Ndoto ya Utekaji na Ujumbe niliopewa

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Nadhani ni wakati sahihi kwa mimi kufunguka kidogo kuhusu ndoto yangu. Hii kitu imenisumbua sana.

Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya October 2018 nilipata ndoto/njozi nilipokuwa nimejipumzisha iliyonionyesha mfanyabiashara mmoja mkubwa sana akiwa anachukuliwa mateka. Kwa kumbukumbu zangu lilikuwa tukio la haraka ila lilikuwa wazi kabisa halikuhitaji tafsiri ya ndoto.

Nilipoamka tu, nikajua bila shaka ni tukio linakuja kutokea. Unajua kuna ndoto unaamka hauna uhakika nayo au hata details zake kama zimepotea ila hii ilikuwa tofauti. Nilianza kujiuliza sana kwa nini nimepewa ndoto ile? Inanibidi niitangaze? Inabidi nikaripoti polisi? Inabidi niiandikie uzi haraka katika Jamii Forums? Inabidi niiombee ili isitokee? Niwasiliane na wafanyabiashara wakubwa kuwaambia wajihadhari? Kwa kweli sikujua la kufanya.

Nilichokuwa nina uhakika nao ni kuwa aliyetekwa katika ndoto ile ni mfanyabiashara mkubwa sana na nikawa najisemea kama ni Tanzania, huyu atakuwa ni mmoja kati ya wafanyabiashara watatu wakubwa.

Nikawa najiuliza nikiandika kitu kama hiki katika mitandao naweza kuishia kukejeliwa, kutukanwa au kupuuziwa kabisa. Nikajua wengine wataniambia natafuta kiki au likes za lazima. Hii ilikuwa inanipa wakati mgumu sana kwa sababu mimi siyo mtu wa namna hiyo. Vilevile nikawa nafikiri, hivi nikipost, vyombo vya usalama hawataniletea usumbufu mkubwa kabla ya tukio au baada ya tukio pale litakapotokea, kunichunguza kama na mimi nahusika kwa namna moja ama nyingine.

Wakati naendelea na mambo mengine nikiendelea kutafakari, siku ya Jumanne, October 2nd 2018, dada yangu akanitumia message akinipa taarifa kuwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili, James Nee mwenye makazi yake Afrika Kusini amepata ajali. Nilishtuka sana kwa sababu wiki kama tatu nyuma nilikuwa nafanya shughuli zangu mida ya mchana kuna sauti ikaniambia nifute nyimbo zote kwenye simu yangu isipokuwa nyimbo za gospel. Haukuwa ujumbe wa kawaida na sijawahi kuupata hapo kabla. Amini usiamini, dakika ile ile nikafuta kama ilivyoniambia, nyimbo nilizoziacha ni za kumtukuza Mungu tu. Wakati huo sikuwa na collection kubwa ya nyimbo za Injili ila nilizokuwa nazo nyingi zilikuwa ni nyimbo 10 za James Nee kutoka kwenye album yake. Kifo chake kilinigusa sana na kiliwashtua na kuwagusa wengi sana. James Nee alikuwa one of a kind. Toka nilipomsikia kwa mara ya kwanza, muziki wake umekuwa ni muhimu sana katika maisha yangu ya kiroho. Nilipopata taarifa ya kifo chake nikakumbuka mara moja ujumbe niliopata wiki chache zilizopita.

Kuna mtu alileta uzi hapa kuhusu kifo hiki na niliyasema haya kwenye uzi ule.

Msanii na mwimbaji injili wa Prophet Bushiri, James Nee afariki kwa ajali ya gari! - JamiiForums

Takribani wiki moja baada ya ujumbe ule ndiyo nikapata ndoto ya kutekwa kwa mfanyabiashara mkubwa.

Siku ya Alhamisi October 11th 2018, nilipopata taarifa za kutekwa kwa Mo kwa kweli mwili ulisisimka. Kama ningekuwa na maswali yoyote kuhusu ndoto niliyoipata wiki kadhaa kabla, ile taarifa ilikuwa imeyajibu maswali yale. Swali lililokuwa limebaki ni, kwa nini nimepewa ujumbe huu? Nini natakiwa kufanya? Hili bado nilikuwa sina jibu.

Mimi ni mtu ninayejaribu kusoma Biblia mara kwa mara na kutafakari Neno la Mungu. Nikakumbuka katika Biblia watu kama kina Ibrahimu na Yakobo waliposikia sauti ya Mungu walimjengea Madhabahu sehemu ile waliyokutana naye. Na mimi nikasema nitamjengea Mungu madhabahu hapa nyumbani. Nikacheki online wengine wanasemaje kuhusu kujenga madhabahu, kuna video moja ya TD Jakes ilinisaidia sana. Nikaamua kutenga chumba kimoja kwa ajili hiyo. Nikaweka vitu vichache vinavyonihusu pamoja na fungu la kumi kwa kazi moja niliyokuwa nimeifanya hivi karibuni.

Kuna uzi niliuanzisha kama wiki imepita nikagusia hili la madhabahu nikaahidi nitarudi na ushuhuda.

https://www.jamiiforums.com/threads...-madhabahu-mahali-hapo.1495358/#post-28800620

Baada ya hapo, nikaenda katika maombi. Kwanza nikafanya toba halafu nikawaombea wazazi na ndugu zangu hadi na mababu na mabibi na vizazi vyangu vyote vilivyopita. Nikaendelea na maombi nikimkumbusha Mungu baraka na vipawa vingi alivyonijaalia.

Nikaenda kusoma Biblia Kitabu cha Isaya 48. Sikujua kwa nini nilienda kusoma chapter ile na wala sikuwa najua itazungumzia nini. Nilipoanza kusoma tu nikajua kuna uwepo wa Mungu mahali pale.

Isaya 48:3, 5-8 - Neno hili linasema Bwana amenionyesha mambo mapya kabisa, yale yaliyofichwa…..

Inawezekana hii chapter (Isaya 48) ni kwa ajili ya Mo Dewji kuisoma. Niliona sehemu alisoma theolojia na nimewahi kumsikia akisalimia watu ‘Bwana Yesu asifiwe’ kwa hiyo sidhani kama atakuwa na tatizo na kusoma Biblia. Kama kuna mtu anaweza kumtumia hii chapter nitashukuru.

Kwa siku tatu zilizofuata niliendelea kutafakari nini natakiwa kufanya. Siku ya Jumanne October 15th, 2018 asubuhi wakati naendelea na sala mbele ya Madhabahu nikamuuliza Mungu ana mipango gani na mimi? Nikamuomba asikae kimya aseme na mimi nipo tayari kusikia na kutenda atakaloniambia. Baada ya hapo nikatoka nikawasha Radio Upendo FM (naisikilizaga sana hii radio), ghafla nikakutana na mafundisho na mahubiri ya Muinjilisti mmoja (jina sikulifahamu) akawa anaongelea hicho hicho nilichokuwa nimetoka kuomba dakika chache tu zilizopita. Katika kusikiliza mahubiri yake alikuwa anasisitiza sana kuhusu kitabu cha HABAKKUK. Yaani nikisikia mistari aliyokuwa ananukuhu ilikuwa ni kama Mungu ananijibu directly. Ilipofika saa 7 mchana, Upendo FM wakakatisha maombi wakaweka taarifa ya habari. Nikawatumia message wanitumie jina na contact za yule muinjilisti ila hawakunijibu. Nikatoka pale nikaenda kusoma kitabu chote cha Habakkuk - kina sura tatu tu (unaweza kusoma na wewe ujue ujumbe niliopata kwa sababu ni wa muhimu sana)!

Message niliyowatumia Upendo Radio ni hii hapa.

1429CC17-7559-4B2D-9B9A-8EEDCA6E3243.jpeg

Habakkuk 2:2-3, Mungu anamjibu Habakkuk: Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; Ijapokawia ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Mungu anaendelea kumwambia Habakkuk kwamba wale wenye kuonea, kuua na kuteka watu kama samaki mwisho wao waja.

Mwisho katika sura ya 3, Nabii Habakkuk anafanya sala. Anatabiri njaa na ukame unakuja. Anatabiri Mungu akija kufanya kisasi kwa watesi wote na wauaji na wanyanganyi. Lakini anamalizia kwa kusema (Habakkuk 3:18-19), atamfurahia Bwana na kumshangilia Mungu wa wokovu wake naye atamuendesha hadi mahali pake palipoinuka!!

Usiku wa kuamkia October 20, 2018, around 12:30 am nilienda tena katika maombi. Nikasoma tena Habakkuk chapter zote 1-3, then nikasoma kitabu cha Nahum, chapter zote 3. Ujumbe niliopata ni kuwa Bwana anakuja kuwateketeza wale wanaowapa watu wake mateso. Anakuja kuwaangamiza wale wanaochukua watu wake mateka, wanaofanya udhalimu, nk. Bada ya hapo nikamuomba Mungu kama anaweza kuondoa udhalimu na mateso hayo bila kuwaongezea watu wake mateso zaidi.

Baadaye wakati nafanya mambo mengine, around 3 am, nikakumbuka passage moja kitabu cha Matendo ya Mitume inayosema katika siku za mwisho, watu watatabiri na wataona maono…’

Muda haukupita, nikakutana na uzi mmoja humu wenye title ya 'Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono nilioona)’. Na yeye anaongelea ndoto aliyoipata October mwanzoni ambayo anaona kama imetokea kweli ya kifo cha Mwandishi Isaac Gamba. Nilipoiona nikajua labda finally nimepata mtu wa kuzungumza naye kuhusu hii issue. Nilimtumia ujumbe kumuomba tuongee (cheki uzi wake).
Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono niliyoona) - JamiiForums

Ilipofika kama saa 10 alfajiri, taarifa ndiyo zikatoka za kupatikana kwa Mo.

Cha muhimu kwangu, nimetimiza nilichoambiwa katika Habakkuk 2:2-3, niliambiwa niiandike wazi ndoto hii na kwa mtiririko ili yeyote atakayeisoma aielewe.

Bado sijui Mungu ana makusudi gani na sijui kama kuandika ujumbe huu nimechelewa, nimewahi au nimefanya kwa wakati sahihi. Ila naona kuna mambo mengine makubwa sana na ya ajabu anaenda kunionyesha (siyo maneno yangu ni ahadi yake mwenyewe).

Sura nyingine nilizosoma na ambazo zimenipa ujumbe muhimu ni:
Isaya 41
Waefeso 6
 
Ndoto zako zinachelewa mkuu,ukiota andika muda huohuo tujue namna ya kukabiliana na tatizo maana ni uhai wa mtu,ila mengine unaeza acha tu,mfano ukiota kuhusu mawe ama jiwe hivi unaweza kausha tu.
 
Inabidi kufuata maelekezo mkuu. Sikuwa najua cha kufanya na kwa kweli sikuwa na mtu wa kunishauri ndiyo maana nikajaribu kumtafuta yule Mchungaji niliyemsikia kwenye radio. Nilipomkosa nikasema kama ni ujumbe wa Mungu ni yeye mwenyewe ataniambia nifanye nini.
 
Kodi zetu yananunua wabunge na madiwani kulipia hiyo hasara wanamteka moo ili warudishe kodi za watu yalitaka trillion mbili familia ya moo ikasoma mchezo wakakimbilia kwenye media uwezo wetu ni bilion moja watekaji wakazidiwa akili hawana namna zaidi ya kutema bungo
 
View attachment 906087

Habakkuk 2:2-3, Mungu anamjibu Habakkuk: Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; Ijapokawia ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Mungu anaendelea kumwambia Habakkuk kwamba wale wenye kuonea, kuua na kuteka watu kama samaki mwisho wao waja.

Mwisho katika sura ya 3, Nabii Habakkuk anafanya sala. Anatabiri njaa na ukame unakuja. Anatabiri Mungu akija kufanya kisasi kwa watesi wote na wauaji na wanyanganyi. Lakini anamalizia kwa kusema (Habakkuk 3:18-19), atamfurahia Bwana na kumshangilia Mungu wa wokovu wake naye atamuendesha hadi mahali pake palipoinuka!!

Usiku wa kuamkia October 20, 2018, around 12:30 am nilienda tena katika maombi. Nikasoma tena Habakkuk chapter zote 1-3, then nikasoma kitabu cha Nahum, chapter zote 3. Ujumbe niliopata ni kuwa Bwana anakuja kuwateketeza wale wanaowapa watu wake mateso. Anakuja kuwaangamiza wale wanaochukua watu wake mateka, wanaofanya udhalimu, nk. Bada ya hapo nikamuomba Mungu kama anaweza kuondoa udhalimu na mateso hayo bila kuwaongezea watu wake mateso zaidi.

Baadaye wakati nafanya mambo mengine, around 3 am, nikakumbuka passage moja kitabu cha Matendo ya Mitume inayosema katika siku za mwisho, watu watatabiri na wataona maono…’

Muda haukupita, nikakutana na uzi mmoja humu wenye title ya 'Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono nilioona)’. Na yeye anaongelea ndoto aliyoipata October mwanzoni ambayo anaona kama imetokea kweli ya kifo cha Mwandishi Isaac Gamba. Nilipoiona nikajua labda finally nimepata mtu wa kuzungumza naye kuhusu hii issue. Nilimtumia ujumbe kumuomba tuongee (cheki uzi wake).
Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono niliyoona) - JamiiForums

Ilipofika kama saa 10 alfajiri, taarifa ndiyo zikatoka za kupatikana kwa Mo.

Cha muhimu kwangu, nimetimiza nilichoambiwa katika Habakkuk 2:2-3, niliambiwa niiandike wazi ndoto hii na kwa mtiririko ili yeyote atakayeisoma aielewe.

Bado sijui Mungu ana makusudi gani na sijui kama kuandika ujumbe huu nimechelewa, nimewahi au nimefanya kwa wakati sahihi. Ila naona kuna mambo mengine makubwa sana na ya ajabu anaenda kunionyesha (siyo maneno yangu ni ahadi yake mwenyewe).

Sura nyingine nilizosoma na ambazo zimenipa ujumbe muhimu ni:
Isaya 41
Waefeso 6
Hivi tukio likitokea halafu wewe ukaliota hiyo ni ndoto au kumbukumbu tu ?
 
Nililiota wiki ya kwanza ya October na nimehangaika nayo sana hii ndoto, nilikuwa nina uhakika inakuja kutokea.

Kama swali lako ni kutaka tu kujua, nadhani unaweza kuota baada ya tukio labda kufunuliwa zaidi kitu kilichofichwa. Mimi mwenyewe nilitegemea either kwenye ndoto au hata nikiwa macho baada ya tukio la kutekwa Mo ningepata ujumbe fulani ndiyo maana mjadala mzima toka umeanza sikuwa nacomment chochote.
 
Nililiota wiki ya kwanza ya October na nimehangaika nayo sana hii ndoto, nilikuwa nina uhakika inakuja kutokea.
Hii ni ngumu kuaminika. Kwanini usubiri tukio litokee ndiyo uje kutuambia ndoto yako ?
 
Kama umesoma vizuri nimeelezea sababu. Nitafaidika nini na kutunga kitu kama hiki halafu niandike maelezo yote hayo yawe ya kutunga kweli?

Kuna uwezekano ningepost kabla ya tukio ningelala central na kina Manara. Ila kama ujumbe ungenitaka nifanye hivyo, ningefanya ninachoambiwa bila woga. Ila labda Mungu aliniambia hivyo niliposoma Isaya 41 labda kwa woga wangu nikajifanya kutoona, najaribu kuwa mkweli.
 
Sijasema umetunga nimesema ni vigumu kukuamini

Ninachoweza kukwambia matukio ya mwezi huu na mimi yamenishangaza. Ila soma Habakuki 1:5, hata Mungu hategemei wengine kuniamini ndiyo maana hata uzi ule wa kuhusu madhabahu niligusia kwamba kuna kitu nitakuja kupost kuna watu hawataamini. Nilikuwa bado nawaza kama nipost au nisubiri.
 
Kodi zetu yananunua wabunge na madiwani kulipia hiyo hasara wanamteka moo ili warudishe kodi za watu yalitaka trillion mbili familia ya moo ikasoma mchezo wakakimbilia kwenye media uwezo wetu ni bilion moja watekaji wakazidiwa akili hawana namna zaidi ya kutema bungo
Utatusaidia mwnye upelelezi ww
 
Nadhani ni wakati sahihi kwa mimi kufunguka kidogo kuhusu ndoto yangu. Hii kitu imenisumbua sana.

Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya October 2018 nilipata ndoto/njozi nilipokuwa nimejipumzisha iliyonionyesha mfanyabiashara mmoja mkubwa sana akiwa anachukuliwa mateka. Kwa kumbukumbu zangu lilikuwa tukio la haraka ila lilikuwa wazi kabisa halikuhitaji tafsiri ya ndoto.

Nilipoamka tu, nikajua bila shaka ni tukio linakuja kutokea. Unajua kuna ndoto unaamka hauna uhakika nayo au hata details zake kama zimepotea ila hii ilikuwa tofauti. Nilianza kujiuliza sana kwa nini nimepewa ndoto ile? Inanibidi niitangaze? Inabidi nikaripoti polisi? Inabidi niiandikie uzi haraka katika Jamii Forums? Inabidi niiombee ili isitokee? Niwasiliane na wafanyabiashara wakubwa kuwaambia wajihadhari? Kwa kweli sikujua la kufanya.

Nilichokuwa nina uhakika nao ni kuwa aliyetekwa katika ndoto ile ni mfanyabiashara mkubwa sana na nikawa najisemea kama ni Tanzania, huyu atakuwa ni mmoja kati ya wafanyabiashara watatu wakubwa.

Nikawa najiuliza nikiandika kitu kama hiki katika mitandao naweza kuishia kukejeliwa, kutukanwa au kupuuziwa kabisa. Nikajua wengine wataniambia natafuta kiki au likes za lazima. Hii ilikuwa inanipa wakati mgumu sana kwa sababu mimi siyo mtu wa namna hiyo. Vilevile nikawa nafikiri, hivi nikipost, vyombo vya usalama hawataniletea usumbufu mkubwa kabla ya tukio au baada ya tukio pale litakapotokea, kunichunguza kama na mimi nahusika kwa namna moja ama nyingine.

Wakati naendelea na mambo mengine nikiendelea kutafakari, siku ya Jumanne, October 2nd 2018, dada yangu akanitumia message akinipa taarifa kuwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili, James Nee mwenye makazi yake Afrika Kusini amepata ajali. Nilishtuka sana kwa sababu wiki kama tatu nyuma nilikuwa nafanya shughuli zangu mida ya mchana kuna sauti ikaniambia nifute nyimbo zote kwenye simu yangu isipokuwa nyimbo za gospel. Haukuwa ujumbe wa kawaida na sijawahi kuupata hapo kabla. Amini usiamini, dakika ile ile nikafuta kama ilivyoniambia, nyimbo nilizoziacha ni za kumtukuza Mungu tu. Wakati huo sikuwa na collection kubwa ya nyimbo za Injili ila nilizokuwa nazo nyingi zilikuwa ni nyimbo 10 za James Nee kutoka kwenye album yake. Kifo chake kilinigusa sana na kiliwashtua na kuwagusa wengi sana. James Nee alikuwa one of a kind. Toka nilipomsikia kwa mara ya kwanza, muziki wake umekuwa ni muhimu sana katika maisha yangu ya kiroho. Nilipopata taarifa ya kifo chake nikakumbuka mara moja ujumbe niliopata wiki chache zilizopita.

Kuna mtu alileta uzi hapa kuhusu kifo hiki na niliyasema haya kwenye uzi ule.

Msanii na mwimbaji injili wa Prophet Bushiri, James Nee afariki kwa ajali ya gari! - JamiiForums

Takribani wiki moja baada ya ujumbe ule ndiyo nikapata ndoto ya kutekwa kwa mfanyabiashara mkubwa.

Siku ya Alhamisi October 11th 2018, nilipopata taarifa za kutekwa kwa Mo kwa kweli mwili ulisisimka. Kama ningekuwa na maswali yoyote kuhusu ndoto niliyoipata wiki kadhaa kabla, ile taarifa ilikuwa imeyajibu maswali yale. Swali lililokuwa limebaki ni, kwa nini nimepewa ujumbe huu? Nini natakiwa kufanya? Hili bado nilikuwa sina jibu.

Mimi ni mtu ninayejaribu kusoma Biblia mara kwa mara na kutafakari Neno la Mungu. Nikakumbuka katika Biblia watu kama kina Ibrahimu na Yakobo waliposikia sauti ya Mungu walimjengea Madhabahu sehemu ile waliyokutana naye. Na mimi nikasema nitamjengea Mungu madhabahu hapa nyumbani. Nikacheki online wengine wanasemaje kuhusu kujenga madhabahu, kuna video moja ya TD Jakes ilinisaidia sana. Nikaamua kutenga chumba kimoja kwa ajili hiyo. Nikaweka vitu vichache vinavyonihusu pamoja na fungu la kumi kwa kazi moja niliyokuwa nimeifanya hivi karibuni.

Kuna uzi niliuanzisha kama wiki imepita nikagusia hili la madhabahu nikaahidi nitarudi na ushuhuda.

https://www.jamiiforums.com/threads...-madhabahu-mahali-hapo.1495358/#post-28800620

Baada ya hapo, nikaenda katika maombi. Kwanza nikafanya toba halafu nikawaombea wazazi na ndugu zangu hadi na mababu na mabibi na vizazi vyangu vyote vilivyopita. Nikaendelea na maombi nikimkumbusha Mungu baraka na vipawa vingi alivyonijaalia.

Nikaenda kusoma Biblia Kitabu cha Isaya 48. Sikujua kwa nini nilienda kusoma chapter ile na wala sikuwa najua itazungumzia nini. Nilipoanza kusoma tu nikajua kuna uwepo wa Mungu mahali pale.

Isaya 48:3, 5-8 - Neno hili linasema Bwana amenionyesha mambo mapya kabisa, yale yaliyofichwa…..

Inawezekana hii chapter (Isaya 48) ni kwa ajili ya Mo Dewji kuisoma. Niliona sehemu alisoma theolojia na nimewahi kumsikia akisalimia watu ‘Bwana Yesu asifiwe’ kwa hiyo sidhani kama atakuwa na tatizo na kusoma Biblia. Kama kuna mtu anaweza kumtumia hii chapter nitashukuru.

Kwa siku tatu zilizofuata niliendelea kutafakari nini natakiwa kufanya. Siku ya Jumanne October 15th, 2018 asubuhi wakati naendelea na sala mbele ya Madhabahu nikamuuliza Mungu ana mipango gani na mimi? Nikamuomba asikae kimya aseme na mimi nipo tayari kusikia na kutenda atakaloniambia. Baada ya hapo nikatoka nikawasha Radio Upendo FM (naisikilizaga sana hii radio), ghafla nikakutana na mafundisho na mahubiri ya Muinjilisti mmoja (jina sikulifahamu) akawa anaongelea hicho hicho nilichokuwa nimetoka kuomba dakika chache tu zilizopita. Katika kusikiliza mahubiri yake alikuwa anasisitiza sana kuhusu kitabu cha HABAKKUK. Yaani nikisikia mistari aliyokuwa ananukuhu ilikuwa ni kama Mungu ananijibu directly. Ilipofika saa 7 mchana, Upendo FM wakakatisha maombi wakaweka taarifa ya habari. Nikawatumia message wanitumie jina na contact za yule muinjilisti ila hawakunijibu. Nikatoka pale nikaenda kusoma kitabu chote cha Habakkuk - kina sura tatu tu (unaweza kusoma na wewe ujue ujumbe niliopata kwa sababu ni wa muhimu sana)!

Message niliyowatumia Upendo Radio ni hii hapa.

View attachment 906087

Habakkuk 2:2-3, Mungu anamjibu Habakkuk: Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; Ijapokawia ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Mungu anaendelea kumwambia Habakkuk kwamba wale wenye kuonea, kuua na kuteka watu kama samaki mwisho wao waja.

