...jamani naomba nisaidieni, je kuna ndoa kweli hapa iwapo................
...ila sidhani kama kuna sehemu yoyote ambayo nimesema huo ni utaratibu wao waliojiwekea wenyewe..
sijui ila nafikiri ingekuwa ni utaratibu wao sidhani kama angekuwa analalamika na kutaka ushauri kwa watu nje ya familia.
inawezekana ukweli akaujua yeye mwenyewe
...ila mimi nimewakilisha kile nilichokiona kwa macho- face value of the story
Nini mtazamo wako katika ndoa za aina hii?
Usawa upi bibie mnaolilia??Usawa kwa wanawake Afrika bado sana.....
Usawa upi bibie mnaolilia??
Kama huamini dini basi nakubaliana na wewe.........kuran tukufu na Biblia vinasema wazi wazi....mwanamke atakuwa chini ya mwanaume....
......hizi gender gender zenu nyie..haya..!!
Salamu ndugu zanguni.... jamani naomba nisaidieni, je kuna ndoa kweli hapa iwapo................
1. Pesa za mume hazieleweki zinapokwenda na ukiuliza ni ugomvi ila za mke anataka ajue ametumiaje na anataka mshahara ukitoka tu basi akabidhiwe na yeye ndie awe anayepanga matumizi. Na mke haruhusiwa kununua hata handkerchief ataambiwa yuko extravagant ila mume anauwezo wa kutumia laki tano au sita within a week ikaisha na asiulizwe matumizi.
2. Mke hatakiwi kusaidia ndugu zake na akiomba pesa kwa ajili ya ndugu zake (mke) basi mume hukasirika hadi mke anajuta...
3. Mume siku zote yuko negative about chochote anachokifanya mkewe ingawaje pesa zikipatikana yeye ndie wa kwanza kuzidai
4. Kila siku mume anatafuta makosa kwa mkewe hata kama ni kwenda na kufukua ya nyuma kabla hawajaoana
5. Mume anapenda aabudiwa hata na wakwe zake. kwake yeye wakwe zake si kama wazazi bali watumwa ambao wanastahili kumnyenyekea yeye.
Kwa upande wangu mimi nahisi kama huyu mume anamtumia tu huyu mdada na hana mapenzi ya kweli nae hivyo si ajabu akamwaga huko mbeleni mambo yake yakishakuwa mazuri....
Nini mtazamo wako katika ndoa za aina hii?
Tunakubaliana na hayo kuwa tena tumetoka kwenye mbavu zenu. Ila sasa hio isiwe ndo chanzo cha kunyanyasika kwa mwanamke! Laa hasha, na ndio kikaletwa kitu usawa kwa wote. upo hapo! Nyongeza kwa hao wanawake wanaotaka kuwa juu na kuwatawala wanaume nadhani ni pungwani kidogo. Maana nadhani binadamu hawezi kutawalia na binadamu mwenzie zaidi ya Mungu tuu.
Ndoa zenye utata.............. laiti kama kusingekuwa na mambo ya kupelekana kwa kasisi sijui, maumivu ndani ya ndoa wala yasingekuwepo nafikiri
Kasisi ni shahidi tu,ndoa ni yao wanaofunga. Tunaishi mara moja tu huku duniani. Ni muhimu pia kujua malezi na aina ya familia ambayo mtu wako/mtarajiwa wako anatoka. Angalia sana nduguyo atakosa vyote.
Jamani aksanteni sana kwa ushauri wenu kwa kweli umenisaidia na kunipa moyo wa kuweza kumshauri dadangu ili ajue kipi cha kufanya. Nilikuwa naogopa kumshauri mwanzo kwa kuhofia kuwa huwenda nitakuwa nakosea kwa kuwa mie sijaolewa mambo ya ndoa siyajui.
Aksanteni sana