Ndoto hizi zimenichosha

Masalia Mpya

Member
Mar 24, 2023
53
63
Habari zenu kwa ujumla

Nimekuwa nikiota ndoto zinazofanana fanana.

Iko hivi mimi naishi Dodoma, ila ni mwenyeji wa Lindi. Nimezaliwa huko na kusoma huko mpaka secondary. Chuo nikatoka kwenda mikoa mimgine. Kuanzia hapo nikawa narudi Lindi kama mgeni. Miaka 5 nyuma tulihamisha makazi na kuhamia Mtwara, yaani familia nzima walihama kwa hiyo Lindi tunakwenda kama wageni.

Sasa hivi nina familia yangu huku Dodoma naendelea na maisha yangu, hata nikienda kwetu Mtwara pia naenda kama mgeni siku chache naondoka.

Ndoto zinazonisumbua ni hizi, yaani kwa week mara 2 au 3 naota niko ambako tulishahama, maisha yanaendelea hapo Lindi. Kama ni misiba/ sherehe/ maisha ya familia yetu/ mtaani naota niko Lindi niko na majirani wa Lindi, ndugu walioko Lindi yaani kama vile hatujahama.

Sijawahi kuota niko Mtwara tuliko hamia, hata nikiota wazazi wangu au ndugu zangu naota tuko nyumbani Lindi.

Nashindwa kuelewa, mbona sioti nikiwa Dodoma au Mtwara? Mbona huku nina majirani na hata ndugu wengine Dodoma na Mtwara ila nawaota walioko Lindi? Kwa kweli zimenichosha.

Naombeni ushauri
 
NAFSI Yako imefungwa huko, Kwa ufupi Kwa kuwa umefungiwa huko,

Inahitaji msaada Ili utoke kifungoni ndipo uhame Rasmi.
 
Kuna kitu kilitokea huko kikakuathiri sasa bado huja ki solve ndo maana unaota sana ndoto ukiwa huko
 
Nafsi inakumbuka kwao ilipo zaliwa na kukulia hakuna jipya hapo zaidi, Baada ya muda nafsi itazowea makaazi mepya na kutulia.
 
mi tangu 2014 nimeondoka mkoani na sijawahi kurudi, ila mpaka leo ndoto hizo zinanijia hapo hakuna cha nafsi kuzoea wala kusahau kuna maana yake kiroho
 
Kuna kitu kilikuvutia sna huko lindi, ndio maana akili yako ina kumbukumbu nzuri za lindi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom