Ndoa za siku hizi kwanini ni shida?

Ndoa za siku hizi kwanini ni shida?

LadyJanja

Senior Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
101
Reaction score
48
Yan siku hizi mtu hata unaogopa kuolewa ..yan watu wanalia na kulalamikia ndoa zao dooooh...mungu asaidie kizazi chetu tuu
 
Pole mdogo wangu. Kwani samaki wanapovuliwa kila siku, wenzao wanahama kwenye maji?

Just play your game!
 
Mi natamani sana kuoa but wanawake wengi wanataka ndoa zinazowapa Uhuru wa kufanya ya kwao
 
Niliwambia msishinde MMU mtapotoka. Ona sasa umeshaogopeshwa kwa maneno ya watu hapa.

Acha uoga...explore ur own world.. Pray to God., you have a wife,a good wife smwhere.
 
Mi natamani sana kuoa but wanawake wengi wanataka ndoa zinazowapa Uhuru wa kufanya ya kwao

Noo sio hvo usiogope is just the matter uhakikishe unaemuona ni ur best friend mnaelewana sana na unampenda kwa dhati because foreva is too long to be unhappy
 
Niliwambia msishinde MMU mtapotoka. Ona sasa umeshaogopeshwa kwa maneno ya watu hapa.

Acha uoga...explore ur own world.. Pray to God., you have a wife,a good wife smwhere.

Amen..praying is the most important thing
 
MISINGI YA NDOA

~ Ndoa ni jambo jema (ni mapenzi/will of God)
~Kuna utimilifu wa kimaisha mwanamume na mwanamke wanapooana. Hata Mungu alisema si vema mtu huyu akaishi peke yake.
Kumbuka pia hata wajane vijana wanashauriwa kuolewa kama ni ngumu kwao kuishi bila kuwaka tamaa.

~Tangu awali wanawake walikuwa hawakutani na wanaume mpaka atakapoolewa. Hivyo aliyemtoa bikra ndo aliyekuwa mume wake. Na baada ya kuoana walitakiwa kuishi kwa uaminifu, no kuchepuka.
Ndiyo maana wanaume wakaambiwa usimtamani mke wa jirani yako pia usizini.

Kwa wasomaji wa neno wanakumbuka kuwa sifa za mabinti zilizokuwa zinatajwa moja wapo ni kuwa bikra, mariam, esther, mke wa isaka n.k mifano ni mingi.

SHIDA IKO WAPI?
~Watu wa leo hawataki kufata misingi ya ndoa. Wanataka wafanye wanavyojua wao.
~ukiwaambia vijana wanatakiwa kuwa bikra kabla ya kuoa wanakuja juu na kuona siyo sawa. Angalia hata mmu mada ikihusu bikra uone wasivyopenda.

~tabia kuanza kujamiiana kabla ya ndoa imeshika kasi sana na imezaa tabia ya kuanza kuishi pamoja bila ndoa. Kisingizio kikubwa eti wanaangaliana tabia.
Inawezekanaje kuangaliana tabia kwa kuharibu tabia?

~matokeo yake wanajikuta wameonja aina tofauti za watu. Kumbuka siku zote watu hawafanani, hivyo hiyo tabia ya kuonjaonja haiwezi kuisha. Ndipo hapo badala kuita "kufanya uzinzi" wakaita "kuchepuka" ili neno lisiwe na ukakasi, wazini kwa uhuru zaidi.

Hili ndilo tatizo kubwa, yapo na mengine lakini la "kucheat" ndilo linaua ndoa nyingi, linafanya watu kuishi bila upendo na furaha, watu wanakuwa na maumivu ya ndani.
 
Sababu zipo nyingi tu na zinajadiliwa huku kila mara,Mungu akikupa wa kwako aliyemkusudia,mnaofanana naye hutajutia na utafurahia ndoa. ILA ukioa mke msiofanana UTAKOMA.
 
Sababu zipo nyingi tu na zinajadiliwa huku kila mara,Mungu akikupa wa kwako aliyemkusudia,mnaofanana naye hutajutia na utafurahia ndoa. ILA ukioa mke msiofanana UTAKOMA.

Na Mungu akikupa wa kwako habari za "cheating" utazisikia tu kwa watu wengine.
 
Back
Top Bottom