Ndoa ya miaka 16 ipo hatarini kuvunjika kisa mtoto wa nje

Varbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,117
856
Rafiki yangu alinihadithia mgogoro kwenye ndoa yake japo chanzo nilipata kukijua miaka mingi iliyopita! Wakati rafiki yangu akiwa na miaka 19 alipata mtoto na msichana wa mtaani dogo enzi hizo alikubali lkn kumbe yule dada alikua na kadi mbili za clinic.

Baada ya raia kumtonya jamaa akasusa kila kitu na msichana akasepa na mtoto! Baada ya masomo na miaka mingi kupita rafiki yangu akaoa! Miaka mitatu ndani ya ndoa yule mtoto akaibuka na mama yake kumtafuta baba yake! Msimamo wa rafiki yangu ukawa bila DNA sihusiki na huyo mtoto! Kutokana na utata wa awali! DNA Ikafanyika results 99.9999% matching!! Rafiki yangu akaogopa kumwambia wife ambae tayari alikuwa na mimba ya mtoto wa kwanza! Akaona Ngoja amhudumie mtoto kupitia sister wake basi dogo kapiga kitabu na shule za uhakika Hadi mwaka huu anakwenda kuanza chuo kikuu.

Maneno yalikuwa mengi mke wake alisikia kua mumewe ana mtoto mkubwa zaidi ya yule alie naye! Jamaa akiulizwa anakataa kutokana na ukali wa mkewe! Sasa Siri imefichuka na mke anaona maisha yao yote yalitawaliwa na uongo! Anataka kuvunja ndoa!

Anaomba ushauri wenu afanyaje!? Now kijana yupo ana miaka 22 mwaka wa kwanza UDSM.
 
Kwann alimficha mke wake?

Na huyo mwanamke kwann anataka kuvunja ndoa? Jibu ni anataka kuvunja ndoa sio kwasabab ya huyo mtoto bali anahisi kuna maovu mengi yamejificha/amefichwa hapo cha mhimu ni mwanaume kufunguka ukwel wa mambo yote na mwambie sababu za yeye kumficha alafu amuache huyo mwanamke achukue mwamuzi atakayo ona ni sahih kwake, ayo maamuzi ndio yataonesha ukomavu wa akili yake
 
! Sasa Siri imefichuka na mke anaona maisha yao yote yalitawaliwa na uongo! Anataka kuvunja ndoa! Anaomba ushauri wenu afanyaje!? Now kijana yupo anamiaka 22 mwaka wa kwanza UDSM.
Wamechokana tu hamna lolote, huwezi kuvunja ndoa kisa mtoto tena ambaye ni mkubwa kuliko umri wa ndoa. Ni ujinga, wapeane tu muda
 
Wanaume wa kinondoni ni bure kabisa
IMG_20210928_225926.jpg
 
Kwa zama tulizopo,
Ni aibu sana kwa mwanaume kulilia ndoa,

Ndoa zipo kwa ajili ya kuwasitiri na kuwaheshimisha wanawake,

Wanawake ndio wanapaswa kuzipigania na kuzilinda ndoa zao kwa nguvu zote,

Wee mwanaume kazi yako ni kutimiza tu mahitaji yao ya msingi na ya ziada ili maisha yaende vizuri.

Ukiona mwanaume analia lia kisa ndoa inataka kuvunjika, Jua hamna kitu mule.

MWANAUME MSIMAMO BHANA, HATA KAMA NIMEKOSEA KIASI GANI LIWALO NA LIWE.
 
Ni aibu sana mwanaume kulilia ndoa,

Ndoa zipo kwa ajili ya kuwasitiri na kuwaheshimisha wanawake,

Wanawake ndio wanapaswa kuzipigania na kuzilinda ndoa zao kwa nguvu zote,

Wee mwanaume kazi yako ni kutimiza tu mahitaji yao ya msingi na ya ziada ili maisha yaende vizuri.

Ukiona mwanaume analia lia kisa ndoa inataka kuvunjika, Jua hamna kitu mule.

MWANAUME MSIMAMO BHANA, HATA KAMA NIMEKOSEA KIASI GANI LIWALO NA LIWE.
Ngoja waje MADUNGAYEMBE humu yatakavyotoa povu.
 
Shida iko wapi? Mwache avunje

Mtoto aliye mkubwa zaidi ya wanae wote Ana shida gani?

Ila haya maisha ni noma nna mjomba wangu Ana watoto wa 3 wakubwa (zaidi ya miaka 30+) ila mke (shangazi) ye anamfahamu mmoja tu.
 
Uyo jamaa ako hamna kitu kabisa,

Hivi mke anaanzaje kua mkali kwa mume wake?

Yaani anaanzaje anzaje kwanza?

Anakua anafoka, anampiga makofi au anakua anafanya fanyeje mkuu?

Yaani huo ujasiri wa kua mkali kwangu anautoa wapi kwanza

Nnachokiona apo,
Hiyo ndoa iko dominated na mwanamke.
Uyo mwanaume sio bure kuna kitu amelishwa.

Sisi wanaume wa kiafrica hatujaumbwa laini laini hivyo aisee.
 
Ngoja waje MADUNGAYEMBE humu yatakavyotoa povu.
Mwanaume kukosa msimamo ni hatari sana kwa afya ya ndoa.

Uyo mwanaume kiazi sana.

Uku kwetu,
Taratibu na mila zinasema ukija kuoa mke upate ruhusa kutoka kwa mke mkubwa.

Ila Babu zetu enzi hizo walikua wanatoa tu taarifa kwa wake zao kua
"wiki ijayo naongeza mke"

Hiyo inakua ni taarifa na sio anaomba ruhusa, Na ni haina discussion.

Ukiona hautaki mke mwenzio, kung'uta matako urudi kwenu.

Na unalazimishwa kabisa kuhudhuria, na kushiriki shughuri zote za kusherehesha ndoa ya mumeo kuongeza mke mwingine.

Sasa,
Sijui wanaume wa sikuhizi wanafeli wapi kwenye suala zima la kuonesha misimamo .

YAAN Mwanaume unakua laini laini utadhani wewe ndio umeolewa.

HII NI AIBU SANA KIUKWELI.
 
Back
Top Bottom