FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,867
- 5,064
Ingawa mimi si muamini sana wa ndoto niotazo,nikiamini kuwa ni mambo ya kawaida tu ila juzi juzi hapa kuna jambo limeniacha na maswali.Niliota ndoto nimekutana na Nyoka wa kijani uso kwa uso,wakati tunaangaliana na nikiwa nimepoteza matumaini ya kumuepuka mara nikagundua yule Nyoka alikuwa amekatika na alikuwa kwenye dakika zake za mwisho za uhai.Palepale nami nikashtuka usingzini.
Siiku chache baadae nikiwa site mchana baada ya kazi nikaamua nijipumzishe chini ya mti,nikiwa kifua wazi na head phone masikioni huku nikiwa na hali ya kusinzia, mara kwa pembeni naona kijani inacheza cheza,kugeuka ni jamaa yupo spidi ile mbaya anakuja,nilichokifanya hata ukunipa milioni tano nirudie siwezi,niliweza kuruka kiubavu na kuangukia upande wa pili huku simu ikining"ina na kuangukia upande mwingine,jamaa kuona vile naye akasita na kujichomeka kwenye mawe yaliyokuwa pale pemben.Huku niikiwa na taharuki nimesimama pembeni mara akawa anachomoza kichwa ananiangalia kisha anarudi,Mimi si shabiki sana wa kuua Nyoka,na hata sikumshtua jamaa yangu tuliyekuwa naye pale site maana najua lake ni moja tu,ni kumuua.
Basi akawa anachomoza tunaangaliana kisha anarudi,hatimaye aliondoka sikumuona tena,ila Nyoka ni Nyoka nikubali nimehamaki kwa muda kabla kichwa kubwa sawa.Rangi na muonekano ni vile vile niliyemuona ndotoni.Hili limenishangaza kiukweli.