Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,635
- 6,535
- Thread starter
- #21
Mkuu Mungu anasema na sisi kupitia ndoto kwa hiyo unapoonyeshwa kitu katika ndoto unapswa ku take action na hasa kuombea ili jambo hilo lisitokee kama ni baya na kama ni zuri unaomba ili litokee kwa hiyo kama ungechukua hatua ukaomba tukio la Mo huenda lingeepushwa na Mungu husema na kila mtu kwa njia tofautitofauti na huangalia nani aseme naye nini ili achukue hatua,so kwa kutochukua hatua kwako unapaswa kuomba toba kwamba hukuomba mpaka jambo hilo likatokea na pili umshukuru Mungu kwa kuepusha mabaya kwa Mo na huenda waliomba wengine baada ya kutekwa ndo Mungu akaingilia kati kunusuru. Kwa ufafanuzi zaidi juu ya ndoto nunua kitabu cha Mwalimu Mwakasege pale Luther house posta mpya kama unaishi Dar kama mkoani tafuta namna utakipata kinaeleza vizuri kabisa juu ya ndoto na hatua za kuchukua,ulimwengu wa roho ni dhahiri na mambo yote yanaanzia huko kabla hayajaja kwenye ulimwengu wa mwili.
Asante sana. Nitafanya toba leo. Mwezi huu umenionyesha mengi. Hauwezi amini, September 30 nilienda kwenye semina ya Mwalimu Mwakasege, na hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria semina zake nadhani ndani ya siku chache ndiyo hiyo ndoto ilitokea. Bahati mbaya sikuweka rekodi ilikiwa siku gani exactly nilipata ndoto.
Wakati natafuta majibu ya hii ndoto nilimsikiliza Mwalimu Mwakasege kwenye youtube.