Ndoto ya leo imenifikirisha sana

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
10,766
22,149
Habari wakuu,

Usiku wa kuamkia leo nimeota kua napanbana na watu wenye nguvu za giza. Zamani kidogo imani nilikua nayo kiasi yani ilikua nikiota ndoto za namna hii basi huwa nawashinda vikali hao mahasimu wangu, na wala sikua naona kama kuna shida juu ya hizo ndoto.

Lakini hii ya leo iko tofauti na imeenda mbali zaidi, kama nlivosema awali nimeota napambana na hao viumbe lakini ajabu ni kua wapinzani wangu walinizidi nguvu lakini pia hawakutaka kunidhuru ni kama walitaka tu kuonesha wao ni watabe.

Basi baada ya hapo kuna mzee ambae nae alikua hasimu wangu akaaniita tukae mahali na mimi nikshauri tukakae wapi na ajabu nilikua na shauku ya kuongea nae, huyo mzee alikua na ndevu nyingi na mkononi kashika bible na wakati huo hata mimi nimeshika bible ila yake ni zile kubwa wakati yangu ni kale kadogo kabisa.

Mzee akaniambia kua imani yangu ni haba mno naonaje nikiungana nae, mi nikasema asubiri nikafikilie ila akilini mwangu eti nikawa nawaza kua nikitoka hapa sirudi tena kumpa jibu lake. Tuliongea vingi ila ndo hivo bahati mbaya nimesahau vingi nakumbuka hicho cha imani ambacho ni kweli saivi sio mtu ninaesali.

Baada ya hapo nikastuka, sijui ilikua saa ngapi ila nkambonji tena nikawa naota maluweluwe yasiyokumbukika.

Hivi ndoto ya namna hiyo ina maana kama hiyo tu au kuna ujumbe uliojificha??
 
Ndoto hizi!!!!

Juzi nimemuota dada fulani niliyekuwa nafanya nae kazi kituo kimoja kabla hajahama. Sikumbuki tulikuwa tunaelekea wapi, lkn ninachokumbuka ni kuwa tulishikana mikono (hata sijui ilikuaje hadi ikatokea hivi.......ni dada fulani ninayeheshimiana nae sana). Ajabu siku ya pili asubuhi tu kanipigia kunisalimia na hata haikuwa kawaida yake. Nilishangaa sana kwakweli
 
Acha kabisa mkuu, ndoto huenda zinakuaga na maana ila kuzitafsiri ndo kipengele
 
Yesu Anakupenda. Mtii na umfuate

Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
 
Ndoto hizi!!!!

Juzi nimemuota dada fulani niliyekuwa nafanya nae kazi kituo kimoja kabla hajahama. Sikumbuki tulikuwa tunaelekea wapi, lkn ninachokumbuka ni kuwa tulishikana mikono (hata sijui ilikuaje hadi ikatokea hivi.......ni dada fulani ninayeheshimiana nae sana). Ajabu siku ya pili asubuhi tu kanipigia kunisalimia na hata haikuwa kawaida yake. Nilishangaa sana kwakweli
Bwana kakuletea mke mwema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom