alama za nyakati.
Mpe mtaji
 
Salamu na poleni kwa miangaiko ya kutafuta kutimiza ndoto zenu wana Jamiiforums

Naandika hapa nikiamini kuna watu tofauti tofauti, wapo wenye kuweza kusaidia ndoto yangu kutimia, Ila pia wapo wenye uwezo wa kunishauri nikapiga hatua moja mbele na wapo wenye kukatisha tamaa, KARIBUNI WOTE.

Naanza kama hivi, Nilivyokua form two nilianza kupenda kufuatilia masuala ya biashara na uchumi hapa ni baada ya kuanza kua mjanja hapo hatusomi uchumi (form two) ila nikaanza kupenda nikazidisha kufuatilia, nakumbuka tulikua tunaruhusiwa kuangalia taarifa ya habari saa mbili mimi nikawa nabaki( nakua wa mwisho kutoka DH) mpaka taarifa za biashara na uchumi zifike nijue nini kimejiri.

Baada ya muda kupita(form 3) nikajiwekea malengo ;

* Liwalo na liwe, nitakuja kusoma uchumi kwa malengo ya kuja kuwa mchumi" Bank Kuu ya Tanzania , Wizara ya Fedha au Taasisi yoyote."

Katika malengo yangu haya nilipenda sana kuwa mchumi kwenye upande wa kuandaa policy au kuchambua masuala ya kiuchumi au hata kuwa miongoni mwa waandaa budget ya Nchi.

Nilikomaa na ndoto yangu, nikasoma kwa bidii, nikafauli vizuri ngazi zote namshukuru Mungu nikahitimu DEGREE yangu ya kwanza, BACHELOR OF SCIENCE AGRICULTURAL ECONOMICS and AGRIBUSINESS.

Nikafaulu vizuri pia siyo mbaya saana G.P.A ya 3.7,

Kufupisha ninachoandika ndoto yangu ikawa ni ile ile ya kutafuta sehemu ya kufanya kazi za kichumi, Ila kwa bahati mbaya mpaka leo sijabahatika kupata nafasi hii,

Nilibahatika kupata nafasi ya kufanya kazi na kampuni Y ya kilimo kwa mkataba nikamaliza mkataba ila bado ndoto yangu ni ile ile, sijajua lini na siku gani nitatimiza ndoto yangu Ila naamini iko siku itatimia.

KIFUPI NAFANYA HAYA

Bado nafuatilia sana masuala ya kibiashara na Kiuchumi, Kitaifa na Kimataifa nasoma sana vitabu vya uchumi najaribu kua updated sana sana kwenye hii nyanja Pia najaribu sana kutafuta connections.

KWANINI NIMEANDIKA HAPA.

1. Ni kukutia moyo wewe ambaye unandoto yako na hujui ni jinsi gani utafanikisha, USIKATE tamaa endelea kufukuzia ndoto yako, Mwombe Mungu sana sana pia"IKO SIKU"

2. Ni kuomba kwa mtu yeyote wa Serikalini au private sector mwenye kuweza kunishika mkono nikafikia hii ndoto yangu" NA KUSUDIA KUSEMA NAOMBA "SUPPORT" YAKO

3. Nikuombe mwana JF kama unauwezo wa kumshika mtu mkono ukafanikisha yeye kutimiza ndoto yake, Msaidie pengine kesho atakusaidia pia au utalipwa kwa njia nyingine.

4. Narudia, Usikate tamaa, pambana kutimiza ndoto yako, Ipo siku.

NOTE, Masuala ya kujiajiri usiyalete hapa.
Ushauri wangu, hapo hapo kwenye hiyo kampuni waliyo kuajiri hakikisha unaitendea haki hiyo nafasi, pia nje ya mshahara wanaokupa jitahidi uwe mtu wa kujitolea sana..
 
Mimi ninategemea kwa Elimu uliyo nayo unishike Mkono Uniajiri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom