Ndoa Yangu

SEHEMU YA 07

Akiwa ameongozana sambamba na mamayake Atu alisogea hadi kitandani nilipolala. Nilitamani ninyanyuke ila nilishindwa. Lakini cha ajabu kwa mara ya kwanza sauti ilitoka ingawa kwa shida sana lakini midomo ilinyanyuka.
"A-TU-GA-NI-LE" Niliita kwa kisitosito lakini nilifanikiwa kumwita binti yule huku machozi ya kutoamini yakizidi kunitoka. Hakika moyoni niliiona faraja na tumaini ambalo sikujua wapi litokapo. Atuganile alishindwa kujizuia na kujikuta naye machozi yakimdondoka.
"Mungu atakusaidia usilie...utapona mume wangu!" Aliongea maneno hayo huku akinishika kiganja cha mkono wa kulia na kulihisi joto lake likipenya kwenye maungo yangu mithili ya dawa iliyokuwa inaingia mwilini kuniponya na kunipa nguvu mpya.
Hakika nilishangaa leo Atu ananiita mume kama vile alivyoniita kwenye ndoto ile ya ajabu iliyotokana na tukio la mazingara.
Watu waliendelea kuingia na kutoka lakini si Atuganile. Sikutaka kabisa atoke. Niliona kama ndiyue mtu anayeweza nisaidia kupona haraka kila nilipomuona pembeni yangu. Mama Atu nilimsikia hata akimuaga mwanae ambaye hakutaka kabisa kuniacha mwenyewe. Nilishangaa kuona Atuganile ananionesha upendo wa ajabu ambao sikutaraji kuupata tokea aliponikatia simu siku ile.
Kitu ambacho sikukijua kumbe siku ile niliyopata matatizo ambayo ilikuwa jana yake. Habari zilipofika shuleni kwa kina Atuganile, ilimbidi atoroke na kuja kijijini kujua mengi zaidi kutokana ilibaki wiki moja tu shule kufungwa na walishamaliza mitihani.
Alijua fika Atuganile kuwa nampenda sana na kumbe tabia yake ilizidi kuwa kivutio moyoni mwake pasipo mwenyewe kujua lakinio sifa zangu zilimfikia.
Muda wa kuona wagonjwa ulipoisha Atu alibaki kama muhudumu wangu aliyekuwa akinipa uji na kunifutafuta. Hakika alinionesha upendo wa wazi na kuwaaminisha hata mafundi wenzangu kuwa kweli yule binti tunaendana sana na pia nina bahati mno kupendwa vile na binti mzuri, msomi na mwenye heshima.
Jioni ya siku hiyo hiyo mama sambamba na dada zangu wawili walifika wakiwa wametokea Dar huku wakiwa na nyuso za wasiwasi. Wote hawakuamini kunikuta nikiwa bado mzima. Walimshukuru sana Mungu ingawa nilishindwa kuzungumza vizuri lakini kushinda kwangu na Atu kulisaidia kunifanya ninyanyue mdomo kusema maneno machache kama kuitika salamu na mengineyo ingawa niliumia sana lakini nilijikaza nisionekane dhaifu mbele ya Atu wangu. Usiombe kupenda!
Kwa mara ya kwanza mama nilimtambulisha Atuganile kwa ishara kuwa ndiye binti niliyemwambia nimempata kwaajili ya Ndoa. Na hakika mama alipata faraja sana kutokana na heshima waliyooneshwa na Atuganile kwa kuwasalimia huku akikunja goti kabisa na alipotambulishwa kuwa ni mamaangu mzazi alisalimia tena kwa kupiga goti kabisa. Hakika ilipendeza na kufariji sana. Moyoni nilisali na kumuomba Mungu nipone haraka na ajaalie suala la Atu kuwa wangu wa maisha.
Usiku huo mama wakiongozwa na Atu walifanya maombi makubwa kuniombea. Hapo ndipo kikaonekana kipaji chengine cha Atuganile na kubainisha kuwa alikuwa mchamungu mzuri kumbe. Aliomba kwa imani hadi machozi yalimtoka.
".....Baba katika jina la Yesu tunakuomba na kukutumaini... Hakika kama ulivyotuahidi na kutukumbusha kuwa tusichoke kukuomba nasi usiku huu tunajiweka mbele yako muokozi wetu.... Utulinde na kumuondolea maradhi haya ya ajabu kijana wako baba.... Naiita nguvu yako kuu iweze kupenya na kuuleta uzima kwa kijana wako Onesmo. Hakika mbele ya Nuru yako hakuna giza lenye kuiziba....Navunja pepo la maradhi yehova.....Roho mtakatifu shuka na utende muujiza...Navunja mapepo ya maradhi na kuyachoma kwa moto wako mkuu baba... Uwajaalie watu wako wote wanaoteseka na pepo la maradhi ili wapone haraka warudi kukutumikia wewe muokozi.....Baba katika jina la Yesu tunaomba na kushukuru...Ameen" Yalikuwa ni baadhi ya maneno ya Atu katika maombi yale usiku ule. Imani ilizidi kunishiba nafsini kwa maombi ya Atuganile. Upande mmoja nilihisi kweli nuru njema ikijaa nafsini mwangu. Hakika kama ni maombi tu ya Atu basi muujiza wake ulianza kutendeka palepale hospitalini.
Kwani baada ya maombi usiku ule walielekea kulala kwenye nyumba ya daktari mmoja wa pale aliyekuwa ndiye daktari wangu na huku nyuma nikabaki na fomeni wangu usiku huo na dariri njema zilianza kuonekana. Kwanza niliweza hata kukaa na kutingisha viungo vyangu mwenyewe, kitu ambacho sikuwa naweza. Ingawa sikuweza kutembea wala kusimama mwenyewe lakini asubuhi yake niliweza kusema pasipo kuhisi maumivu makali ya koo kama ilivyokuwa awali.
Hiyo ilizidi kuwa chachu kuu ya kumpenda zaidi na zaidi Atuganile. Na si kwangu tu bali hata mama na dada zangu waliofika na kumuona.
Zilifika siku nne nikiwa hospitalini Kyela tokea nipatwe tatizo. Nilirudiwa kufanyiwa vipimo vyote lakini bado majibu yalisoma niko sawa asilimia zote sina ugonjwa wowote kisayansi. Hapo ndipo kila mmoja alichoka. Maombi ya Atuganile hayakukoma. Kila siku tulifanya sala pamoja tukiomba na kushukuru. Sindano nazo hazikukoma. Lakini kila nilivyochomwa sindano nilijisikia hali mbaya sana na hata kuhisi kama zitaendelea basi zinaweza kunimaliza kabisa. Safari hii niliweza kuzungumza ingawa si kwa sauti kubwa lakini pia hata maumivu hayakuwa makubwa kama awali.
"Mama! kama majibu yanaonesha siumwi sasa kwanini bado nipo hapa na hizi sindano ni za nini? Jamani mi sizitaki tena sitaki kuchomwa sindano." Niliongea siku hiyo ya nne na ndiyo siku niliyogoma kabisa kufanyiwa matibabu pale. Madaktari walinilazimu na kunisihi lakini mimi nilichoamini kinachonipa nguvu si sindano bali ni maombi ya Atu ambayo yalisikiwa moja kwa moja na Mungu. Na hapo ndipo nilipoletewa faili langu na kuambiwa kama sitaki basi nitie saini yangu ili waniruhusu. Bila kisto wala hofu nilikubali na kutitia sahihi. Na hiyo ikawa siku yangu ya mwisho kulala pale hospitali ingawa sikuwa na nguvu za kutembea mwenyewe lakini nilishikwa kila upande mpaka gest. Tulisindikizwa na Atuganile sambamba na mamaake aliyekuwa anakuja kila siku ingawa bintiye alilala na mamaangu pamoja na dadazangu wakishirikiana kuniuguza na kunifariji. Habari ya kugomea kwangu matibabu pale Kyela kila mmoja aliipokea kivyake. Wengine waliniunga mkono huku wengine wakinilaumu. Kampuni ililipa gharama zote na kuniingizia mshahara wangu wa mwezi ili uweze kunisaidia pamoja na laki moja kwaajili ya nauli ya kurudi Dar kwa matibabu zaidi kama tulivyodai.
"Vipi Atu mwanangu si tutaenda wote nawe ukamuuguze mwenzio na kuendelea kumfanyia maombi eeeh!" Mamaangu alimuuliza Atu huku akimuomba.
Atu hakubisha zaidi alikubali ingawa alidai kuwa kwakuwa anaingia kidaqto cha nne basi shule zitapofunguliwa tu itamlazimu arudi haraka kuendelea na masomo.
"Hilo halina tabu mwanangu." Ndipo hapo mamaangu walipozungumza na mamaake Atuganile ambaye kwa sauti ya huruma alisema.
"Mwanangu Atuganile nilipenda sana likizo hii aitumie kujisomea kwaajili ya kupambana na kidato cha nne ili asifeli.Ila hakika kijana wake Onesmo ni kijana wa tofauti sana na nimeona kiasi gani wanapendana na mwanangu ingawa sipendi kuona wanaingia kwenye mahusiano kwa sasa. Najua Atu bado mtoto ila One tayari anajua kila kitu. Hivyo nakuomba mama One, kwa dhamana yako namruhusu mwanangu muende naye ila ninachokusihi msiwape uhuru wa kulala pamoja pindi One atapopata nguvu na ahueni inaweza kutokea ya kutokea halafu ndoto za mwanangu zikafia njiani. Ila nimekubali One awe mkwe wangu hapo badae pindi Atu akimaliza shule."
Maneno ya mama Atuganile yaliungwa mkono na mama. Kesho yake asubuhi na mapema mama Atu ambaye naye alilala gesti moja nasi, alitusindikiza mpaka kituo cha basi na kupnda basi pamoja na Atuganile ambaye sikuamini muda wote kama sasa anaenda kwetu kama mke wangu mtarajiwa. Hakika moyo ulifura furaha huku nafsi ikiyaona matumaini. Matumaini ya ushindi wa kupata mke bora aliyekamili kuanzia sura, umbo, mpaka tabia.
Lakini doooh! sikujua kama Ndoa yangu inaweza kuwa Nuru iliyobebwa na nafsi ya kiza.
Atuganileeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!???
 
SEHEMU YA 08
Tulisafiri salama usalimini. Tulifika jijini Dar. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Atuganile kukanyaga jiji hili lenye uso wa malaika kwa nje huku likiwa na moyo wa shetani kwa ndani. Watu wawili waliokuwa wakinishikilia muda wote pindi nitembeapo alikuwa dadaangu mmoja na Atuganile wangu. Tulifika nyumbani na matibabu sasa yakawa ya kiroho kutokana na tatizo langu pindi nilipolihadithia kile nilichokiona kikinitokea ingawa nilificha kuhusu kumuona Atuganile katika ulimwengu ule wa ajabu ambao sikujua kama nilikuwa naota ama nilifika kweli.
Kila siku walikuja wachungaji kunifanyia maombi na kukemea mapepo. Atuganile alikuwa mstari wa mbvele katika kila sala. Heshima, upendo, unyenyekevu na adabu iliyopotea kwa mabinti wa kileo ilikuwa ni vitu alivyobaki navyo Atuganile. Kila aliyemuona pale nyumbani alimsifu kwa uchapaji kazi, na kila mkubwa aliyemsalimia alimkunjia goti. Hakika tabia zake hazikutumbeza sisi pekee bali hadi majirani walimpenda mno na kutamani mabinti wao wangekuwa kama Atuganile. Kwa kipindi cha mwezi mmoja aliokaa nasi tayari alishapata umaarufu kwa tabia zake nzuri na za kusisimua hata uhadithiwapo tu. Hakuwa mzururaji Atuganile wala mtu wa kukaa na mabinti rika lake kuzungumza kwa vikundi. muda wote alikuwa karibu nami kunifariji na kunifanya niweze kujikaza hata kuanza kuchukua mazoezi ya kutembea baada ya mwezi mmoja. Alikuwa yeye ndiye mwalimu wa kunifanyisha mazoezi. Alisogeza mwezi mmoja mbele baada ya shule kufunguliwa ilimradi ahakikishe ananiacha katika hali ya kuridhisha. Na kweli kila mtu alimshukuru pale nyumbani na kumuombea mazuri kwa mwenyezi Mungu. Ingawa alipenda sana shle lakini kitendo cha kuwa tayari kuchelewa kwenda shule kwa sababu yangu ilizidi kudhihirisha jinsi gani nina thamni zaidi kwake. Alikuwa tayari hata kukutana na adhabu shuleni eti yopte kwa sababu yangu. Aaaaah! Atuganile ama kweli alituonesha yeye ni binti wa kiafrika aliyefunzwa nini maana ya utu na heshima.
Ilipotimu miezi miwili sasa niliweza kutembea mwenyewe pasipo kushikiliwa. Niliweza kuzungumza hata kwa sauti mtu akanisikia. Ingawa sikuwa na nguvu ya kufanya kazi hususani kunyanyua vitu vizito lakini nguvu ya kumbeba Atuganile nilikuwa nayo. Sikujua ilitokea wapi nguvu hii.
"Baby leo nataka nikubebe!"
"Wee One nisije nikakuvunja buree!"
"Univunje! mimi mpingo wee panda uone."
"Akuu, mi naogopa!"
"Basi ngojaa..." kwa ghafla nilimkunja miguuni na kumshikilia mgongoni na kumnyanyua Atu siku hiyo asubuhi tulipokuwa uwanjani tukifanya mazoezi.
"Aaaah hahahaa jamaniii bebiiii" alitoa ukelele wa kudeka na kuzidi kunipa ujasiri na nguvu. Hata watu wengine waliokuwa wanafanya mazoezi asubuhi hiyo walituangalia sana. Ilikuwa kawaida kila ninapopita na Atuganile watu kutukodolea. Si wa kike si wa kiume, wakubwa kwa wadogo. Hakika ilinipa taswira njema kiasi gani tunaendana. Pia nilielewa uzuri wa Atuganile uliwachanganya japo kuwa Dar kulikuwa na wazuri wengi lakini bado Atu alikuwa na kitu cha kipekee sana ambacho kinaweza ustua moyo wa kidume yeyote pindi amtazamapo. Uso wake ulishiba nuru ya huba. Na japokuwa nilikuwa mgonjwa bado lakini sikutaka kuonesha udhaifu pindi nitembeapo na Atu.
"Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki. Atu amenifaa kipindi hiki kigumu cha ugonjwa, hakika sitoweza kumuacha wala sina cha kumlipa kikubwa zaidi ya kumuoa. Hakika Mungu ndiye alinipa mtihani ule kama ufunuo wa kumuona mke bora wa maisha yangu. Hakika bwana amenionesha. Atu ni mke halali kabisa kutoka kwa Mungu." hivyo ndivyo nilivyowaza siku zote na kuamini hivyo. Nilisema na moyo wangu hata kumwambia kila niliyemuamini kumwambia mambo yangu ya ndani. Kiufupi Atuganile alionesha kila aina ya sifa ya mwanamke bora tena hadimu katika kizazi cha leo.
Baada ya zaidi ya siku hizo sitini hatimaye ilisalia siku moja ya Atuganile kuwa nasi kabla ya kurudi Mbeya kuendelea na masomo. Hiyo ilikuwa siku ya maumivu mengine kwa upande wangu. Maumivu ya kuwa mbali tena na Atu ambaye nilishamzoea sana ingawa kwa kipindi hiko chote tulichokuwa pamoja hatujawahi kulala pamoja usiku. Kama alivyoomba mama Atu na ndivyo mama alivyohakikisha inakuwa hivyo. Lakini kwa usiku huo mmoja ilibidi nimuombe mama Atuganile alale chumbani kwangu kwa nia ya kuzungumza mipango yetu mingi ya baadae. Ingawa mama alikubali lakini alinisisitiza kuwa nisije kuthubutu kutenda dhambi kabla ya ndoa. Nilimuelewa mama amaanishacho na kumuahidi kuweka zingatio.
Usiku huo nilitamani usiishe. Ilikuwa mara ya kwanza kuwa kitanda kimoja na Atuganile tena usiku. Tulizungumza na kupeana ahadi nyingi sana.
"Atuganile, wewe ni mzuri sana naogopa hata unavyorudi huko wanaweza kuniibia ukanisahau! mwaka mmoja ni mwingi sana hebu niahidi Atu"
"One, amini sikuwahi kuwa na mwanaume yeyote hata wa kufanya naye utani zaidi yako. Wewe ndiye mtu wa kwanza kukuita mpenzi wangu..Amini nakupenda sana zaidi ya sana. Na siku zote nitakusubiri wewe tu." Kwa sauti yake ya kinanda Atu alinambia na kuyafanya mapigo yangu yaende kasi kadri alivyonikumbatia. Joto la mwili wake lilipelekea hata pumzi zangu kutoka kwa mihemko ya hamu huku sauti yangu ikizidi kuwa nzito pindi nilipomuuliza.....
"Ina maana Atu hadi hapo ulipo hujawahi kufanya mapenzi?"
"Ndio One! wala sijui yana utamu gani na sitaki kuujua utamu huo kabla ya kuolewa. Mama alinambia zawadi nzuri ya heshima kwa mwanamke mwema ni kukutwa bikra na mume wake wa ndoa. Zaidi ya hapo hakuna zawadi yoyote ya heshima kwa mke mbele ya mume." Majibu ya Atuganile yalizidi kunichanganya hata kumfanya kifimbo cheza wangu aanze kuchezacheza kwa ubea akitamani kuona na kuhakikisha kile kisemwacho na binti yule malkia wa mtima wangu.
"Atu kama hujawahi kunidanganya basi nahisi leo ndio mara ya kwanza unanidanganya."
"Kwanini One mume wangu jamani?"
"Tuseme kweli Atu wewe ni bikra?"
"Kweli jamani kwanini nikudanganye sasa ina maana gani?"
"Naomba Atu wangu tena nakuomba sana kama ni kweli hebu toa nguo nikuone!"
"Mmmh! siwezi jamani One naomba uwe muelewa na mwenye imani"
"Atu, ina maana huwezi kuvua nguo mbele ya mtu uliyejitoa moyoni mwake kuwa mumeo wa maisha?" Nilibembeleza sana na kutumia kila aina ya maneno ya ushawishi yenye chachandu za utamu hata mwishowe niliweza kuanza mpambua Atuganile nguo moja baada ya nyengine.
"One nakuomba sana, nakupenda sana leo kwa mara ya kwanza naruhusu unichungulie lakini si kwa kunifanya kitu chochote zaidi nakuomba sana mume wangu shinda moyo kuwa na subira." Alinisisitiza Atuganile kipindi nilipokuwa nafanya ukaguzi mwilini mwake. Lakini daah! ama kweli sisi wanaume ni watu wa ajabu mbele ya wanawake, mbali ya sisitizo la Atuganile wangu lakini usiku huo nilijisahau kabisa kama mimi ndiye mgonjwa ambaye bado sikuwa na nguivu za kutosha lakini pale nilipomtazama Atu alipobaki na kufuri tu la pinki, akili zangu zilizidi kuhama na kufikiria kutoa kitu ambacho wanaume wengi tunaamini kama ni bahati (bikra) kukikuta kwa mwanamke tena aliye mzuri kama Atuganile.
Muda huo wote Atu alijiziba uso kwa viganja vyake akishindwa kustahimili kunitazama pindi nilipokuwa naukagua mwili wake. Hakika sifa kubwa nyengine ya Atuganile ilikuwa ni usafi. Alikuwa msafi mno mwilini mwake. Hakuwa na alama ya doa wala ukurutu. Alivutia kumtazama mapaja yake mazuri wala hakuwa hata na harufu yoyote mbaya hata ile kwa mbaali. Na zaidi hakuwa anajipulizia pafyumu zaidi ya kujipaka mafuta ya mgando lakini bado asili ya ngozi yake labda kutokana na usafi wake aliendelea kunukia vizuri kabisa.
Uvumilivu ulizidi kunishinda pale nilipomkalia juu Atu kwa lengo la kumchunguza eti kama bikra kweli lakini sasa ibilisi alinikaa kichwani na kusahau hata alichonambia mama na kujiandaa kufanya kitu ambacho hatujakubaliana na yeyote hata Atu mwenyewe.
 
SEHEMU YA 09

"ONEEE!" Alistuka sana Atu punde dungudungu langu lilipogusa maungo yake. Hakika pasipo ubishi kwa jinsi nilivyomvizia ingekuwa ametoboka basi walau kichwa kingezama, lakini ukweli Atu alikuwa 'sild' mtoto bado mpya kabisaaaa. Huo ndio ulikuwa ukweli niliouhakiki hata kabla sijamseti njoma nchumali toboa tobo akafanye mambo yake. Lakini alijikuta akishindwa baada ya Atu kuruka nyuma ya kitanda na kubana miguu huku akiwa ameonesha kuogopa na kukasirishwa na kitendo changu cha kutaka kuvunja mkataba.
"Kwanini unakosa subira One? kwanini unataka kunipa wakati mgumu eeh! ina maana unanionesha jinsi gani una tamaa ya ngono si ndio? basi usijali fanya na wengine ila mimi siwezi hadi nitapoolewa kama utaweza kunisubiri sawa kama hutoweza basi utakuwa sio mpango wa Mungu." aliongea Atu huku akitoa machozi.
Hakika moyo uliniuma na kuona makosa yangu. Nilimkumbatia na kumuomba msamaha kwa maneno matamu.
"Naomba uniamini One wangu eeh! yaani niweze kujitunza miaka yote shule tena nikiwa mwenyewe sina mtu yeote wa malengo halafu nishindwe mwaka mmoja? Naomba usinidhanie mabaya hivyo One. Nakupenda sana moyoni mwangu nimukuweka wewe tu wa maisha yangu naomba uwe na subira nisubiri mimi mume wangu." Aliongea Atu na kunikumbatia pia.
Nilimuacha avae nguo zake huku akiwa na uso wa tabasamu sikuwa na jinsi zaidi ya kuulazimu moyo uwe na subira. Jambo lengine nililoligundua kwa Atuganile si mtu wa kuchukia muda mrefu na ni mwepesi wa kuelewa na kusamehe.
Basi usiku huo tulipiga stori za hapa na pale mpaka alfajiri ilipofika Atu alijiandaa na tulimsindikiza mpaka kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo huku akiwa tumemfungashiwa zawadi mbalimbali ikiwemo simu kubwa ya kisasa kwaajili ya mawasiliano, madaftari, begi la shule, nguo kadhaa na nilimpa pesa tasilimu laki moja za kuanzia matumizi shuleni huku nikumuahidi kumtumia pesa zenginezo pale zitapohitajika ili mradi asome kwa amani na aepuke vishawishi kwani tayari yeye ni mke wa mtu anayesubiri ndoa tu.
"One kaka angu endapo usipomuoa huyu binti sidhani kama utaoa mke bora. Hakika hii ni bahati aliyokushushia bwana! Atuganile ni mke mwema sana na atakufaa maishani." Hayo yalikuwa maneno ya dadaangu mkubwa siku tuliyomsindikiza Atuganile tukiwa tunarejea nyumbani baada ya basi alilopanda kuondoka. Hata marafiki zangu wa karibu waliokuwa wanakuja kuniona pindi nilipokuwa nyumbani hawakuisha kumsifia mchumbaangu Atu mpaka majirani walinisisitiza kuwa nisije kumuacha binti yule.
Moyoni nilijisikia fahari na kumuamini Atuganile kwa asilimia kubwa pengine hata ndugu zangu wa karibu kama dada zangu ama marafiki wengineo.Ukisema kwa wakati huo uupasue moyo wangu katika watu niwaaminio basi utaikuta picha ya mamaangu mzazi na Atuganile. Tena nathubutu kusema hata kwa asilimia walikaribiana sana. Ingawa imani ilizidi sana kwa mama lakini bado na Atuganile nilimuamini kwa kiwango kikubwa mno. Hakukuwa na sababu yoyote ya msingi niliyoiona ambayo ilifanya nisimuamini Atuganile. Hakika alikuwa ni mwanamke anayeweza kumpagawisha mwanaume yoyote kwa tabia zake alizotuonesha ukijumlisha na uzuri wake wa ndani na nje! hakika huwezi kuruka.
Niliuachia moyo wangu ugande kwa Atuganile. Macho yangu yakapofuka kwa wanawake. Hakika nilikufa na kuoza kama wasemavyo vijana wa mjini. Nilidata kwa kumpenda Atuganile. Kila mara tuliwasiliana hususani nyakati za usiku kwa kuchati. Mara nyingi Atuganile aliniandikia maneno 'I LOVE YOU SO MUCH ONE, YOU'RE MY EVERYTHING THE ONE AND ONLY'
Hakika maneno haya yalinipa nguvu na imani kuwa mimi ndiye kidume na Atu ni wa kwangu pekeyangu.
Baaa ya miezi mitatu kupita, mwezi mmoja baada ya kuondoka Atuganile hatimaye nilipona kabisa. Niliweza hata kufanya kazi japokuwa barua ya kumalizika mradi na kusimamishwa kazi ililetwa nikiwa nyumbani. Nakumbuka Sulu alikuja kunitembelea siku moja baada ya kazi kuisha huko Mbeya na nilimuhadithia juu ya Atuganile alifurahi sana na hakuamini kama kweli Atu alikuwa 'sild'
"Ila One kuna kitu ambacho umehofia kufanya ni heri ugefanya tu mwanangu! mi nawajua wanawake... Anaweza akakupenda kupita maelezo lakini kama atatokea mtu huko akakuzidi na kumpochoa mtoto basi andika umekosa. Wee ungamchapa kabisa wanawake vigeugeu hawa! Watu wanawinda na asikudanganye atakuwa mtaalamu wa kukataa kila siku, kila mara ama kila atayemtongoza."
Maneno ya Sulu yalinifanya nicheke sana na kumpuuza huku nikimuona hayajui mapenzi wala hajawahi kupendwa ama kupenda.
"Sikia Sulu, yule mtoto anajitambua mwanangu! sio kama mademu zako uliowazoea magubegube. Kwanza mtoto msomi na ana ndoto za kufika mbali."
"Powa mzee kama ni hivyo ila kuwa muangalifu hata kama unampenda sana angalia asiyajue mazaifu yako anaweza kuja kukutesa baadae."
Alinisistiza Sulu.
*********
Siku zilikwenda huku nikizidi kujipanga kimaisha hususani baada ya kupata pesa zangu za mafao (nssf) nilifungua biashara ya video game (play station) pamoja na duka la nguo. Nilijianda vizuri kimaisha kwa kweli kiasi fulani nilijitahidi kutumia pesa zangu katika mambo ya msingi kimaisha. Usisahau hadi kipindi hiko nilikuwa na kiwanja changu ambacho tayari nilishauanza msingi niliamini pindi biashara zangu zitapokuwa zimenyooka basi ningeanza kujenga taratibu huku nikiwa na mke wangu kipenzi Atuganile. Mwaka ulikatika na hatimaye Atuganile alihitimu kidato cha nne na shauku ikabaki kwenye majibu ya kuendelea. Kwa akili alizokuwa nazo Atuganile kila mtu aliamini angefaulu pindi majibu yatapotoka.
Katika mawasiliano nilimtaka Atuganile aje tena kipindi akisubiria majibu lakini hilo halikuwa rahisi baada ya kuambiwa tayari alishalipiwa 'tuition' huko huko kipindi akingoja majibu yatoke. Ingawa tulikuwa mbali lakini mawasiliano yalituweka karibu mara zote. Si yeye tu bali hata mamaake na mamaangu walikuwa na mawasiliano ya ukaribu sana.
Siku hazikuganda na hatimaye ilifika siku ya matokeo kitaifa ya kidato cha nne mwaka huo. Shauku yetu ilikuwa juu ya matokeo ya Atuganile.
Lakini katika jambo ambalo hakuna aliyelitarajia Atuganile hakuweza kuchaguliwa kuendelea na masomo ya juu. Namaanisha matokeo yake hayakuwa mazuri ingawa alipata daraja la nne. Alilia sana Atuganile. Alilia huku akilalama kuona ndoto yake inaishia njiani. Malengo yake ilikuwa asome ili aje awe daktari.
Kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa kila kitu kwake kama alivyoniita na kuniandikia. Chozi lake liliniuma sana. Moyo wangu ukawa tayari kulipokea chozi la Atuganile na kulifuta. Hapo ndipo niliingia mkataba wa uchumba rasmi. Tulisafiri mpaka kwa kina Atu na kwa kuwa mira zetu zilikuwa tofauti tulifundishwa mira za kwao na kuweza mpata mshenga na kuandika barua ya uchumba. Ilijibiwa na tulitoa kifungua uchumba na baadhi ya vitu vya mila huku kubaliano kubwa likiwa ni ndoa baada ya Atuganile kufikia elimu ya chuo. Niliahidi kumsomesha kutokana na kwao kukosa kabisa uwezo wa kumlipia sekondari za binafsi. Hata mama na dada zangu walinishawishi na kunisihi kuwa kumsomesha Atuganile wala sio ujinga kwani ni mtu muhimu sana kwetu na kwa kuwa anazo akili za shule basi nifanye hivyo na atapomaliza kidato cha sita kipindi anajiandaa kuanza masomo ya chuo kikuu basi ni muda muafaka kwetu kufunga ndoa huku yeye akiendelea na masomo ya elimu ya juu nami nikiendelea na shughuli nyengine za kimaisha. Wazo hilo nililipokea ingawa nilipomshirikisha Sulu alinilaumu na kunikumbusha kuwa nisiwaamini sana wanawake ni vigeugeu. Lakini kauli za Sulu zilibaki kunichekesha tu na kumdharau. Nilikubaliana nae sa wanawake ni vigeugeu lakini si kwa Atuganile. Hakika nilimuamini mno. Nilimuamini hata nilipowazungumzia wanawake basi yeye nilimuweka kwenye kundi tofauti kama vile si mwanamke. Nilijisahau kuwa hata Atu naye ni mwanamke vilevile. Hivi kweli Wanawake ni wauaji?! Inaweza kuwa hapana..! lakini kama utaishi nao kizembe hakika watakuua japo hawatakutoa uhai.........Sikujua wala sikuwahi kuona dariri yoyote wala ishara ya ubaya wa Atuganile. Hakika kila unachokisoma ndivyo ilivyokuwa. Huyo ndiye Atuganile ambaye bila shaka hata wewe amekuvutia. Lakini........................! kuwa nami uyaone majuto yangu ambayo hata wewe yanaweza kukukuta kwani kina Atuganile ni wengi sana. Ooooooh! NDOA YANGU!
chozi langu litalipwa!
 
SEHEMU YA 10

Baada ya kupata shule na kulipia gharama za ada na mambo mengine Atu aliweza kusoma huku akiwa mwenye furaha na faraja ya moyo. Shule ilikuwa mkoani Morogoro. Kabla hajaondoka masomoni tuliongea mengi sana na kuniahidi kuwa zawadi yangu ya ndoa atanitunzia wala nisiwe na haraka naye. Si jambo rahisi lakini kwangu lilikuwa. Nilimuamini sana Atuganile na wala hakuonesha kubadilika chochote kitabia hata kimwili bado alikuwa Atu wangu yuleyule. Hakika alinipa nguvu ya kutafuta pesa na kumsomesha hata kupelekea kusimamisha ujenzi wa nyumba yangu nilioianza msingi. Sikuwa tajiri lakini nilipambana kuhakikisha mke wangu mtarajiwa shuleni anaishi katika mazingira bora ya kumuweka mbali na vishawishi. Kwa kuwa hakuwa na ndugu Morogoro ilibidi nilipie na bweni la kulala. Ukijumlisha na gharama za ada ilikuwa ni zaidi ya milioni moja kwa mwaka.
Sikuwahi kuzifikiria pesa hizo wala kujutia kuzitoa kwa ajili ya Atuganile. Kwa pesa ya matumizi pekee ambayo nilikuwa namtumia Atuganile kila wiki ilikuwa si chini ya elfu hamsini. Pia sikuacha kumtembelea kukutana naye walau kwa mwezi mara mbili ama mara moja.
"One nakupenda sana mume wangu. Ila naomba usinielewe vibaya kwa haya nitayokwambia." Alinambia siku moja Atuganile alipokuja kwenye mgahawa wa lodge niliyofikia Morogoro. Ilikuwa kawaida kukutania mgahawani na si mimi kwenda shuleni moja kwa moja kwa maadili ya shule haikuwa wazi kama Atuganile ana mchumba. Ingekuwa tatizo lengine kiserikali ya nchi yetu ingawa kiuhalisia Atuganile hakuwa mtoto. Nilitulia siku hiyo kumsikiliza kitu gani alichoniwia radhi kabla hata hajanambia! ndipo kwa upole akasema.
"One, najua unanipenda pia najivunia kuwa na mwanaume mwenye kujali na kunisikiliza kama wewe. You are my everything Onesmo mume wangu wa maisha. Ila pia najua unajua kama napenda sana kusoma lakini muda mwingi najikuta nakufikiria sana wewe unavyotumia pesa kuja mara kwa mara tena unalala lodge halafu mi nakuja tunazungumza tu mchana naondoka. Nafikiria pesa za nauli unazotumia na gharama nyengine za kuja huku kila mwezi kama utazitunza unaweza kufanya kitu muhimu zaidi mchumbaangu. Pia itanisaidia hata mimi kupata muda wa kusoma. Nakuomba basi hata uwe unakuja huku kila baada ya miezi sita ila si kwania mbaya baby wangu."
Maneno ya Atu siku hiyo yalinifanya nishushe pumzi kwa mara ya kwanza na kuna hisia mbaya ilinivamia nisijue ilipotokea. Atuganile alinisoma hilo baada ya kushusha kwangu pumzi na kukaa kimya kwa muda.
"One baby wangu kama nimekukera ama kukuudhi kwa hilo naomba unisamehe sana. wewe ndiye mume wangu na ndiye mwenye maamuzi ila nimekushauri kwa aida kama mkeo hakika sina cha kuweka moyoni kwa mume wangu ili nisiwe mnafiki. Hakuna mwanaume yeyote anayeweza zishawishi akili zangu zibadilike na kwa hapa tulipofika ni hatua kubwa mume wangu. Unaweza kuhisi vibaya lakini ukweli tuzitunze pesa mume wangu. Si kama sipendi uje hapana tena natamani hata ungekuwa unakuja kila siku ila ndio hivyo baby itatupa muda mimi na wewe kujiandaa kwaajili ya kesho." Alinifafanulia zaidi na zaidi Atu nia ya maneno yake. Hatimaye nilimuelewa na mawazo potofu yaliyotaka kuteka hisia zangu yaliondoka haraka na kunijia mawazo ya kumpandisha zaidi daraja Atuganile kuwa ni mwanamke anayejali sana na mwenye akili ya maisha. Ni kweli nilikuwa natumia pesa nyingi muda mwengine ambazo hazikuwa na ulazima. Kila siku tulikuwa tunawasiliana na Atu na pia kupitia whatsapp tulirushiana picha na video. Sasa nilijiuliza kuna sababu ipi inayonipeleka mara kwa mara Morogoro ikiwa hata nikifika hatulali pamoja wala hatufanyi chochote zaidi ya kuzungumza tena mara nyingi alikuwa anapenda kuja na rafiki yake mmoja aliyeitwa Hellen.
Nilimuelewa mchumbaangu na kufuta imani mbaya kuanzia hapo sikuwa naenda mara kwa mara Morogoro ingawa hali ya kutamani kuongea naye macho kwa macho haikuniisha.
Nakumbuka kuna siku Sulu alikuja kunitembelea baada ya miezi kadhaa kupita. Ilikuwa ni mwaka umepita tokea Atuganile aanze masomo ya kidato cha tano na sita. Sulu kwa kipindi hiko hakuwa anajua mengi kuhusu Atuganile kwasababu ya kumficha mambo mengi. Sikupenda kuendelea kumwambia habari zangu na Atuganile tena kwani mara nyingi aliniudhi kwa maneno yake kuhusu Atuganile.
"One, unajua sasa hivi unabadilika sana?"
aliniuliza Sulu swali lililonipa maswali kadhaa.
"kivipi Sulu?"
"Najua kwa sasa huwezi kunielewa kwa kuwa moyo wako ushapofua utimamu wa akili zako. Ndio maana unanificha mambo yako mengi toka uwe karibu na Atuganile. Nina mashaka yasije haya kutokea hata kwa ndugu zako wa karibu hususani mamaako One! Hebu omaa kichwa wewe ni mwanaume mapenzi hayako hivyo wanawake si watu wa kuwaamini kwa kiwango kama chako utayumba ndugu yangu."
\Kwa mara nyengine tena Sulu alinipa kero ya moyo.
"Kwani mshkaji wangu yule mtoto ulimtongoza nini akakukataa?" Nilimuuliza huku nikishindwa kuzificha hasira zangu.
"Duuh! ndio tumefika huko sasa?"
"Hapana! maana tokea Atuganile aoneshe kiasi gani ananipenda na amejitoa kwa sababu yangu basi mwanangu huishiwi nongwa! mara eeeh mara aaah hivi ulitaka Atu anioneshe nini hadi nimuamini kwenye mapenzi? binti wa watu kajitolea kuacha shule ili aje nkuniuguza mimi! hadi anamaliza kidato cha nne na hadi leo bado yuko vilevile hajaguswa na mwanaume yeyote. Hivi kwa tukio hilo tu la mwanamke kusoma hadi kidato cha nne na bado bikra huoni kama ni mwanamke mwenye akili na msimamo? Mbali na hayo wakubwa wote wanaomjua Atuganile wanamsifia na kunisihi kuwa ni mwanamke bora, lakini wewe tu ndiye kiranga daah! shika zako mwanangu kama huna zuri la kuongea kuhusu Atuganile ni heri unyamaze tu nishachoka maneno yako."
Nilimtolea uvivu Sulu. Kusema kweli katika kitu ambacho sikuwahi kufikiria hapo kabla kama kuna siku nitakuja kugombana na Sulu ama kutoleana maneno yoyote makali. Na hilo sikuweza kulikumbuka kabisa hata siku hiyo nilipomtamkia maneno hayo Sulu huku uso wamhu ukiwasilisha kile kilicho moyoni mwangu.
"Daaah! asante sana One mwanangu. Naomba unisamehe sana kwa ujinga wangu! nimekoma na nimejifunza kaka. Ila cha mwisho nakukumbusha kipindi ukitumia gharama za kumsomesha Atu, umkumbuke na mtoto wa dadaako aliyefeli darasa la saba mpaka sasa yuko nyumbani umpeleke hata shule ya ufundi kwani hata asipokusaidia wewe akamsaidia mamaake itakuwa bado kamsaidia dada yako, akimsaidia bibi yake itakuwa bado kamsaidia mama yako, na wewe utabaki kuwa mjombaake. Lakini siku moja Atu anaweza kuwa si mkeo akawa mke wa mwengine pia na yote uliyoyafanya itabaki kuwa faida kwake na kwao huku kwenu kukibaki hadithi na hasara."
"Sulu tembea mwanangu achana na mimi. Jali maisha yako na kwenu bwana."
Hivyo ndivyo tulivyoachana na Sulu na urafiki wetu damudamu ukafa rasmi.
Kwa kipindi hiko sikuumia hata chembe kuvunja urafiki wa dhati baina yangu na Sulu. Nilisahau kabisa kama yule ndiye pacha wangu wa site. Nilisahau kama yule ndiye alikuwa anakuja getto kwangu na demu wake hata kumuachia chumba kwa jinsi nilivyomuamini. Nilisahau kama yule ndiye mtu niliyekuwa nina amani kukaa naye na kupiga naye stori muda wote. Nilisahau kama yule ndiye aliyeniaminisha siku ya kwanza kuwa Atuganile nishampata. Nilisahau kuwa yule ndiye alikuwa mshauri wangu mkubwa wa kumwambia mambo yangu mengi na siku zote nilifaidika kwa ushauri wake lakini si ushauri aliokuwa ananipa kuhusu Atuganile. Niliona wazi ananifundisha kuwa na roho mbaya na ubinafsi. Pia aliniudhi zaidi kumuhisia vibaya Atuganile ikiwa hajawahi kuishi naye hata siku tatu tu! wala hakuwa na mazoea naye kivile hata ya kuitana shemeji ingawa waliwahi kuonana.
Ingawa ni kweli kulikuwa na mtoto wa dadaangu alifeli darasa la saba lakini sikuwa nimemsahau ila uwezo wa kiuchumi wa kusomesha watu wawili sikuwa nao japokuwa ada ya kumsomesha Atuganile ilikuwa kubwa zaidi haikufikia hata nusu ya kumsomeshea mtoto wa dadaangu. Ila kwa kuwa hata dada zangu walimkubali Atuganile, niliamini pindi atapomaliza shule, tukaoana akaanza chuo basi itakuwa rahisi kuwasaidia ndugu zangu wengineo kwani naye atakuwa amepata kazi yake ya utabibu itayoleta kipato kikubwa ndani ukichangia na kipato changu basi wajomba zangu watasoma tu kwani elimu haina mwisho.
Lakini daaah! sikujua kama mtoto wangu kuhusu Atuganile aitwae 'ubishi'.... siku moja ataniletea mjukuu aitwae 'majuto'...
Masikini NDOA YANGU
 
SEHEMU YA 11
Siku zilisogea hatimaye ikapita miaka miwili zaidi Atuganile alihitimu kidato cha sita. Katika katika hali ambayo ilinistaajabisha kidogo ni baada ya Atuganile kurudi Mbeya moja kwa moja kabla hajapitia Dar wala kunitaarifu kuwa anaondoka siku hiyo hadi nilipompigia.
"Atu mbona umeondoka kabla hajaja kama tulivyozungumza ihali likizo ni ndefu hadi matokeo yatapotoka?" niliuliza kwa njia ya siu pindi Atu liponambia kuwa tayari yuko Mbeya ameondoka jana yake.
"Mume wangu naomba unisamehe kwakweli, ila nilikutafuta ukawa hupatikani halafu nilimkumbuka sana mama, nikaona ni bora nije kwanza nimuone ndio nije huko kwako bebiii."
"Mmh!" Niliguna baada ya jibu lake huku nikivuta kumbukumbu kama kuna siku za karibuni simu yangu haikuwa hewani. Jibu lilikuwa hapana! lakini hiyo haikunipa sana mashaka ya hisia tofauti juu ya Atu. Moyo wangu ulinambia kuwa ni kweli amemkumbuka sana mamayake na alinitafuta ila muda mwengine mitandao inadanganya kwa kuzidiwa 'network'. Niliongea pia na mama yake kama kawaida na siku zikaenda huku nikimruhusu mchumbaangu akae kwa mama mpaka kiu chake kitapokatika ndipo aje jijini tufanye taratibu zenginezo. Tayari nilikuwa na sauti kwa namna moja kwa kina Atuganile hata wajomba zake walijua kuwa Atu ana mchumba na ndiye aliyemuendeleza kielimu.
Alikaa zaidi ya mwezi kabla ya kuja tena jijini. Nakumbuka tuliwasiliana hata nikamtumia nauli. Niliganda ubungo kumsubiria mpaka mishale ya saa moja usiku huku tukiwasiliana hatua kwa hatua.
"Niko Mbezi baby wangu nimechoka kweli. halafu simu inaelekea kuzima chaji."
Hiyo ilikuwa ni meseji yake iliyonizidishia umakini hata nikasimama jirani kabisa na geti la kuingilia mabasi yatokayo mikoani hususani nikiisubiri SAI BABA ya Mbeya ambayo ndiyo alinambia amepanda. Niliganda na kukodoa pasipo kuiona basi hiyo. Simu nilipiga haikupatikana. Sikufa moyo nikajipa imani kuwa huenda foleni ya Mbezi Kimara ndio tatizo ingawa ilishafika saa tatu kasoro usiku. Hatimaye iligota saa nne usiku. Hakuna cha Saibaba wala Saimama niliyoiona ikiingia ikitokea Mbeya muda huo. Hapo ndipo nilipokata shauri na kuingia ndani kabisa hadi ofisi za Saibaba kuwauliza wahusika nini kimetokea juu ya basi yao.
"Kaka, mbona basi yetu ya Mbeya ilifika mapema saa kumi na mbili!" alijibu dada niliyemuuliza na kunifanya nichoke maana hadi saa kumi na mbili niliwasiliana na Atuganile alinambia kuwa wapo Mlandizi. Hapo nikajaribu tena kupiga namba ya Atuganile haikupatikana tena. Moyo ulibadili mapigo na wasiwasi kunivaa. Nilielekea hadi zilikopaki basi husika za Saibaba na kuiulizia basi iliyotoka Mbeya. Nilikuta ikiwa inamaliziwa kuoshwa. Hakuna hata dalili za Atuganile wala harufu yake. Nilishusha pumzi na kuanza kupwiyanga kituo kizima nikizunguka na kumtafuta Atu wangu hususani kwenye maeneo waliokaa wasafiri waliokuwa wanasubiri ndugu zao na pia kwenye maeneo waliokuwa wanalala wasafiri na kadhalika. Kote sikufanikiwa kumuona Atuganile. Mawazo yakaanza kwenda mbali lakini kuna tumaini jipya likaja akilini mwangu.
"Atakuwa amenitafuta, amenikosa na kuelekea nyumbani mwenyewe, si anapajua kwa mama bwana itakuwa kaenda huko. Atu ni msomi mke wangu ana akili ya kujiongeza." nilijifariji na kutoka nje ya kituo. Nilipanda daladala na nilipokuwa njiani nilimpigia tena Atuganile, ilikuwa tayari saa tano usiku. Mara simu yake safari hii iliita lakini haikupkelewa hadi ikakata. Nilihema na kuhisi kijasho chembamba kikianza kunivuja kwa shauku ya wivu wa kujua wapi alipo mke wangu mtarajiwa. Nilipiga tena ikakatwa. Nikapiga ikakatwa tena.
Nikiwa nimekodoa huku nikihisi naelekea kudata kwa maswali ndipo simu yangu iliingia ujumbe kutoka kwa mchumbaangu. Haraka niliufungua na kuusoma.
"Mume wangu nimekusubiria na kukutafuta sijakuona ila kwenye basi pia nilikuwa na mamaangu mdogo ndio akaniomba twende nikamsalimu bibi sijamuona miaka mingi, ikabidi niongozane naye sasa hivi nipo huku kwa bibi temeke. Kesho asubuhi nitakutafuta mume wangu unielekeze nije kwetu. Samahani sana baby I love you so much more than love my everything Mmmwaaaah."
Niliusoma na kuurudiarudia ujumbe huo zaidi ya mara tatu. Nilishusha pumzi na kushukuru kama yuko salama Atu wangu. Lakini nilifikiria na kujiuliza mbona Atuganile hakuwahi kunambia kama kuna bibi yetu hapa Dar? Nilijiuliza na kulipotezea swali hilo nikiamini huenda alipitiwa tu na kwakuwa masaa hayagandi basi kesho yake atanijuza mengi.
Na kweli kesho yake tuliwasiliana na Atu na kunambia kitu kipya kilichoniumiza kidogo ingwa nilishindwa kumkatalia.
"baby nakuomba univumilie leo tu! jana tulifika usiku bibi alilala hivyo ameniomba basi nishinde leo tuzungumze vizuri nakuahidi kesho mapema nitakuja mume wangu. Lakini kama utaona si vyema mi nakusikiliza wewe tu my everything siwezi kupinga."
Nilimkubalia Atuganile ombi lake kwa sauti ya kawaida tu isiyoonesha kukwazika ingawa ukweli baada ya kukata simu nilimlaumu sana huyo bibi yake. Kipindi nikiwa mawazoni simu iliita tena nilipoangalia alikuwa Atuganile.
"Baby naomba ongea na mamaangu mdogo mtoto wa bibi niliyekuwa naye jana."
alinambia na kumkubalia huku nikiiandaa sauti yangu ya ucheshi ingawa moyoni nilikuwa na maumivu ya kucheleweshewa Atu wangu. Tuliongea ingawa kwa muda mfupi na mama mdogo ambaye alionesha kufurahi sana kunijua. Baada ya kumaliza naye simu alirudishiwa tena Atu aliyeniaga kwa kunichumu huku akinambia
"Nikijaaaa kesho uniandalie juice ya parachichiie eeeeh"
nilicheka na kidogo nilihisi amani moyoni mwangu. Nikawa na hakika kweli Atu yuko kwa bibi yake na yule niliyeongea naye pale alikuwa ni mamaake mdogo ingawa wote sikuwahi kuwajua kwa sura.
Saa zilisogea, jua likazama na usiku ukaingia. Siku hiyo baada ya kufunga ofisi nilikuwa natazama mpira na marafiki bandani. Baada ya mechi kuisha tuliweka kijiwe tukipiga stori nyingi tofauti za kimpira lakini katika maongezi maongezi sijui ilikuwaje tukajikuta tumehamia kwenye wanawake.
"Unajua wanawake noma sana mwanangu! unaweza kuzungumza nae ukajiona uko peke yako lakini kumbe wenzako nao wanachachua kama kawa.."
"Ooohooo mi nawaambiaga hawa Fredi mwanamke si mtu wa kumuamini kivileee au hamjasoma stori ya mtoto wa Becker ile jinsi Zai alivyoleta mtifuano?"
"Juma nawe achana na mambo ya stori, Mtoto wa Beka mwenyewe boya tu usikute ya kwake yanamshinda."
"Hta kama Mavugo, lakini mimi nitabaki naamini wanawake ni viumbe dhaifu na ndio wanaotubadilisha kitabia wanaume au unaonaje One?"
"Mh!" niliguna baada ya kuulizwa swali hilo pasipo kuongeza kitu kwenye maongezi ya washkaji.
"Ndio hivyo mwanangu! wanawake hatari babu. Tena wa mijini ndio kabisaaa. kwanza jiulize huyu mwanamke kila siku anaweza kutongozwa na watu zaidi ya watatu. Mara mwezi je, wangapi?"
"Tisini hao babu a ha ha haaa"
"Sasa piga hesabu mara mwaka!"
"Duh! noma sana."
"Utataka kunambia huyo demu wako uliye naye mwaka wa tatu sasa ametongozwa na vidume wangapi kwa muda wote huo? na je wote amewaambia NO?"
"Ha ha ha haaa daah! mwanangu ukiyafikiria hayo utapasuka kichwa bure."
"Ndio hivyo. Mpende ndio lakini sio umuamini kama amekuzaa utakuja kujitia kitanzi siku utapoyaona makucha yake. Leo unaweza wasiliana naye akakwambia nipo kwa shangazi kumbe wenzako wanakamua. Akija kwako bebiii oooh i love you wizi mtupu."
"ha ha ha haa daa Fredi bwana. sema kweli eeh"
"Ndio hivyo ndo maana mwenzako moyo wangu upo kwaajili ya kusukuma damu. Ila kumuweka mwanamke kamwe haitatokea nisije kufa na kihoro. Tatizo hawaridhiki wala hawathamini nyeti zao wanawake wa siku hizi."
"Daah! ila hata wanaume nao muda mwengine tumezidi ujue wanaume wengi hawatosheki na mwanamke mmoja utakuta lazima umtamani mwengine na wazuri hawaishi. Lakini mi naamini wanawake watulivu wapo wengi tu ila wanaume wenyewe ndio wanawabadilisha."
"Daaah! wee One mwanangu ndio hujui kitu kabisa na hiyo imani ukizidi kuifuga utakuja kufa kwa sababu ya wanawake."
"Sio hivyo Fredi tatizo nyinyi mnaangalia upande mmoja tu kuwasema wanawake halafu hamtazami upande wa pili wa shilingi. Kweli nyani haoni kundule. Mi naamini sisi wenyewe ndio tunawafanya wanawake wasitulie. Unakuta mwanamke anakupenda lakini hujali upendo wake. Unatongoza wengine, hutimizi ahadi! hivi unadhani mwanamke ataendelea kukuvumilia tu? acheni lawama wanangu kama mkitulia siku moja mtapata wanawake wa ukweli kama demu wangu." Nilikanda na kujifagilia.
"Ha ha ha ha haaaa One mwanangu wee kweli bado huwajui wanawake. Ukitaka kujua mwanamke ni kiumbe dhaifu zaidi na ni msaliti angalia hata katika historia upande wa imani hivi ushasikia wapi alikuwepo nabii ama mtume wa kike aliyetumwa na Mungu?"
"Mh! tusiende huko sasa."
"Ndio hivyo wewe tena hata nikikuuliza swali huyo demu wako unayetutambia sasa hivi usikute wanatindua wenzako huko alipo wewe unabaki kudanganywa tu."
Mashambulizi waliyageuza kwangu tena na kuniona imani yangu imepotoka. Ilibidi niachane na washkaji na kurudi zangu geto huku wakiwa wamekitibua kichwa changu na kuanza mfikiria Atuganile nikichanganya na maneno yao nilijikuta usingizi ukinipitia katikati ya mawazo mazito.
"Karibu sana baby wangu hapa ndipo ninapoishi mamaa" Nilimkumbatia Atuganile baada ya kufika asubuhi na mapema na kumuingiza chumbani. Kila nilivyomtazama nilimuona wazi ameongezeka uzuri. Umbo lake sasa lilitanuka tofauti na awali.
"Baby, kwa sasa nadhani ni muda muafaka kulila tunda kwa mara ya kwanza mke wangu ushatoka kwenye usekoseko sasa unaingia kuwa mwanachuo. Nipe baby wangu Atu." Kwa sauti ya huba nilibembeleza mara baada ya kucheza cheza na Atu kitandani na kuanza kumchojoa nguo moja baada ya nyengine.
"Lakini baby nakupa leo kwa mara ya kwanza ila usiniache jamani nakupenda."
"Siwezi kukuacha mke wangu hakika wewe ni tunu niliyoshushiwa." Niliendelea kumchombeza huku mate ya uchu yakinidondoka. Nilimrambaramba na kulibusu kufuli lake kabla ya kumchojoa na kumuacha utupu huku yeye akijiziba uso kwa mikono kama siku ile ya kwanza nilipomvua nguo.
Lakini safari hii nilipokutana na taswira ya utupu wa Atu tu niliiona tofauti kubwa na mara ya kwanza siku ile. Kwanza weusi ulizidi tofauti na mwanzo, pili ulikuwa umefunguka kwa juu tofauti na mwanzo ulikuwa umefumba, tatu kuna kaharufu kalisikika nilipousogelea tofauti na siku ile. Moyo ulianza kwenda mbio lakini nilipotezea hilo kiugumu na hapo bila kumchelewesha nilijiweka sawa kupeleka mashine. Ajabu safari hii hakuruka, hakulia, wala mashine haikugoma zaidi ya kuzama yote moja kwa moja na kunifanya nichomoe huku nikiwa nimebadilika hadi rangi kwa hasira na taharuki nikafoka..
"ATUGANILEEE! IKO WAPI ZAWADI YA NDOA ULIYOAHIDI KUITUNZAA"
Moyo uliniuma na kujikuta nikianza kulia kwa kwikwi huku nikiwa na uhakika kuwa tayari Atu amenisaliti na si mara moja wala si kwa mtu mmoja kwa hali halisi niliyoikuta. Moyo uliuma zaidi na zaidi nikiwa najiuliza nimfanyeje lakini ajabu nyengine yeye hakuonesha wasi zaidi ya kuanza kuvaa nguo zake.
"Kama hunitaki usinipotezee muda, wala nisikupoteze muda niache niondoke.." Aliongea kwa kebehi.
"Atuganileeeeee!? .." Nililia zaidi na zaidi huku akili yangu ikiwaza kumfanyia kitu kibaya Atu kwa usaliti wake wa dhahiri na kunikosea heshima. Papo hapo nikachukua kisu kilichokuwa pembeni ya meza mue chumbani na kumsogelea kabla hajafungua mlango wa kutokea.
"Aaaaarrrrhhhggg nakufaaaaa" alitoa yowe Atuganile pindi alipogeuka na kukiona kisu mkononi mwangu huku nikiwa nimebadilika sasa hadi rangi ya ngozi kwa hasira. Mwanaume nikaiva haswa.
"Kuuufaaa shetani ATUGANILEEEEE"
AAAAAAAAAAAAH!! Nilistuka usingizini. Lool! kumbe yote hayo yalikuwa ndoto. Asubuhi ya kweli sasa ndio ilitimu. Nilikurupuka na kukaa kitandani. Jasho lililokuwa linanivuja ilikuwa si masihara. Moyo ulikuwa kasi sana huku nikihema kwa shida.
"Atuganile?" nilijisemea mwenyewe na kujifuta machozi ambayo kweli yalinitok pindi nilipokuwa naota ndoto ile ya ajabu kuhusu Atuganile. Nikachukua simu yangu iliyokuwa pembeni ya kitanda na kuitazama kwa muda huku nikifikiria jambo. Ilikuwa tayari saa kumi na mbili na nusu asubuhi.
"Akiniletea sababu leo lazima niende mimi huko Temeke nikamuone huyo mama na bibi yake isije kuwa nachezewa mchezo." Nilijisemea huku nikishuka kwenye majina ya simu mpaka jina 'My Lovely Wife' huyo alikuwa Atuganile, lakini kabla sijampigia simu yangu ilivibrate na kuita. Kutazama mpigaji likatoka jina lile lile.
'Paaagh! Atuganile!' Moyo ulipasuka na kuipokea simu huku nikibana pumzi zangu ambazo hadi muda huo zilikuwa hazijakaa sawa kwa ndoto ya ajabu na ya kushtusha kiasi kile.
 
SEHEMU YA 12

Sauti tamu iliyoshiba furaha niliisikia upande wa pili.
"Baby nishajiandaa tayari mume wangu nielekeze sasa." Alikuwa ni Atuganile na ikabidi nijichangamshe kiulazima ili asigundue hali niliyokuwa nayo. Nilimuelekeza kuwa achukuwe taxi na ampe simu dereva nimpe maelekezo vizuri. Na kweli alifanya hivyo huku nikiamka na kujiandaa kwaajili ya kumpokea mchumbaangu Atu.
Lisaa limoja na nusu mbele Atuganile alifika. Nilikuwa nimejongea karibu na barabara kwenye duka la mpemba kutokana na nilipopanga wakati huo gari haikuweza kufika. Macho yangu yalikutana tena na Atu wangu kwa mara nyengine baada ya muda kupita. Moyo ulilipuka kwa furaha iliyokuwa inakinzana na kichwa kilichobeba maswali mengi ya dukuduku juu ya ndoto niliyoota.
Alinikumbatia kwa nguvu Atu huku akinibusu hadharani kwa furaha. Watu walinishangaa kama kawaida ya watu wa uswahilini, pasipo kupoteza muda nililipia Taxi na kumchukua Atu wangu moja kwa moja mpaka magetoni.
Nilijitahidi sana kuficha dukuduku langu siku hiyo. Muda wote Atu alikuwa mwenye furaha na alikuwa amenibebea zawadi mbalimbali zikiwemo kadi za upendo. Kichwani mwangu siku hiyo niliapa lazima nifanye naye mapenzi Atu kwa mara ya kwanza. Nilikuwa na kila sababu. Sikuwa tayari kuendelea kusubiri siku ya ndoa nisije uziwa mbuzi kwenye gunia. Nilifikiria kuwa huenda nishasalitiwa kweli kama nilivyoota japo upande mmoja wa moyo ulikataa.
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale huku tukichezacheza kitandani mara mvua ilianza kunyesha huku kibaridi cha feni kikizidi kuchombeza hisia za kufanya michezo ya kikubwa.
"Baby, kwa sasa nadhani ni muda muafaka kulila tunda kwa mara ya kwanza mke wangu ushatoka kwenye usekoseko sasa unaingia kuwa mwanachuo. Nipe baby wangu Atu." Kwa sauti ya huba nilibembeleza mara baada ya kucheza cheza na Atu kitandani na kuanza kumchojoa nguo moja baada ya nyengine.
"Lakini baby nakupa leo kwa mara ya kwanza ila usiniache jamani nakupenda."
"Siwezi kukuacha mke wangu hakika wewe ni tunu niliyoshushiwa." Niliendelea kumchombeza huku mate ya uchu yakinidondoka. Nilimrambaramba na kulibusu kufuli lake kabla ya kumchojoa na kumuacha utupu huku yeye akijiziba uso kwa mikono kama siku ile ya kwanza nilipomvua nguo.
Akili ilistuka na kumbukumbu ya ndoto kunivaa. Nikashangaa kuona maongezi yanafanana kama ya kwenye ndoto hata rangi ya kufuri yenyewe ileile kama ya kwenye ndoto achilia mbali mkao niliomuweka na ule upande aliogeukia.
"No! Atu hivi kweli wewe ni bikra bado?" Nilimuuliza huku nikijikuta naishiwa nguvu ya kumchojoa zaidi nguo yake ya ndani nikihofu kisitokee kile kilichotokea ndotoni.
"One baby? mbona hivyo jamani mume wangu ina maana ushanihisi vibaya kichwani mwako?" alishtuka na kurudi nyuma Atu huku akibana miguu.
"Sijawahi kukudanganya One wangu wala siwezi kuutoa mwili wangu kwa mwanaume mwengine wakati tayari upo mtu sahihi tena uliyejitoa hadi kunisomesha? hapana baby daaa siamini..." aliongea huku akilia sasa.
Nilijikuta nakuwa mpole tena na kumuomba radhi huku nikijilaumu kuiendekeza ndoto.
"Hawezi kunidanganya Atuganile wakati amekubali tufanye mapenzi." Moyo ulinambia nafsi ikakubali huku akili ikitupilia mbali fikra za ndotoni.
Nilibembeleza hadi nikamuweka sawa kwa mara nyengine Atuganile.
"One baby wangu nasikia inauma sana siku ya kwanza naogopa baby." aliitoa sauti puani kipindi sasa kidume nilikuwa tayari kula tunda nililolisubiri kwa muda mrefu. Kwa hamu ya huba kidonda cha mahaba hatimaye nilimuweka bayana Atuganile halisia.
Nilimbusu kwanza, hakuwa kama nilivyomuona ndotoni ingawa hakuwa kama nilivyomuona kipindi kile ugonjwani.
Niliachana naye na kumbusu mashavuni Atu huku nikimnyonya na kumtomasa matiti. Akili zangu zilikuwa sawa sikuwa na haraka ya kumdunga sindano kabla ya kumuandaa. Nilihakikisha namtomasa kumtoa kwenye ulimwengu wa raha na kumeleta kwenye dimbwi la utamu. Nilipeleka mkono bondeni ili nizidi kumsolola bi mwali lakini alibana miguu na kunizuia.
Kila nilivyojitahidi haikuwa rahisi. Alinizuia na kunikumbatia tu.
Nilikumbuka kuwa mwanamwali kumtoa uwali inahitaji hali y nguvu na ujasiri.
Hapo ndipo nilipojiandaa zaidi na nilipoona kalegea na kumuweka upande wa 'v' nikaupeleka mkuki kunako kwa ustadi.
"Aaaaaaaahhhhh Ooooonee!"
Alitoa ukelele Atu huku akinisukuma kwa nguvu kipindi nimembana na kupiga kasia mbili tu lakini alifanikiwa kujichomoa. Alijikunja pembeni ya kitanda na kuanza kulia wakati huo nilijikuta nikimaliza haja nje ya mlango. Nilipojicheki ulungwana una vidamu damu.
"Ooooh waaoo!" Nilitabasamu na kujipongeza moyoni. Nilijiona kidume na kufutilia mbali hisia za ndoto ya ushetani na maneno ya washkaji. Nilimsogelea Atu na kumkumbata huku nikimfariji.
"Usilie baby ndio ukubwa huo mke wangu."
"One inauma sana aaah! nimevunja ahadi ya mama kwa kukuamini One wangu wewe ndiye mume wangu."
"Ni kweli Atu nakuapia mbele za Mungu kamwe hautajuta kuwa nami."
Huo ndio ukawa mwanzo mpya wa imani ya juu kabisa kuhusu mapenzi yangu kwa Atu. Kunisubiria miaka yote bila kuguswa hadi mimi? Hakika nilimuona zaidi ya shujaa wa kukwepa vikwazo vya wanaume. Niliamini sasa hawezi tena kumtamani mwanaume mwengine yeyote zaidi yangu.
"Mwanamke ukimtoa bikra hawezi kukuacha."
Moyo ulinambia na hayo maneno niliyasikia tokea shule kuwa mwanamke atawaacha mabwana wote lakini si yule aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa huba na mahaba.
Tulilala siku hiyo huku siku ya pili nikimpeleka Atu kwa mama. Walifurahi sana na kama kawaida haklukuwa na dosari yoyote kitabia kwa Atuganile. Alizidi kuwa mtamu. Heshima ya mwana wa kale. Akikupa hata maji lazima akupigie goti. Mavazi yake ya heshima yalificha maumbo yake nyeti.
Alikaa kwetu wiki moja kabla ya kwenda tena kwao Mbeya. Yote ilichagizwa na hamu ya kuwa na mama akinambia kuwa muda si mrefu ataenda kuolewa nami hivyo ni vyema kwa nyakati hizi azitumie kuwa jilani na mamaye ambaye atammiss kwa muda mrefu pindi atapokuwa kwenye majukumu ya kifamilia kwetu.
"Baby mimi ni wa huku, naomba uniruhusu tu niende tena nyumbani kabla yamatokeo kutoka mume wangu si unajua ndio watanifaidi kuniona mara ya mwisho mwisho kabla sijawa mke rasmi.!"
Huku akinichezea kidevu alinidekea siku akiniomba ruhusa Atu ambayo sikuthubutu kumpinga wala kumnyima. Hakika nilimuamini sana.
Siku zilisonga hatimaye majibu ya mtihani wa kidato cha sita yalitoka. Kwa shauku na hamu ya kujua mke wangu amepangiwa chuo cha wapi lakini katika ajabu na kushangaza Atuganile alifeli kabisa. Tena alipata daraja la mwisho. Daaah hii ilishangaza na kustusha kwa binti mpenda shule tena mwenye ndoto ya kuwa daktari huku akifanya vizuri kwenye masomo lakini anafeli vibaya kwenye mitihani?
 
SEHEMU YA 13

Kila mmoja aliyapokea matokeo ya Atuganile kwa masikitiko makubwa. Nilipigiwa simu na mama mkwe mtarajiwa kunijuza juu ya kupoteza fahamu kwa Atuganile pindi majibu yalipotoka. Niliumia sana na hatukuwa na budi zaidi ya kumfariji Atu.
"Mume wangu nisamehe sana nimekuangusha ingawa ulijitoa kunisomesha lakini ukweli napenda sana kusoma, natamani kutimiza ndoto yangu!" alinambia siku moja baada ya kupata fahamu pindi tulipowasiliana.
"Usijali Atu wala usiumie kihivyo. Kuanguka si kushindwa kutimiza lengo, bali kushindwa kutimiza lengo ni kukata tamaa ya kusimama na kuendelea kufukuzia lengo. Nakuahidi nitakuendeleza mpaka utimize ndoto zako." Nilimwambia kwa njia ya simu na kumpa moyo Atuganile.
Kilichofatia nyumbani baada ya kuzungumza na ndugu zangu juu ya mchumbaangu tulikubaliana sasa kabla hajaendelea elimu ya chuo cha kulipia itabidi tufunge ndoa kabisa.
"Mwanangu unaona kiasi gani pesa zilizopoteana pia kwa sasa binti ameshakuwa zaidi ya mwanzo na watu hukua na kubadilika. Nitakuwa na amani mama yako kama utamuoa kabisa Atu ndipo uendelee na kumsomesha baba usije someshea wenzako kwa sasa."
Hayo yalikuwa mawazo ya mama na tuliyakubali thabiti. Niliwasiliana na Atu hata yeye pia alikubali tufunge ndoa kabisa na kwakuwa ataenda chuo moja kwa moja ingawa si kwa kutumia matokeo yake ya kidato cha sita bali yale ya kidato cha nne.
Sikuumiza na pesa zilizopotea ndani ya miaka miwili nikiamini kuna makubwa pia amejifunza mke wangu kwenye masomo yake mbali na kufeli.
Kwao hakukuwa na kikwazo chochote zaidi ya kukubaliana nasi kwani tayari tulishajitambulisha na kutoa vianzio vya kimila na desturi miaka miwili nyuma. Wote walifahamu kuwa Atu ni mchumba wa mtu na sasa mwenyewe anataka amuoe kabisa na atamuendeleza masomo ya chuo wakiwa wanaishi pamoja.
Walikubaliana nasi na tukapanga tarehe na mwezi wa kwenda kuoa ambapo tulikubaliana harusi kufanyika mkoani Iringa kwa babaake mdogo aliyehamisha makazi huko.
Hapo ndipo taratibu rasmi za mipango ya ndoa zikaanza. Ndoa ya matumaini na faraja. Siku zote nilikuwa naitamani siku hii ifike. Hakika moyoni mwangu nilifurahi mno kuona sasa ile ndoto ya muda mrefu juu ya kumuoa Atuganile inaenda kutimia.
Kadi za ndoa na michango zilisambazwa kila kona kwa watu tuliofahamiana, ndugu na marafiki. Si kwa upande wangu tu, bali hata kwa upande wa Atuganile.
Siku zilienda na hatimaye siku ya siku ilifika katika kanisa kuu la Anglikana Iringa Ndoa yetu na Atuganile ilifungwa. Kutoka jijini Dar tulikodi coaster na gari nyengine ndogo kwaajili ya maharusi. Kitu kikubwa kwa kweli zaidi ya asilimia sabini ya harusi ilitokana na pesa zangu mwenyewe. Michango kutoka kwa ndugu ilikuwa michache mno. Labda kutokana sikuwa na ndugu wa kutosha walio karibu nasi ama wenye mioyo ya utoaji. Pia umasikini nao ulichangia kwa namna moja. Lakini pia katika harakati za ndoa nilijikuta natumia msingi mzima wa duka la nguo ili kufanikisha ndoa yangu ambayo niliiona ni muhimu kufanyika kuliko kitu chochote. Hakika sikuiona walau theluthi ama chembe ya hasara ya kumuoa Atuganile. Ukiachilia mbali gharama ya mahali na usafiri, pesa iliyotumika kwaajili ya ndoa yangu ni zaidi ya milioni mbili.
Tulifungishwa Ndoa salama na kwakweli katika siku ambayo Atuganile alipendeza basi ilikuwa siku hiyo. Tuliweka viapo mbele ya kanisa na kuunganishwa kuwa mwili mmoja. Tukiapa kuvumiliana katika hali zote. Shida na raha, uzima na maradhi mpaka pale kifo kitapokuja kututenganisha.
Hapo ikawa rasmi historia ikaandikwa na pete zikatuama vidoleni. Vigelegele na shangwe zilisikika na nyimbo tukaimbiwa. Atuganile sasa akawa wangu rasmi. Mrs Onesmo. Niljisikia fahari na furaha isiyo kifani. Ingawa katika harusi yangu hiyo niliumia kwa namna moja kutohudhuriwa kwa rafiki yangu kipenzi wa zamani Sultani Rwambo ama Sulu. Lakini nilijifariji na kupotezea kwa kuwa sikuwa na mwasiliano naye tena ya karibu tokea tulipokwazana na kutupiana maneno siku za nyuma.
Tulikaa siku moja baada ya ndoa na mapema msafara uligeuza kesho yake kumalizia sherehe tulizoziandaa jijini Dar. Tulikodi ukumbi na ukapambwa ukapambika. Picha zilichukuliwa za video na kawaida. Watu walijaa na kupendeza sana. hakika harusi yetu ilihudhuriwa na watu wengi hata sikutarajia. Ilifana kana kwamba aliyeoa alikuwa mtoto wa bosi. Mungu ndiye mkuu wa kushukuriwa kila kitu kilienda salama na wazazi walituusia mengi juu ya maisha ya ndoa. Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia mama Atuganile akitukumbatia na kudondosha machozi mbele yetu. Atuganile naye alilia pia. Ilionesha jinsi gani wapendanao mama na mwana leo wanaachanishwa kwa mtindo ule. Utoto sasa uliisha Atauganile amekuwa Mrs One.
Baada ya kumaliza sherehe za Dar kilichofata ni kumaliza mambo ya desturi za kwetu hususani zile siku saba ambapo bibi alihusika kumuogesha mke wangu na kumfunza mambo kadha wa kadha hususani tamaduni za kwetu.
Hayo yalitimia na siku saba zikapita. Bibi alirejea kwake nasi tukabaki na maisha yetu. Huo ndio ukawa mwanzo rasmi wa maisha ya Ndoa Yangu.
Kuanzia hapa sasa ndipo penye kila kitu kilichopelekea maisha yangu kugeuka na kuwa simulizi yenye kuchoma na kuumiza.
Hakika sikuoa ili nijichimbie shimo la maumivu na mateso la hasha, bali nilioa ili niipate faraja. Sikufanya ubaya wala kumtenda mtu dhambi. Lakini iweje wanitoe machozi? aaaaaaah! Atuganileeeeee! Sikujua kama utakuwa chanzo la chozi langu lililobeba maumivu ya moyo na mateso ya mwili. Kwa sababu ya Ndoa yangu..........! bado naamini kwamba chozi langu...litalipwa.
 
SEHEMU YA 14

Maisha yalianza kuwa mazuri na ya amani ndani ya ndoa. Siku zote nilifanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha kila kitu kinaenda sawia ndani hususani kula, mavazi, furaha na amani. Kwa kuwa kipindi namuoa Atuganile ilikuwa katikati ya mwaka. Mwezi wa sita, hivyo ahadi ya chuo ilikuwa palepale lakini tulikubaliana tusubiri mpaka mwezi wa tisa. Hilo lilinikaa akilini siku zote. Kumbuka kwa kipindi hiko nilikuwa nategemea zaidi biashara ya 'game' kwa kuwa tayari nilifilisika mtaji wa duka la nguo baada ya kutumia pesa zake za msingi katika shughuli za ndoa na mwishowe nikashindwa kulipia flemu na kuagiza mzigo mpya.
Kwenye nyumba niliyokuwa nimepanga pia alipanga dada mmoja ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa dadaangu. Urafiki wao ulinifanya nizoeane naye na kumuona sawa kabisa na dadaangu. Aliniita kaka nami nilimwita dada.
Tokea awali kabla hata sijaoa ukweli sikuwa na mazoea sana na wanawake. Maneno ya washkaji zangu mbalimbali kuhusu wanawake yalinikwaza muda mwengine moyoni na kutokubaliana nao ingawa muda mwengine nilihisi yakiniingia akilini lakini bado niliamini si kila mwanamke atakuwa na tabia kama walizokuwa wanaamini rafiki zangu. Pia kwa upande wa mke wangu Atuganile tabia zake zilikuwa nzuri na zenye utofauti mkubwa sana na mabinti wengi wa mijini. Hivyo baada ya kumuoa nilihakikisha kila siku, kila mara nikimsihi na kumkumbusha kutopenda kujenga mazoea na watu ovyo hususani wanaume na hata kuwa na lundo la marafiki. Nilijua mtaa mzima baada ya kujua nimeoa wanaweza kunifanyia hila juu ya mke wangu ili nami niwe miongoni mwa walioumia kwenye mapenzi. Ingawa nilimuamini sana Atuganile lakini sikuchoka kumuelewesha juu ya hadhari hizo.
"Atu mke wangu, hapa Dar ni tofauti sana na mikoani. Watu wa aina zote wako hapa. mashetani na mafedhuli waso haya. Si wakubwa si wadogo. Unaweza kuwaona machoni wastaarabu lakini mioyoni ni washenzi. Chunga sana mke wangu kujenga mazoea nao. Umemuona huyu mama mwenye nyumba nzuri jilani yetu!"
"Ndio mume wangu sijui wanamwita mama Poa?"
"Ndiye, huyo mama anajiuza kwenye mahoteli huko. Ni mshenzi tu. Pia pale ukienda dukani usipende kuzoeana na wale wauzaji wa pale ni washenzi tena wengine wana ushirikina. Ukiwapa mkono wakakushika kiganja unaweza kujikuta unajikanyaga ukatenda dhambi. Pia hata hawa madada madada usipende kuzoeana nao kabisa. Kama mtu akikuomba kwenda popote sijui umsindikize sokoni ama wapi! mwambie wewe ni mke wa mtu hivyo kama anakuhitaji aje aniombe mimi. Usicheke nao ovyo wala usiwaoneshe hasira baby."
"Sawa mume wangu nimekuelewa!" Ndivyo alivyokuwa ananijibu mke wangu kila nimueleweshapo jambo la msingi. Hakuwa mkaidi kwa maneno wala msemaji.
Nilijivunia nikiamini ananisikia vizuri.
Mtu pekee niliyemuamini na kumpa uhuru alikuwa ni Mwajuma. Yule dadaangu wa hiyari rafiki wa dadaangu mkubwa ambaye alikuwa mpangaji mwenzangu pale. Niliamini Mwajuma atakuwa mwalimu mzuri juu ya Atuganile. Nakumbuka hata kabla sijamuoa Atu niliwahi kumtambulisha siku za nyuma na ndiye aliyekuwa amemzoea zaidi kuliko mtu yeyote pale mtaani.
Uzuri wa Atuganile niliamini unawachanganya wengi mitaani kila apitapo na kitu chengine nilichokuwa nahakikisha sifanyi makosa ni mavazi.
Nilihakikisha mke wangu anavaa mavazi sahihi ambayo hayachoreshi mwili wake wala hayamuaniki maungo yake nyeti ili kumpunguzia adha ya vishawishi vya wakwale waliotapakaa kila pembe ya jiji hili lililosheheni wanaume wakosa haya na wanawake waso haiba.
Mwezi mmoja ulikatika baada ya ndoa. Ila kitu kimoja kilichoanza kunishangaza ingawa hakijanistua ni kuhusu mke wangu kutopenda tufanye mapenzi. Yaani tendo la ndoa lilikuwa gumu sana kwa upande wake. Ukitaka aanze kukosa furaha ya kweli basi pale nilipokuwa nataka mchezo wa haki yangu wakati wa usiku.
"Baby, sijui kwanini nakuwa hivi, sijazoea kabisa kufanya mapenzi mume wangu wala sioni raha yake. Naomba hata tuwe tunafanya mara moja kwa wiki baby. Pia nasikia tukifanya mara kwa mara utanichoka mapemaaa. nakupenda sana mume wangu." Alinambia Atu maneno hayo mara kwa mara.
Nilijitahidi kuhakikisha namuandaa vya kutosha sana kabla sijamkwea. Nia yangu nimuweke sawa kisaikolojia ili naye afurahie tendo kama mimi lakini hisia zake zilikuwa za muda mfupi sana. Sikuweza kujua kwanini mke wangu alikuwa vile. Niliwahi mshauri hata kwenda hospitali lakini hakutaka katakata. Na kwakuwa nilikuwa sipendi kumuudhi basi sikuwa namlazimisha zaidi ya kufanya pale anapohitaji pasipo kumuhisi vibaya zaidi.
Mwenyezi Mungu ni mwingi wa hekma na mitihani anatupa viumbe atupendao ili tuzidi kuwa jirani naye. Ikiwa ni mwanzoni mwa mwezi wa pili wa Ndoa yangu ikiwa ni mwezi wa nane lilitokea tatizo la mgao wa umeme. Biashara yangu ilikuwa inategemea zaidi umeme na sikuwa na jenereta. Tatizo hili lilizidisha ukata wa maisha na ukizingatia tarehe ya kodi ya nyumba ilifika sambamba na kule kwenye frem ya 'play station game' pia ilikaribia kwisha kodi.
"Tutafanyaje mume wangu na hali hii?" lilikuwa swali la Atuganile usiku mmoja baada ya umeme kupitiliza siku mbili na kushindwa kuingiza pesa.
"Usijali mke wangu wala usiogope." Nilimfariji huku moyoni nikiwa sijafa tumaini.
"Hivi nitasoma kweli baby maana mwezi wa tisa huo unakaribia." aliongea Atuganile kwa sauti ya kukata tamaa.
"Kwanini usisome mamyto. Utasoma tu kwa jina la bwana kila kitu kitakuwa. Hii ni mitihani midogo tu. leo tunakula ugali kachumbali mama ila kumbuka jana tulikula kuku basi kesho tutakula bata." Nilimchekesha huku nikimpelekea tonge la ugali lenye kachumbari juu. Ukweli siku hiyo hata mboga tulikosa na ndani hatukuwa na akiba. Yaani kesho yake tulikuwa tunaamka watupu kabisa. Lakini siku zote nilifunzwa kumtumaini Mungu juu ya mgawanyiko wa riziki. Pia mazingira magumu nilishayazoea na ndiyo yaliyonilea, hivyo niliamini hata Atuganile haitakuwa shida kwa mazingira yale. Awali nilishakubaliana na moyo wangu kama mazingira ya maisha yatabadilika kama ilivyotokea leo pia haitoleta tabu kwa Atu kwa kuwa hata kwao hali ilikuwapo. Tena afadhali ya pale anakula ugali huku anatazama video tena 'flat screen' anasikiliza mziki mkubwa ingawa sabufa, anatazama filamu azitakazo huku anapepewa na feni, kitanda kizuri, masofa mazuri.
Lakini kabla ya hapo alikulia kwao ambako alikula ugali na mboga ya majani yasiyoungwa, tena akitazama kibatari na kukikinga na upepo kisizimike, nyumba ya nyasi, kitanda cha kamba, jiko la ndani moshi kibao wa kuni! sembuse maisha ya sasa tena yupo na mtu mwenye kumpenda na kumjali kama mimi? Hakika hilo halikunipa wasi ingawa sikupenda kuona mke wangu anapata shida.
Usiku huo tulilala hivyo na kesho yake asubuhi na mapema nilitoka nikiwa nimeshika mkononi kichezesheo cha game ama kwa jina maarufu 'pad'.
Umeme ulikuwa bado tatizo. Nilitembea kwa miguu zaidi ya kilometa tano mpaka kwa mshkaji wangu mmoja ambaye naye alikuwa anachezesha 'game'. Yeye aliwahi nipigia siku za nyuma kuwa padi zake zimekufa hivyo alihitaji walau padi mbili ama moja ya kununua kama ninazo lakini nilishindwa kumuuzia kipindi hiko. Ila kwa sasa nilibanwa ilibidi nimfate asubuhi subuhi.
"Niaje man."
"Poa One nambie!"
"Fresh, sasa jembe kuna pad hii hapa ya mtumba yenyewe kutoka zenji kama vipi nifanyie madusko nikuachie jooh!"
"Daah! mwanangu.. mi nilishanunua ila kuna mwana naye kafungua game mtaa wa kati labda umsikilizie mida mida akifungua umpelekee. Yeye anatumia jenereta anatupiga bao sana."
"Daah! anafungua mida gani?"
"Kama saa sita sita hivi."
"Mh! sasa mwanangu huna hata la teni ama buku tano uniazime mara moja nakuachia mzigo baadae nitakuja man tumalizane na mshikaji nitakurudishia!"
"Mh! One mwanangu siko vizuri jeshi."
"Daah nifanyie hivyo kaka, niko ovyo shemeji yako nimemuacha mkavu boy"
"Kweli One ningekupa hata kama si kukukopa ila niko vibaya inabidi nilipe hela ya mchezo leo."
"Daah! mwanangu nisaidie basi hata buku mbili nikamuachie ya chai tu shemejio nistiri kaka."
Nilibembeleza nikitamani hata kupiga magoti lakini ukweli hata jamaa nikabaini kuwa hana ingawa moyo mwengine ulihisi kama ananifanyia kusudi.
Nilimuaga na kumuahidi nitarudi baadae. Sikutaka kusubiri zaidi ya kuzunguka mitaani nikijaribu kuiuza ile pad moja hata kwa bei ya hasara ili kwanza nikamtulize 'wife' nyumbani ndipo nianze michakato mengineyo. Lakini hadi inatimu saa tano nilijikuta miguu imekuwa meupe kwa vumbi nikiwa sijafanikiwa.
Ikabidi nirudi kulekule kwa jamaa aliponielekeza kwa mchizi mwenye jenereta.
Kama Mungu ile nafika naye jamaa ndio alikuwa anafungua,.tena umeme ulikuwa umerudi.
Na kweli nilipoongea na mchizi hatukuvutana sana mwishowe nilimuuzia kwa shilingi elfu kumi. Kutazama saa tayari saa sita mchana. Akili yangu yote ilikuwa kwa mke wangu Atuganile. Mbiombio niliwahi kwa mwendo wa kijeshi mpaka nyumbani huku nikiwa na nguvu mpya mbele ya macho ya mke wangu.
Lakini nilipofika na nilichokikuta sikuamini hata kidogo.
Moyo ulinipasuka macho yakishindwa kuamini..... Machozi yakaanza kunilengalenga huku pumzi zikibana na kutafuna kifua changu kwa mshituko.
 
SEHEMU YA 15

"Njoo!" Ndiyo sauti niliyoweza kuitoa kwa muda huo nikimwita mke wangu niliyemkuta barazani akiwa na yule dadaangu wa hiyari sambamba na demu fulani ambaye sikuwahi kumjua jina zaidi ya kumuona ona tu na nilimjua kuwa mcharuko. Niliwakuta wakiwa bize na story huku wakicheka. Mke wangu alikuwa amepakatia ungo wa mchele akichagua chuya huku wenzake wakimsaidia. Hilo lilikuwa jambo la kwanza lililoustua moyo wangu. Nilishindwa hata kusalimia na kupitiliza ndani.
"Umekula?" nilimuuliza huku midomo ikinichezacheza baada ya kunifata ndani. Atu aliogopa na kusogea mbali nami kidogo huku akivunja vunja vidole.
"Ndio mume wangu, wifi alininunulia chapati akachemsha chai tukanywa. Naomba nisamehe kama nimekosea mume wangu sirudii tena." Kwa sauti ndogo aliongea huku akiinamia chini. Nilishusha pumzi za aibiko na kumuuliza swali lengine.
"Sawa, na je ule mchele unaochagua wa kina nani?"
"Mume wangu mchele ni wetu ila dada na mwenzie wananisaidia tu ili niwahi kupika nilijua mume wangu umeondoka huna kitu na hujala ndio nikawa nakuwahishia."
"Nani kakununulia wakati nimekuacha huna kitu?" Nilimuuliza huku nikianza kuhisi kizunguzungu kinaninyemelea.
"Mchele nimekopa dukani kwa Mangi ila viungo nimemuomba dada amenipa."
Nilijikuta nauma midomo na kumtazama kwa mshangao mkubwa mke wangu huku nikiwa siamini kama kweli yeye amenitia aibu kiasi kile kwa njaa ya masaa kadhaa tu?
"Atuganile mke wangu! hivi una akili kweli wewe? Yaani unaenda kukopa mamii? Atu unaniaibisha mara hii hata miezi mitatu bado? Unataka kunambia ushazoeana hadi na wauza maduka eeh!" Nilifoka huku mchozi yakinitoka ingawa nilikuwa silii.
"Hapana mume wangu sio hivyo."
"Kumbe? kumbee vipi?"
"Ni wifi ndiye wanamfahamu nimekopa kwa jina lake yeye."
"Sio hivyo kabisa Atu. Ina maana yote niliyokuwa nakwambia juu ya mazoea ya namna hiyo madukani yalikuwa yanaingilia huku yanatokea huko si ndio..? daaah!"
Nilipiga ngumi moja ukutani kwa hasira ya fedheha niliyoanza kuiona mtaani hata mule ndani. Lakini mara mlango wetu ukagongwa na yule dada huku akiipaza sauti.
"Atu mamiii unaunguza nyama hukuuu."
"Nyama?!" nilishangaa zaidi.
"Mke wangu umekopeshwa hadi nyama? eeh!" Nilimuuliza tena Atuganile ambaye alizidi kubinya kucha na kusugua vidole vya miguu akichora sakafu huku akiwa ameinamisha kichwa na kuitika kwa ishara ya kukubali.
"Nani huyo aliyekukopesha nyama?"
"Buchani kwa babu lolo mume wangu nisamehe sikuwa na nia mbaya ila nilitaka kuona unakula vizuri leo." Huku naye akiwa uso umetapakaa machozi alipiga magoti kuniomba msamaha.
"Daaah! mke wangu!" Niliachana nae na kutoka nje kumwita yule dada.
"Da Mwajey nakuheshimu sana na huyu ni mke wangu wala si wako nakuomba tuheshimiane usimpelekepeleke vibaya kihivyo kumzowesha kwa wanaume samahani sana. Sasa vile vitu kula mwenyewe hatuna haja navyo na iwe marufuku kutoka na mke wangu pasipo ruksa yangu. Sitaki." Niliwaka.
"Hee! One umechanganyikiwa nini? kwani huyo mkeo mtoto mdogo hadi mimi niwe nampelekapeleka? hee! kama umeanza kunikosea adabu naomba usinitibue nyongo hee!. Kaa na mkeo umkanye naye asinisumbue kumsindikiza sehemu zake sitaki ujinga ujinga mimi ooohooo! chefuu..." Kejeli alizotoa yule dada sikuamini. Nilirudi tena ndani nikamkuta Atuganile kajilaza kitandani. Nilikaa pembeni yake mikono kichwani na kujiinamia kwa muda. Niliumia fikirani sikupenda hata siku moja tuwe watu wa madeni ama kudhalilika mitaani. Kilichoniumiza zaidi kuona mke wangu kwanini anachukuwa maamuzi pasipo ruksa yangu? Kwanini hajanisubir ama kunambia kama anataka kukopa!. Niliijua vizuri mitaa yetu ilivyo. Nilijua kitendo cha Atu kukopa kitazua hadithi mpya ya unafiki dhidi yangu mitaani. Sikuipenda aibu hii wala kuifikiria.
Nilishusha pumzi na kumshukuru Mungu kisha nilimkumbata mke wangu pale kitandani alipolala huku nikimpapasa kumfariji mpaka nami usingizi wa mang'amung'amu ukanichukua.
Kuja kustuka tayari jioni. Siku hiyo ikabidi twende wote kulipa madeni yale aliyokopa mke wangu huku nikiwatambulisha wale wakwale kwa mara nyengine kuwa yule ni shemeji yao, wamuheshimu wasimmendee mendee. Hakika kitu chengine kilichokuwa kinanisumbua ni wivu. Wivu wangu wa kumpenda sana Atuganile na kuhakikisha milele anabaki kuwa wangu tu. Ilikuwa fanya utani nami lakini sio kwa mke wangu. Chakula kile kilipikwa usiku na siku ikaisha huku nikiwa nimesamehe kilichotokea japo kuwa maneno ya Dada Mwajuma yaliustua moyo kinamna yalinipa maswali yasiyo majibu ingawa sikuyatilia maanani kivile.
Siku chache zilipita harakati zikiwa zinaendelea.
Nakumbuka siku hiyo zikiwa zimepita siku chache mke wangu aliniomba jambo.
"Mume wangu, kutokana na hali ilivyo nilikuwa naomba nifungulie walau mtaji wa kuuza maandazi hapa nyumbani ili tusaidiane pesa za ndani kuliko kukaa hivihivi." Wazo la Atu halikuwa baya kwa namna moja kimaisha, lakini halikuwa zuri kwa namna nyengine kwa upande wangu. Nilimkatalia kwa mara ya kwanza nikifikiria vitu vingi. Kwanza bado mapema sana tokea tufunge ndoa tena iliyogharimu pesa nyingi kiasi za kufungua biashara nzuri. Pili nilihisi aibu ya kuonekana maisha yamenishinda mapema. Tatu nilihofia inaweza kuwa njia rahisi ya kuzoeana na wakwale wengi hata wakamshawishi mke wangu akabadilika. Lakini kwa kuwa Atu mwenyewe hakuisha kubembeleza sana na kunitoa wasi huku akinipa maneno matamu ya Mungu. Hapo ndipo nikamruhusu kwa sharti moja. awe anachoma usiku ama alfajiri hayo maandazi kisha mimi ndie niwe naenda nayo kule kwenye 'game' siku umeme ukiwepo ama ayaweke kwa nje tu ya pale kwetu ila asiende kujichanganya na wauzaji wengine maeneo ya barabarani ama kupeleka dukani.
Alinielewa na kesho yake akaanza kufanya hivyo baada ya kumpa elfu ishirini na tano ya kuanzia mtaji. Hakika ilikuwa ajabu lakini kweli, ingawa alianza kwa unga mchache lakini maandazi ya Atuganile yaliisha haraka mno. Niliporudi ilibidi nimuongeze pesa na kuchanganya na pesa yake ya mauzo ndipo alipozidisha kipimo sasa. Aliuzia palepale nyumbani akifanya hivyo kwa siku mbili na mambo yalikuwa yanaenda vizuri.
Lakini daaah! Atuganile sijajua kama ilikuwa visa vya makusudi ama kichwa chake kilikuwa kizito. Kwa mara nyengine alifanya tena yaleyale ya 'haja' ingawa safari hii hakikuwa 'kinyesi' ila ilikuwa 'mikojo'. Haja ndogo yenye kuzua harufu kali ya muda mrefu na kuharibu rutuba.
Siku hiyo alipomaliza kuchoma maandazi yake asubuhi subuhi baada ya mimi kuondoka, aliacha kuyaweka pale nyumbani ndipo kiguu na njia mpaka dukani kwa mangi. Pasipo kunambia chochote wala kuniaga. Kwa bahati nami siku hiyo sikwenda mbali kitu ambacho hajakijua. Nilikuwa eneo ambalo niliweza kumuona alivyofika dukani na kuzungumza na mangi ingawa sijasikia mazungumzo yao zaidi ya kushuhudia akimkabidhi kidishi cha maandazi kisha akiondoka huku akichekacheka na Mangi naye alikuwa anajichekesha pale dukani. Moyo uliniuma kwa mara nyengine. Niliumia na kujiuliza.
"Ina maana haelewi ama?!....Atuganilee!?"
 
SEHEMU YA 16

Uvumilivu ulinishinda, dakika zilezile nami nilichapa mwendo hadi nyumbani. Ajabu sijamkuta na mlango wa chumba chetu ulikuwa umefungwa. Nilishangaa sana ikiwa nilimshuhudia mwenyewe akitoka pale dukani kurejea nyumbani.
"Ina maana hajafika? Kapitia wapi?" Nilichoka na kukaa chini pale mlangoni huku kijasho chepesi kikianza kunivuja hali ya kwamba ilikuwa asubuhi.
Niiganda zaidi ya masaa mawili pasipo mke wangu kutokea. Nilirudi ile njia ya dukani nikipita si chini ya mara mbili sijamuona. Nilienda mpaka bombani nako hakuwepo. Nilipiga simu yake iliita lakini haikupokelewa mpaka inakata. Nilipiga zaidi hata ya mara hamsini.
"Atuganile? hivi mke wangu yuko sawa kweli? daah!" Kidume nilizidi kuchoka na kunyekenyeka viungo. Lakini nikiwa sina hili wala lile mara niliisikia sauti kama ya mke wangu nyumba ya pili ikisema.
"Asante mama usijali nimekuelewa mamaangu."
Nilihisi hata utumbo kunitetema. Nilisimama na kujifuta vumbi la pale chini nilipokaa na kuzunguka nyuma ya nyumba kwenye uchochoro kujibaza huku nikibana pumzi na kufikiria nianzeje anzeje kumuuliza Atu kwa kumtega ili nijue kama kuna mchezo ulikuwa unaendelea ama ni presha zangu tu hajabadilika kitu?
Watu waliopita walinishangaa na kuendelea na yao. Nilisikia kwa mbali mlango wetu ukifunguliwa na baada ya dakika mbili mbele nilirudi nikijifanya ndio nafika muda huo.
"Waoo baby umewahi leo au umeme umekatika huko?" aliniuliza Atu huku akinikumbatia na kunibusu.
"Hamna baby vipi mbona maandazi siyaoni hapo nje yameisha nini?" Niliuliza kwa kumtega kana kwamba sijui chochote.
"Hamna baby tena nilisahau kukwambia mume wangu. Nimepata ushauri kuwa dukani ndio kuna wateja wengi wanafika pale hivyo nimemuomba yule mkaka amenikubalia niwe naweka pale maandazi ananiuzi jioni naenda kufata hela."
nilitetema hadi nnyongo kwa maneno ya Atu ambae kwanza hakuonesha kama amefanya kosa.
"Anhaa! kakupa nani hiyo ruksa?" nilimuuliza huku sauti yangu ikianza kubadilika na kuwa ya mtetemo wenye ukoromo kama mtu aliyekaukiwa koo kwa kiu ya muda mrefu. Hali hii ilimshtua kitu Atu na kubadilika kuwa mpole.
"Hapana mume wangu kama nimefanya kosa naomba nisamehe basi nitaenda kuyafata."
"Nijibu kwanza swali langu! ni nani huyo kum* aliyekushauri hivyo na kumsikiliza kama Mungu wako hata kunificha na kutii amri yake? Inaelekea hata siku akikushauri ulale na mwanaume tofauti yangu utafanya hivyo kabisaa si ndio eeh!"
"HAA! Jamani mume wangu?!"
"Ssshhhp! Atu hivi unanitaka nini mke wangu wewe jamani? Mbona unamkaribisha shetani kwenye ndopa yetu teketeke kabisa jamanii daah! Nimerudi muda mrefu haukuwepo hapa pia unaweza kunambia ulienda wapi? Atuganile! Hivi......" Nilishindwa hata kumalizia kauli yangu na kujikuta nakaa chini kabisa nikishindwa kujuacha kumfanya mke wangu kwa muda ule.
"Mume wangu nisamehe One wangu jamani, yule mama powa aliniita nikamsaidie kumuoshea vyombo leo alikuwa hajisikii vizuri. Nisamehe mume wangu nimeshindwa kumkatalia ndipo nilipokuwa." thibitisho lake hili lilizidi kunitafuna moyo kwa maumivu. Nilishamkanya mke wangu si chini ya mara moja juu ya yule mama na kumwambia vizuri tabia zake. Nilihisi kuanza kuumia na kuionja kwa kuiramba shubiri ya ndoa nikiwa sijui wala kufikiri kuwa kuna glasi nzima imeandaliwa kwaajili ya Ndoa yangu.
Sikumjibu kitu Atuganile zaidi ya kusali kimyomoyo nikimuomba Mungu anipe nguvu na moyo wa subira. Nilimlaani shetani niliyehisi anaanza kuinyemelea ndoa yetu ili aitibue amani ikosekane. Katika kitu ambacho nilijitahidi kukizuia ni kumfokea mke wangu ama kumpiga ingawa siku hiyo nilimwambia maneno makali kwa mara ya kwanza tokea tufahamiane miaka michache nyuma.
Alishuka pale chini na kukaa nami Atuganile akinifariji na kuniomba radhi. Nilijikaza na kufuta machozi ya hasira na kujitahidi kuziweka sawa akili zangu.
Nilisimama na kumnyanyua Atu wangu huku nikimtazama usoni ambapo naye machozi yalimtapakaa. Hakika alinionesha jinsi gani naye anaumia pindi niumiapo. Nilimfuta machozi na kumbusu kabla sijachukua biblia na nikamwambia tuishike kwa pamoja tufumbe macho tuombe. Moyo wangu ulinambia hakuna njia yoyote ya kumfukuza shetani zaidi ya maombi. Hakika siku hiyo niliomba zaidi ya saa zima kana kwamba nilisomea uchungaji au nilikuwa baba Askofu. Atu naye hakuwa nyuma katika kuitikia. Tulimlaani shetani na kuuomba ulinzi wa bwana uikinge maradufu ndoa yetu takatifu. Hakika baada ya maombi hayo nilijiona mpya kabisa nafsini. Nilisahau udhia wote uliotokea dakika chache na siku chache za nyuma.
Maisha yalisonga na nilimzuia mke wangu kufanya biashara ile baada ya kupata wazo moja nalo si lengine bali ni kuuza kiwanja kilichokuwa Mbezi ambacho nilinunua kwa msaada wa mama kabla hata sijamfahamu Atuganile. Kitu ambacho Atu hakukijua kama nina kiwanja tayari na nilishaanza kuchimba msingi wa nyumba. Akili ilinituma kama nitauza kile kiwanja basi nitafufua msingi mkubwa wa duka la nguo na hata kulipia deni la nyumba na kumpeleka chuo mke wangu ambapo tayari mwezi wa tisa ulikaribia. Mpango huu sikumwambia Atu hapo kabla wala sikuwa na haraka ya kufanya hivyo ingawa tulikubaliana na mama. Sikuwa na wasiwasi kuhusu kujenga hakika niliamini biashara zangu zitapoimarika basi hilo ni suala dogo kabisa.
Mwezi wa nane ukiwa unaelekea mwishoni kabisa kabla ya kuanza mwezi wa tisa. Sawa na miezi miwili tu ya ndoa yangu. Mtihani mzito zaidi uliikumba ndoa yangu. Hakika ilikuwa zaidi ya picha ya jakamoyo. Ubongo ulipoteza muelekeo wa kufikiri huku moyo ukishindwa stahimili maumivu. Niliuhisi mkuki wa moto ukinichoma katikati ya kifua changu. Daaaaaaaaah! hakika hapa ndipo nilipoanza kumeza funda la kwanza la shubiri ya ndoa niliyojimiminia mwenyewe pasipo kujua utamu wake.Usiombe kupenda sana ndugu msomaji. Mapenzi yanaumizaa mwanawaneee eeh! Usiwaone mabaunsa wakitembea barabarani ama wanajeshi vitani ukaona ni mashujaa kupitiliza. Hapana. Hakuna shujaa katika mapenzi. Huyohuyo baunsa ama mwanajeshi anaweza kutokwa machozi kama mtoto mdogo kwenye mapenzi hususani kwa mtu aliyempenda na kumuamini mno. Mapenzi yasikie tu usiombe kibao kikugeukie.
Nakuhadithia haya ili nawe ujifunze kupitia kila kosa langu na makosa ya Atuganile. Ukiwa mwanamme chonde chonde usije kuwa kama mimi pia ukiwa mwanamke ndio kabisaa nakusihi zaidi ya chonde, heri uwe shetani kabisa kuliko kuwa kama Atuganile.
 
SEHEMU YA 17

Ilikuwa majira ya saa mbili usiku siku chache baada ya yule dada wa hiyari Mwajuma kusafiri. Nilikuwa ndani natazama video huku mke wangu akiwa jikoni anapika. Siku hiyo mke wangu alikuwa na furaha sana mara kwa mara aliingia ndani na kutoka. Furaha yake haikunishangaza wala kunistua zaidi moyoni nilifurahi kila nimuanapo mke wangu ametabasamu huku akija na kunichumu. "Leo naona mke wangu unachati sana" Nilimuuliza baada ya kumuona kila akiingia ana simu mkononi akitoka anayo huku ikivaibrate mara kwa mara kwa ujumbe uliokuwa unaingia na kupokewa.
"Mama huyo baby anakusalimia sana. Vipi nimpigie uongee nae nini?" Aliniuliza huku akiwa ametabasamu.
"Hapana baby nitaongea naye kesho." Nilijibu kwa ufupi huku moyo wangu ukizidi kuchanua tabasamu na kuiona amani na tamu ya ndoa.
Lakini kuna muda sijui hisia gani zilinituma nikatoka ndani na kuelekea jikoni. Hata sijui nini kilinisukuma kwani sikuwa na jambo lolote la msingi lililonifanya niende jikoni. Nilishangaa kuikuta simu ya mke wangu pembeni ya jiko tena chini huku yeye akiwa ameelekea bafuni kuoga. Nilijiuliza kwanini aende kuoga halafu simu aache jikoni asiiache chumbani? Lakini nilipuuzia swali hilo na kuamini itakuwa ameisahau bahati mbaya wakati alipokuwa bussy kuchati na mama. Wazo lilinijia kuichukua kwa lengo la kuiingiza ndani kwa sababu za kiusalama. Kwanza jiko lenyewe lilikuwa kweupe mtu akipita anaiona, pili ilikuwa jirani na moto ambao unaweza kuwa tatizo la usalama wa simu yenyewe. Lakini wakati nainyanyua ilivibrate na kuonesha ujumbe umeingia tena. Kama ujuavyo simu za 'smart' ujumbe unapoingia unaanza kusomeka kwa juu ukipita kabla hata kuufungua.
Hapo ndipo moyo uliponipasuka baada ya kuusoma ujumbe husika ulipojipitisha kwa juu huku namba ikiwa ni ngeni kwenye simu ya mke wangu Atuganile.
'Basi powa nimekumiss my love usikose kuja.'
Ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo. Nilisimama kuutazama na dakika zilezile mke wangu alitoka bafuni na muelekeo wake alionesha mwenye kuwahi jikoni moja kwa moja kabla hata hajaingia ndani kuvaa hali iliyonitafsiria kuwa simu hakuiacha kule kwa bahati mbaya. Akiwa amejifunga taulo alistuka na kuishiwa nguvu machoni baada ya kuniona nimesimama mlango wa jiko nimeishika simu yake.
"Vipi baby!" aliongea kwa sauti ambayo nilimsoma kabisa kuwa ina wasiwasi ndani yake ila alizuga tu. Alinionesha kilichomuwahisha jikoni ni wali alioupalilia.
"Afadhali haujaungua mmh! maana nilikuwa naoga kwa wasiwasi nisije kulisha vya kuungua mume wangu." Alizidi kuongea Atu huku akiutoa moto aliokuwa ameupalilia kisha kuuzima na kubeba jiko juu yake kukiwa na sufuria ya ubwabwa akaelekea ndani moja kwa moja. Nikapiga hatua taratibu na kuingia ndani pia. Tayari nilishabadilika. Mwili unatetema midomo inanichezacheza baada ya kuigundua janja toto ya mke wangu na kuuhisi ushahidi wa wazi kuwa Atuganile kuna kidume kinamsarandia tena nilihisi kila dalili kuwa mtu huyo kakubaliwa japo sikutaka kuamini kama tayari kala mambo.
Niliipekuwa simu yake kuona hizo meseji alizokuwa anachati na mama lakini ajabu hakukuwa na ujumbe wowote kwenye simu ya Atuganile zaidi ya ule niliousoma. Hapo nilibaini kuwa kila ujumbe aliotuma ama kutumiwa alifuta baada tu ya kusoma.
"Mke wangu! huyu aliyetuma meseji kwenye simu yako mwisho 21 ni nani?" nilimuuliza huku nikijitahidi kuzuga kama nimejawa maumivu na hasira ya kuliwa vyangu.
"Jamani mume wangu sio mtu!"
"Sio mtu? Kwahiyo atakuwa nyani ama mbuzi eeeh!"
"Jamani baby ni rafiki tu wa shuleni tena mwanamke mume wangu usinihisi vibaya." alijitetea.
"Mwanamke? ndio akuite 'my love?"
"Jamani mbona kawaida mume wangu kwani kuna ajabu gani."
"Haya mpigie sasa hivi tumsikie."
Alinyamaza na kujimung'unya pasi kunijibu akiendelea kufanya shughuli nyengine hususani kupakua chakula.
"Mi naongea wee unafanya yako mke wangu adabu ya wapi hii? Naomba unijibu tena unambie kweli kabisa huyu aliyekutumia ujumbe na kukwita 'my love' tena akisisitiza amekumiss na usikose! ni nani na wapi huko usipotakiwa kukosa?" Kwa mara ya kwanza siku hiyo niliongea kwa sauti ya juu iliyoshiba ghadhabu kuliko siku zote alizowahi kuniudhi Atuganile.
Lakini kabla hajajibu kitu Atu akiwa kasimama akitetemeka mara ujumbe mwengine ukaingia kwenye simu.
"Vipi Hunny mbona kimya! nijibu basi nilale." Niliusoma na kuchukua simu yangu huku nikiiandika ile namba. mikono ilinitetema na midomo kuuingiwa ububu wa ghafla. Atuganile huyuhuyu kweli ama nilikuwa naota! Sikuamini ikabidi kupitia simu ileile ya Atu nikaipiga ile namba na kumpa.
"Haya ongea hapahapa Atu mke wangu tena usijiumeume neno." Nilichimba mkwala huku nikifunga mlango na funguo. Atu alitetema na kuichukua ile simu akaikata na kuiweka kitandani kabla upande wa pili hajasema kitu. Nilitamani kumpiga ngumi ya kichwa lakini ujasiri huo uliniponyoka na ngumi yangu nikaielekezea ukutani. 'Puu!" mkono ulichubuka na vijidamu kumeremeta ingawa sikuhisi maumivu wala kujua kwa wakati ule.
"ATUGANILE MKE WANGU UNANISALITIII?" Ndilo neno nililolitoa huku nikiichukua tena ile simu baada ya kuita na mpigaji alikuwa yule yule. Safari hii nikamkazia macho Atuganile kama si mimi aliyenizoea. Nikampa simu pasipo kumwambia kitu. Machozi yalimjaa usoni kilio cha aibu kikamponyoka huku akishindwa kuzungumza kitu ingawa aliweza kupokea.
"Halooo..Halloow baby!" Sauti ya kiume upande wa pili ilisikika ikiita baada ya kuona upande mmoja kukiwa kimya hakuna muongeaji.
Moyo ulizidi kuniuma kadiri nilivyothibitisha kuwa yule ni mwanaume. Nilimpora simu Atu na kuongea mwenyewe.
"Hallow mim ni mume wa Atuganile nani wewe?" Swali langu halikujibiwa zaidi simu ilikatwa. Kwa jaziba na hasira niliirusha simu simu na kuibamiza ukutani. 'Paaaaa' Ikaanguka na kupasuka. Atuganile alijikunja chini kwenye kona ya chumba jirani na ndoo za maji mikono kaziba masikio huku akilia. Nilimuacha na kufungua mlango kutoka nje nikiwa nimechanganyikiwa mara nikarudi tena ndani na kuvunja mlango.
"Atuganile mke wangu unataka kuniua na presha hivihivi si ndio? Nini nimekukosea mke wangu hadi uje unisaliti wakati wa ndoa? Eee Mungu baba ndoa yangu ndio kwanza ina mwezi wa pili mbona unanipa mitihani mizito hivi. Atuganile? Kama ulikuwa hutaki kuolewa nami ungesema nikuache huru mama na si hivi unavyonifanyia yaani daaah! Atu mama weeee!" Niliumia kwa kweli. Moyo uliniuma sana nikajipiga piga kifua kuutuliza mshindo wa moyo. Kwa mbaali nilianza kuuona ukweli wa maneno ya Sulu.
"wanawake vigeugeu hawa One! sio wa kuwaamini sana. Watu wanawinda kitaani na asikudanganye atakuwa mtaalamu wa kukataa kila siku, kila mara ama kila atayemtongoza."
Sauti hii ya Sulu nilipoikumbuka ilizidi kuuchoma moyo na kilio cha kwikwi kilibisha hodi. Atu alitulia palepale akishindwa hata kunyanyuka ama kunibembeleza kivyovyote. Sikumfanya kitu ila kwa mbaali nilianza kujifunza kitu kupitia maneno ya Sulu.
"Wanawake vigeugeu!" Moyo wangu ulisema. Lakini mawazo yangu na akili zangu zilivyorudisha kumbukumbu ya tabia zote za Atuganile tokea namfahamu mara ya kwanza jijini Mbeya! kichwa kilikataa kabisa.
"Hapana! hizi si akili za Atuganile! ama kuna mchezo wa kishirikina nafanyiwa ndani ya ndoa yangu?" Swali hili lilibaki kupelea akilini likihitaji jibu pasipo kuruhusu kauli ya moyo kuwa 'wanawake ni vigeugeu' Niliamini hata kama Sulu alisema hivyo lakini si kwa Atuganile. Atakuwa kigeugeu kwa wengine lakini si kwangu mimi. "Yaani hata miezi sita bado? Hao wataalamu wa saikoloji wanasema wanandoa wanaweza kuanza kuchokana kwa mapema mno basi mwaka mmoja ama miwili lakini si hivi.." Nilizidi kujiimanisha imani hii ili kuutuliza moyo ulioweweseka kwa shinikizo la huba na kubadilika kwa mke wangu.
"Mke wangu." Nilimwita Atuganile baada ya kimya cha muda mrefu kupita. Alinyanyua macho kunitazama pasipo kutoa sauti. Jicho lilimuiva kwa kilio cha muda mrefu. Huruma ilinivaa na kujilaumu kwanini nimemfokea Atu kwa kiasi kikubwa muda ule. Niliamini yule ndie chaguo langu sahihi. Mwanamke aliyejitoa kwaajili yangu. Ama kweli mwenye kupenda kweli huwa tayari kubeba kosa la mpenziwe liwe lake hata akamuomba msamaha yeye ingawa ndie aliyekosewa. Yote ni katika kuhakikisha ampendae haishiwi furaha wala faraja haimkauki machoni. Nilijikuta eti mimi ndiye ninayeomba msamaha.
"Nisamehe mke wangu, naomba kuwa na amani, mlaani shetani pakua chakula tule." Daaah! Hakika hata Atu mwenyewe alionesha kutoamini kama kweli amesamehewa kirahisi vile. Tena akiombwa msamaha!
Basi alinyanyuka na kujifuta machozi kabla hajapakua chakula na tukakaa pamoja kula. Ilibidi niweke cd ya Mr Bean na kutazama vituko vyake katika moja ya njia ya kuirudisha furaha. Nilijua kuwa mke wangu alipenda sana maigizo ya Mr Bean. Tulikula huku kila mmoja akichekea moyoni kadiri filamu ilivyozidi kwenda mbele lakini mwishowe tulijikuta tukianza kucheka kwa sauti ingawa bado tulikuwa tukitazamana kwa aibu aibu.
"Nakupenda sana mke wangu kesho nitakuachia simu hii mi nitabaki na ile ndogo usijali mamy kuwa na amani." Nilimwambia
"Halafu wewe je baby? hapana mume wangu mi nadhani tutumie tu hiyohiyo haina haja kuwa na simu. Mtu akinihitaji atapiga kwenye namba zako mume wangu ukiongea wewe ndio mimi baby." Aliongea huku akidekadeka baada ya kumaliza kula na kunimiminia juice ya parachichi kwenye glasi.
Tukiwa tunatazama vituko vya Bean wakati huo tayari ilikuwa saa sita usiku, mke wangu mwenyewe alijifungua taulo na kuvua nguo zake za ndani kabla hajajifunga kanga nyepesi na kujumuika nami sofani huku akinishika shika kimahaba na kuongea kwa sauti ya kichokozi muda wote.
"One ama kweli nazidi kuamini wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu milele. You are my everything baby i love you so much." Alideka Atu huku akinipekenyua pekenyua kwenye tracksuti niliyovaa na kumshikashika njomba nchumali wangu kiustadi kwa mkono wake mlaini huku akinitazama kwa macho malegevu kama anataka kukata roho. Kanga ilimfunguka na kutelemkia kiununo mwake. Matiti yake mazuri ya mviringo yaliyosimama wima yalianza kunichomachoma kifuani huku pumzi zake za huba nikizisikilizia sikioni. Alinisisimua kwa ncha ya ulimi wake wakati mkono wake mmoja ukiwa bado unauchua mkuki wangu kwa huba. Nilijikuta najinyonganyonga na kumshika kiuno mara nilistukia nimevuliwa track yenyewe na kubaki mtupu kabisa. Atuganile alianza kunifanyia utundu wa chumbani ambao sikuwahi kumuona nao wala sikutaraji kama alikuwa nao hata nikazubaika na kushindwa kujiuliza kaujulia wapi. Hakika wanawake ni warogaji wazuri sana ndugu msomaji usisikie. Ingawa wanaume tumewatawala sehemu kubwa kiuhalisia na kuongoza katika ujasiri hadharani... lakini kuna sehemu ndogo sana waliyotutawala wao ambayo inazidi kuwaweka kwenye ujasiri sirini. Ila ubaya unakuja kuwa ujasiri mdogo sirini wa mwanamke una nguvu ya kuudhohofisha ujasiri mkubwa hadharani wa mwanaume.
Hakika penzi alilonipa Atu usiku huo ilikuwa sawa na kutia kijiko kimoja cha asali kwenye pipa la shubiri. Aaaah! Atuganile! sikulilii wewe...Naililia Ndoa Yangu!
 
Huyu Atuganilee...!!!!

Nmetia nanga hapa madame
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…