Mwisho katika sura ya 3, Nabii Habakkuk anafanya sala. Anatabiri njaa na ukame unakuja. Anatabiri Mungu akija kufanya kisasi kwa watesi wote na wauaji na wanyanganyi. Lakini anamalizia kwa kusema (Habakkuk 3:18-19), atamfurahia Bwana na kumshangilia Mungu wa wokovu wake naye atamuendesha hadi mahali pake palipoinuka!!

Usiku wa kuamkia October 20, 2018, around 12:30 am nilienda tena katika maombi. Nikasoma tena Habakkuk chapter zote 1-3, then nikasoma kitabu cha Nahum, chapter zote 3. Ujumbe niliopata ni kuwa Bwana anakuja kuwateketeza wale wanaowapa watu wake mateso. Anakuja kuwaangamiza wale wanaochukua watu wake mateka, wanaofanya udhalimu, nk. Bada ya hapo nikamuomba Mungu kama anaweza kuondoa udhalimu na mateso hayo bila kuwaongezea watu wake mateso zaidi.

Baadaye wakati nafanya mambo mengine, around 3 am, nikakumbuka passage moja kitabu cha Matendo ya Mitume inayosema katika siku za mwisho, watu watatabiri na wataona maono…’

Muda haukupita, nikakutana na uzi mmoja humu wenye title ya 'Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono nilioona)’. Na yeye anaongelea ndoto aliyoipata October mwanzoni ambayo anaona kama imetokea kweli ya kifo cha Mwandishi Isaac Gamba. Nilipoiona nikajua labda finally nimepata mtu wa kuzungumza naye kuhusu hii issue. Nilimtumia ujumbe kumuomba tuongee (cheki uzi wake).
Nimeshtuka ila nimerejea katika ndoto (Maono niliyoona) - JamiiForums

Ilipofika kama saa 10 alfajiri, taarifa ndiyo zikatoka za kupatikana kwa Mo.

Cha muhimu kwangu, nimetimiza nilichoambiwa katika Habakkuk 2:2-3, niliambiwa niiandike wazi ndoto hii na kwa mtiririko ili yeyote atakayeisoma aielewe.

Bado sijui Mungu ana makusudi gani na sijui kama kuandika ujumbe huu nimechelewa, nimewahi au nimefanya kwa wakati sahihi. Ila naona kuna mambo mengine makubwa sana na ya ajabu anaenda kunionyesha (siyo maneno yangu ni ahadi yake mwenyewe).

Sura nyingine nilizosoma na ambazo zimenipa ujumbe muhimu ni:
Isaya 41
Waefeso 6
Mkuu Mungu anasema na sisi kupitia ndoto kwa hiyo unapoonyeshwa kitu katika ndoto unapswa ku take action na hasa kuombea ili jambo hilo lisitokee kama ni baya na kama ni zuri unaomba ili litokee kwa hiyo kama ungechukua hatua ukaomba tukio la Mo huenda lingeepushwa na Mungu husema na kila mtu kwa njia tofautitofauti na huangalia nani aseme naye nini ili achukue hatua,so kwa kutochukua hatua kwako unapaswa kuomba toba kwamba hukuomba mpaka jambo hilo likatokea na pili umshukuru Mungu kwa kuepusha mabaya kwa Mo na huenda waliomba wengine baada ya kutekwa ndo Mungu akaingilia kati kunusuru. Kwa ufafanuzi zaidi juu ya ndoto nunua kitabu cha Mwalimu Mwakasege pale Luther house posta mpya kama unaishi Dar kama mkoani tafuta namna utakipata kinaeleza vizuri kabisa juu ya ndoto na hatua za kuchukua,ulimwengu wa roho ni dhahiri na mambo yote yanaanzia huko kabla hayajaja kwenye ulimwengu wa mwili.
 
Sijasema umetunga nimesema ni vigumu kukuamini

Nimeanza kuyaandika haya maelezo October 15. Leo nimefanya editing kidogo tu. Usishangae hiyo title, nilikuwa najua atapatikana salama.

20181021_163227.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom